Nilikuwa na dreadlocks nilizotunza kwa miaka 9.
Nilizianza kwa mahaba, kwa kugharamiwa mno.
Nywele ilikuwa traaaam ileeee.
Nywele ilikuwa inapeeeendwaaa ileeeee.
Kuna kipindi I went through hell, vuruuuuugu, mapito ya kiwehu haifai.
Katika kitu nilijua nikikiondoa kitanipa mtazamo mpya juu ya maisha, mapenzi , mwonekano binafsi ni kuondoa zile nywele.
Nilitaka kudare kufanya kitu nilikwishaapa sitakuja kufanya. Hata iweeeeje.
Nilitaka kuvuka duara langu la uthubutu.
So it was a dare or die decision.
Dreadlocks zenye budget ya si chini ya 100K kwa mwezi, bidhaa za kuzitunza, uzuri wa ile nywele.
Halafu miaka 9, zilikuwa ndefu, Nene, rangi nyeusiiii, nzitooo, yani traaaam.
Siku nikatoka kazini, paaap!
Nikapita saloon.
Nikazikata ,nikaweka dawa, nikaweka rangi.
Wakati nazikata waliokuwepo saluni najumbuka mmoja alilia, alikuwa Radhi anilipe njsikate.
Ila kulikuwa hakuna kitu nilitamani kufanya for my inner peace kama kukata zile nywele.
So I cut them off.
Na nilizjkata kata kiasi hazikufaa kufanyiwa chochote.
I just wanted to end its era and everything.
Usingizi niliolala hiyo siku anajua Mungu.
Nazikumbuka sometimes, ila sijutii.