Mke wangu anadai niifukuze familia ya kaka nyumbani

Mkuu hongera ila angalia mipaka ya ukaribu...kukujali si lazima aje na night dress.na ukitoka naye kupata bia mchukue na mkeo

Sent from my TV
 
Mkuu Kuwa ''MWANAUME"....kweli unampenda kaka yako,,, na ni jukumu lako haswa kuitunza familia yake hasa watoto....chunga sana,,, mkeo keshaanza kuwabagua...kisa gubu la bi mkuwa(shemejio)....na wewe ushaanza kunoa kisu umfanye asusa...kuwa makini kaka....ukigonga tuu mimba.......mtafutie mradi afanye.....mkeo mzingue kidg....akitishia mwambie aende zake....anabip tuu....ila kumbuka undugu hauishi....ndoa huvunjika.....kaka yako ni muhimu sana...tunza watoto wake....ikishindikana mwambie shemeji arudi kijijini....
 

Ashamtafuna anajikosha to coz mwez uliopita wife alitonywa na wambea shemeji ametoa mimba na hela ilitumwa kwa daktar kutumia cmu ya mume ... Cjui kwa nn anaomba ushauri huku anaficha haya

Sent using Jamii Forums mobile app

nadhani una mengi ya kutujuza ila ni vyema ungeyaweka wazi maana kuna watu tayari wameishamuhukumu mke wa jamaa kuwa ana roho mbaya.
 
Huyo mke wako n matatizo sana, angekuwa anatekeleza wajibu wake kwako shemeji yako asingepata nafasi ya kutekeleza mambo hayo.

Lakin pia utani wa kumuita mume wangu, "mume" I don't entertain!!!!

Ila mh!!! Can't say too much!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkeo ana roho ya uchoyo hilo la kwanza. La pili ,hajui wajibu wake kwenye ndoa. Vitendo anavyokufanyia shemeji yako vilimpasa kushtuka na kujua wajibu wake kama mke kwako.

Wanaume mara zote tunapenda kuheshimiwa ,sio kosa lako kupenda treatment unayopewa na shemejio.

Kaa na familia ya kakaako ,undugu ni kufaana na sio kufanana. Kutunza familia mbili sehemu tofauti kutakuongezea mzigo mkubwa zaidi kimaisha. Be a man and lead your family wisely.
 
Hela ya kumpangia huna mtafutie mtaji ajishughulishe miaka ya kuwa mke wakukaa ndani kama pambo imepita akachakalike apate pesa kujikimu sio akutegemee asilimia [emoji817]
Mwambie awe na mipaka kupakuliwa chakula kama mkeo hajui umuhimu wake yeye pia haimuhusu usikute atayeye mmewealikuwa hafanyi anavyokufanyia bali anataka apandikize hila umuone mkeo mbaya
Ukimtoa out mwambie asifnye majukumu ya mkeo kwani mmeshazoeshana hivo
 
MKUU, MWAMBIE SHEM WAKO APUNGUZE MBWEMBWE, AACHE KUKUKARIMU MITHILI YA MUMEWE, KAZI HYO AMWACHIE MKEO

HALAFU JINSI ULIVYOSMULIA KAMA UNAMTAKA SHEMEJ YAKO HV, AHAHAHA

USICHOKE KUZUNGUMZA NA MKEO NA KUMTIA MOYO KUWA HUWEZ TEMBEA NA MKE WA KAKA YAKO

KILA LA HERI THEN
 
huyo shemeji yako nae ni mtata aache kujishauwa katika ndoa za wenzie mwenye nyumba anaanzaje kujishusha kwake sasa?! nae anapata nguvu kabisa ya kusema kujishusha haweza kama vipi ukampangie chumba. anachekesha akae tena atulie yaani kama hayupo hiyo nyumba ni ya mwanamke mwenzie mwenye mume yupo kisa cha yeye kukimbilia kukupakulia vya nini sasa tena nae kamkuta mkeo kama mpole, ingekuwa mie shemeji yako ungemkuta kijijini kwao
 
Damu nzito kuliko maji, hao watoto ni wa ukoo wenu, usiwatupe. Kuwa kama mwanamme, toa tamko kama hawezi kukaaa na shemeji yako aondoke aende anakotaka, huenda ana jamaa nje ndio kiburi. Na ww kwa nini usimtimizie huyo shemeji mahitaji yake ya kimwili? Yaani mpaka uoneshwe nn ndio ujue anahitaji? (duuu wanaume wa dar bana). Tafuna bana!
 
Hongera ila mwambie mpambe (shemijio) asiwe na mbwembwe za kupitiliza kuliko mwenye mali (wife wako) maana nikionacho hapo ni wivu wa kawaida kwa mwanamke yeyote yule huwa hapendi kuzidiwa,yaani shemeji yako anatoa huduma kumzidi mkeo hivyo hiyo hali inamkasirisha mkeo (ANA HAKI YA KUKASIRIKA),angalia sana asije kukuchonganisha na kakako maana hashindwi kufunga safari mpaka gerezani kumueleza kua unatembea na mkewe na baadae Mkaja pimana DNA bure kwa ugomvi huko mbeleni.
Panapo wakibwa hakiharibiki kitu waite wazee wawili watatu muyazungumze na huyo shemejio aambiwe ukweli tu, afanye yanayomuhusu hiyo kazi ya kupakua chakula na kukufungulia geti wala si yake!! Atulize kipapa chini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo dada anachofanya ni kama kumshukuru shemeji yake kwa mema anayomfanyia yeye na watoto wake!!! Ebu tuache kuwa na negative perceptions.....unafikiri kuishi nyumba ya watu ni kitu rahisi eeenh????
 
Ila mwambieni ukweli shemejie nae kazidisha,unajua unapofika kwa watu unatakiwa Ku behave kwa mujibu wa maisha aliyoyakuta sasa na yeye huyo bi Dada kazidi kujitia tia kwa shemejie,kujikalisha sebuline na night dress kwa shemeji yake si picha nzuri,ipo siku jamaa yenu hapa ataja sema shetani alimpitia,yeye kama baba anatakiwa kiyakemea yote mbaya ili hao wanawake waishi kwa amani humo ndani sasa akiwa lege lege tutarajie ipo siku atateleza tu maana speed ya shemeji si ya kitoto wallah,kumpakulia chakula mume wa mtu inauma jamani wee! Mimi kwa kweli sitaki kabisa hiyo kitu bora mwanaume apakue mwenyewe maana kwenye kuinama kuvuta hotpot waweza pitisha vijimaziwa vyako kwa bahati mbaya kwenye mkono wa mume wa mwenzio mambo yakawa hovyo hovyo!
NYUMBANI KARIBUNI ILA MKIFIKA KAENI MBALI NA WAUME ZA WATU.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkeo ana matatizo ila na wewe nae unamtoaje out shemeji unamwacha mke?
 
Hii ndo maana ,,katika uchaguzi wa kuoa nilazima uangalie sifa za nje kwanza .....binafsi napenda mwanamke kwanza apende watu sana ndugu jamaa namarafiki kisha apende kula
 
Hii ndo maana ,,katika uchaguzi wa kuoa nilazima uangalie sifa za nje kwanza .....binafsi napenda mwanamke kwanza apende watu sana ndugu jamaa namarafiki kisha apende kula

Napenda kula mimi jamaniii
 
1.Hongera sana kwa kumfadhili kaka yako aliyepo matatizoni, huo ni uanaume.
2.Wanawake wakikaa pamoja ni desturi yao kutoaminiana.
3. Mpangishie shemeji yako mpe na mtaji ili azalishe pato lake.
Huyo shemeji yako anataka kuvunja ndoa yako !! Yeye hapo ni mgeni amekaribishwa tu, kwa kweli huyo shemeji yako anakutaka ila anashindwa kukuambia sasa anakwambia kwa vitendo, ataivunja ndoa yako kua mwangalifu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna tatizo sehemu,tena kubwa,tatizo ambalo ww unazidi kulikuza na mkeo anazidi kukusaidia kulikuza..

tuanze na wewe,kwa nini wewe mke wa nduguyo anavaa nguo ya kulalia na anakaa sebuleni mbele yako bila ku hukua hatua ya kuzuia hali hyo?
Kwanini anakuandalia chakula na hulalamiki kila siku na umeridhika?kwa nn unaenda kuka nae bar bila mkeo?

Tuje kwa mkeo,je kwa nn amekasirika wkati hafanyi jukumu lake kwako?kwa nn mnafundishwa na hyo mgeni lakin wote ww na mkeo mmeshindwa kujifunza?unashindwaje kufundishana ndani chumban hali halisi ilivyo na mkeo ajifunze?kwa nn kila siku aridhike ww mumewe uandaliwe chakula na mke wa nduguyo na yy yupo ndani?kuchelewa kwako kurudi nyumbani hakuhalalishi kutokulala kwao mapema,je mkeo hana namba yako ya simu umpigie au akupigie mfungulie geti?upo serious kwel na ndoa yako bro?

Shemeji je anaona nafany heshima lakin ameshindwa kugundua hapo sio kwake na yte anayokusaidia hayastahili kwa sasa?ameshindwa kujua ww ni mume wa mtu na yupo kwa watu?anashindwaje kumwelewesha mkeo cha kufanya kam mkeo kajisahu?
Au bro unataka kumega kisela sema tu unashindwa kuanika hapa jukwaani?au ushamega?

Kuna tofauti kubwa kati ya mjinga n mpumbavu,mjinga anajua ila anajua vibaya,ila mpumbavu hajui kabsa na hajui kua hajui.. Utachagua kupi kunakufaa hapo...na kipi bora kwa faida yako na familia yko. Ita wote usimame kiume tabia hii huipendi na isirudiwe. Mkeo kamkanye chumbani kwamba afanye kam shemeji yako anavyofanya. Tchao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…