sitaki kujua umri wa mleta mada maana wengine wanaweza kuwa watu wazima lakini ovyo, ukubwa sio umri ni busara na ustaarabu.
lakini pia anaweza kuwa ni mdogo wa fikra,nimemsikitikia sana. hawa ndio wale wanaweza hata kuweka picha za wake zao wakiwa wanado.
We si mme kitu anayeweza kutoboa siri za ndani hasa kitandani. Kwani wewe hujambi hata kama siyo sana? Siku utakapoanza kujamba wewe sijui itakuwaje? Ulitaka apige miayo sana kama alama ya kutopata lishe la kutosha? Rudi jandoni ujifunze maana ya unyumba.
wewe inaelekea hujakaa jando na kufundwa.si kila unachokiona kwa mwenza wako basi ukitoe hadharani.kwa tabia yako hiyo mbaya kamwe huwezi kabisa kukaa na mke.badilika sasa ufaidi ndoa yako.
Pole sana, labda anaelekea kupata mwili huyo. Lakini namna ya kukusaidia wewe ni kumshauri mkeo asilale kifudi-fudi (yaani hasilalie tumbo) ingawa hili linaweza kumtesa kama amezowea kulalia tumbo. Pili aangalie vyakula alavyo visiwe vyenye gas sana kama maharagwe fulani fulani...
Lakini kikubwa siyo tatizo labda inakuwa ni tatizo kama akijamba vyanuka/kunukia hapo ndipo taabu. Pole sana
hahahahah nipo shift this night bt nmecheka sana hahahahh wew mi naic mkeo anakula sana maharage,jarbu kupunguza ratiba ya maharage na kande hme kaka,yaezkana hata watoto wanapiga kama vitu vya maza hahahahhh
Mpeleke kwa wataalamu wa afya kwanza.Wakishindwa wanadamu,itakuwa amevamiwa majini au mapepo ambao wanatolewa kirahisi san; kwa njia ya maombezi pale kwa askofu Kakobbe au mahali popote kwenye huduma za maombezi kwa jina la Yesu Kristo !!!
Jamani acheni kumshambulia huyu kijana. Mlitaka matatizo yake ayapeleke wapi? Hapa si ndio mahala sahihi, jukwaa la madaktari? Acheni ushamba bwana, hauwezi kwenda hospitali unaumwa mguu, halafu uogope kutaja ugonjwa wako, ama uanze kutumia mafumbo, utaeleweka kweli?
Kujamba si ugonjwa, umesababisha wewe kwa tigo zako, ni kwa vile kukuheshimu tu angekushitaki kwa njumbe ukome ubishi. Kwanza adabu gani kunsema nkeo kwenye ntandao? Wewe pia wajamba lakini anakukong'oli kwa jicho tu. Ukiona kajamba sana siku hiyo anataka urudie tena. Ni tangazo rasmi kati ya wapendanao.
Unajua hivi vizazi vya .com tabu kwelikweli. Kujenga nyumba huchukua muda mrefu na kuibomoa huchukua muda na katika mapenzi ni hivyo hivyo. kama kweli unampenda mwenza wako kumlinda nilazima kwani mnapokua mwili mmoja maana yake ni kuwa aibu yake ni yako na siri yake ni yako ugonjwa wake ni wako na wako ni wake. Maisha ya ndoa siomajaribio majaribio ni kipindi cha uchumba mwanamke au mwanaume mpaka anapoamua kukuoa au kuolewa ina maana kuwa amekuamini sana kitu cha kujikumbusha ni kwamba ijapokuwa wanaume wanafikiri kufanya mapenzi kwanza ndipo wapende wanawake wanapenda kwanza ndio wafanye mapenzi(hapa naongelea kwa wanaojiheshimu siongelei vodafasta). utakuta mwanaume unakula chakula mkeo alichokuandalia unaanza kukiponda chakula gani hiki hakina ladha umepika vibaya badala ya kutumia lugha nzuri kufikisha ujumbe kwani mkeo au mumeo ndiye rafiki yako wa karibu sana kuliko mtu mwingine yeyote. Maneno kama Pole samahani nisamehe ahsante ni magumu kutamkika lakini yana maana sana.
Mimi katika kukua kwangusijawahi kuona mama na baba wanagombana sio kwamba hawagombani ila baba aliwahi niusia kuwa maranyingi itokeapo mmegomba na mkeo hakikisheni watoto hawajui kwani mara nyingi watoto wakiona baba anagombana na mama watamuonea huruma mama na wakati huo huo watamchukia baba. Ugomvi hautakuwepo kama mnaheshimiana na kujuana tofauti zenu ina maana kipindi cha uchumba ambapo watu wanatakiwa kusomana na kujuana wao ni kipindi cha kufanya starehe tu. hii huwafanya kuingia kwenye ndoa bila kujijua mapungufu yenu na jinsi gani mtatatua matatizo yenu. Lakini kwanini mgombane kama mnaishi kama marafiki wakaribu na wakati mwingine mnataniana na kama ikitokea mnagombana kama mke anaongea kwa sauti ya juu kwa hasira au mume basi kumbatianeni na mmojawapo ashuke chini ili kumfanya mwenzake kurejea katika hali ya kawaida baada ya hapo ongeeni matatizo yenu na mtatue tofauti zeno kwa amani na upendo. Hata kama mmegombana mkisikia mtu anapiga hodi sahauni tofauti zenu jengeni nyuso za furaha kumkaribisha mpiga hodi mkionyesha sura si nzuri aliyewatembelea ataona kama hamfurahii ujio wake wakati yeye kaacha shughuli zake kaja kuwa sabahi. Sema ahsante kwa chochote utakacho fanyiwa na mwenza wako neno hili hufariji sana.
Hivi Leo mwanamke au mwanamme anakaa kwa marafiki zake akiulizwa habari za nyumbani yeye anamponda mkewe au mumewe badala ya kumsifia kwa mazuri yake. Leo hii mtu anaongozana na mkewe au mumewe barabarani anapita mwanamke au mwanaume anaanza kumsifia kuwa mwanamke yule au mwanamme yule ni mzuri.
Kumbukeni kuishi na watoto wenu kirafiki zaidi na jitahidini wasione chuki yeyote toka kwenu wazazi. Wanaume wenzangu huwa tunajisahau mtu unamaliza wiki mmoja nzima mtoto hajawahi muona baba tenga muda wasaidie watoto homework wananulie zawadi wafanyapo vizuri darasani vile vile tumia muda kuongea nao na kutaniana nao hii itawajengea kujiamini na wepesi wakukueleza jambo lolote kwa urahisi usisahau kuonyesha upendo kwao ukifanya hivi watoto watajiwekea mazingira ya kutotaka wakuudhi hivyo watajitahidi kufanya utakalo. Ikitokea watoto wamekosea waonye na uwaeleze kwanini hilo ni kosa madhara ya kosa lenyewe na wanatakiwa wafanyenini kujirekebisha ongea nao kirafiki zaidi waweza kuwa mkali lakini ni inapobidi sio kila kosa wewe mkali. Jua na timiza wajibu wako kama mke au mume saidianeni kazi ndogondogo kwamfano mke ananyonyesha sio mbaya ukasaidia kufua nguo au kupiga pasi au kazi nyingine yeyote unayoona inafaa wakati mwingine mkeo naye ni binadamu anachoka. Ni marufuku nguo zako au za mkeo zikanyooshwa au kufuliwa na hausi girl kwa mfano nikivaa nguo imenyooshwa vzr mfanyakazi mwenzangu akinisifia ilivyosafi then fikra zitakwenda kwa aliyeifua na kuinyoosha. Kaguaneni kabla hamjatoka ndani kwenda kazini.
hasira hasira hasara mke na mume wanapokuwa wote na hasira shetani hukaa katikati kuwafanya mchukue maamuzi na ndio maana maamuzi mengi yachukuliwayo wakati watu wakiwa na hasira huwa ni maamuzi mabaya na mkitulia mnaanza kujutia mfano maamuzi mabaya ni pamoja na kupigana kwa sababu ya hasira.
La mkeo au mpenzi wako ni lako nashangaa kizazi hiki eti mtu anaenda kumfumania mwandani wake kwa kuchukua polisi waandishi wa habari na kupiga picha kuziweka magazetini baada ya muda wanakuja kusameheana na kuishi pamoja. Tukumbuke utu wa mtu unaendelea kubaki na thamani ile ile kumdhalilisha mwanandani wako ni kosa kubwa sana kwani ni kama umejidhalilisha mwenyewe na kujikomoa mwenyewe kwasababu nyie ni mwili mmoja mbaya zaidi unajijengea chuki kwako na watu wanaokuzuka na unajidharaulisha wewe mwandani wako na wanao
Tukumbuke tu kuwa Maisha ya ndoa sio majaribio ni kutenda kwa hiyo timiza wajibu wako kwa maisha ya upendo na furaha kwani furaha hukufanya uwe na afya njema. Kumbuka hakuna mtu hatari katika maisha kama akuandaliaye chakula anaweza kukifanyia chakula vyovyote vile kikaweza kukudhuru ikiwemo kukuwekea madawa au sumu. Ila Mungu aliliepusha hili kwa kuumba upendo na ndio sababu ya tofauti kati ya mwanaume na mwanamke Mwanaume anatamani kufanya mapenzi kwanza ndipo Upendo hufuata wakati Mwanamke anapenda kwanza ndipo anatamani kufanya mapenzi na wewe. Tuwape upendo wa dhati wake/waume zetu kuepusha matatizo ya familia na kuyumba kwa familia
Maisha ya ndoa ni kama Muwa................................................... hivyo tuvumiliane kwani hakuna binabidamu aliyetimilifu kwa kila kitu
EE M.Mungu tujaalie upendo wa dhati na tuepushie mabalaa
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.