Mke wangu anamtesa sana mtoto wa marehemu dada yangu

Yaan mtoto wa miaka nane anamtesa hivyo jamani
 
Ni roho mbaya tu ya mke wa jamaa mbona hata hao wazungu wanaasili/adopt watoto?
 
Kweli mwenzetu kazingua.

Nje ya mada....hivi kumrudisha mke kwao ni adhabu ama zawadi? Hili zali natamani linikute halinikuti sijui kwanini.

Wake zenu huwa wanaogopa kurudishwa kwao? Duh sijawahi pata feeling ya hivyo.
Ukirudi kwenu vile vijamaa vinavokutongozaga vitakoma... Nyumbani kwenu itakua aibu kuanzia kwa wazazi mpaka wewe mwenyewe.. that's how it will feel

Hivo basi ni adhabu plus aibu divide by huzuni. Na pia mimi sina mke hivo sijui kama wanaogopa ila lazima waogope
 
Ni roho mbaya tu ya mke wa jamaa mbona hata hao wazungu wanasaili/adopt watoto?
Of course ni roho mbaya, lakini mtoto kuendelea kukaa hapo ni hatari zaidi na anaweza kupoteza hata familia yote asipokuwa makini
 
Of course ni roho mbaya, lakini mtoto kuendelea kukaa hapo ni hatari zaidi na anaweza kupoteza hata familia yote asipokuwa makini
Sasa si jambo zuri kuruhusu ubaya ushinde , angetimua tu huyo mke au abaki na mke tu na watoto Ila maisha hiwa hayako hivyo
 
Huu upuuzi ndo nilishakataa. Eti nigombane na mke halafu atishie kwenda kwao. Ataondoka mda huo huo. Mke wa mdogo wangu alikuwa na hii tabia ya kumtishia Sana mdogo wangu wakigombana anatishia kuondoka kwenda kwao.

Sasa siku Moja nikaendapo nikawakuta mama mkwe, mashangazi na dada zake wamemuweka kikao na wamembana kweli kuwa anatesa Binti Yao. Aisee nilibadilika na kuwa Simba Kwa ule upuuzi. Nilichomwambia mdogo wangu alingia ndani na kubeba begi lake la nguo make ndo alikuja nalo tu. Waliondoka na Binti Yao hapo hapo. Nikamwambia msimamo wangu ni huo. Nikamwambia Dogo tulia niachie huu msala. Nikiwafukuza wote. Bada ya mwezi walimtafuta Mzee wetu kusuluhisha huu msala. Alivyorud hajawah Tena kufanya huo ujinga na ametulia Sana na kuwa mama Bora.

Hawa vuimbe huwa wakishakuona boya watafanya ujinga sana.ila wakikukuta umenyoka huwa ni wazur sana
 
Halafu kaka zetu kuna muda mnatufelisha sans, hiki kitu sio cha kuomba ushauri!!

Wewe ni Baba, kichwa cha familia kuwa na maamuzi ya kiume
Kuomba ushauri kwa wengine siyo kosa.

Ushauri unaotolewa na wadau, saazingine unaweza kuimarisha maamuzi yake.

Watu wanaomba hadi ushauri wa 'kugonga' na wanapewa, sembuse huu ushauri wa kujenga?
 
Cha kufanya kwanza fukuza huyo mwanamke aende kwao yeye pamoja na ndugu zake wote waliopo hapo. Yani unampa taarifa jioni na wanaondoka asb wote. Hii itawapa funzo kubwa yeye na ndugu zake wote.

Hakikisha haondoki na mtoto wako yeyote na dada wa kazi abaki asiondoke. Alee watoto wenu. Maisha yaendelee

Usimrudishe huyo mke wako mpaka aombe msamaha tena ule msamaha kweli kweli. Atume na wazee kabisa. Yani mwache kwao hata six months hivi. Usimtafute wala nini mwache yeye ndio ahangaike kukutafuta. Hapa inabidi uwe na roho ngumu na uasume kama keshafariki ili maisha yako yasikwame.

Mwisho mkubalie kurudi baada ya miezi 6 kwa masharti unayotaka wewe. Sharti mojawapo ni kukataa ndugu zake. Arudi mwenyewe tu.

Mwisho weka Camera CCTV hapo nyumbani nje na ndani uwe unaangalia yanayoendelea nyumbani ukiwa kazini.

Akirudia tena kumnyanyasa huyo huyo mtoto mpe talaka huyo hakufai. Huyo anaweza kukuua hata wewe, huyo sio binadamu.

Kaa na mtoto wa dadako usimuondoe wa kuondoka ni huyo mwanamke. Pambafu kabisa, shwain
 
Hawa wanawake wapumbavu kiasi hicho huwa mnawaokotea wapi, kweli mwanamke anakutishia ataenda kwao na wewe unamwangalia tu. Kuna namna amekupanda kichwani. Pole yake sana huyo mtoto,
 
Sasa mke ndio umkute naye ni Director wa BOT au Lawyer fulani, na nyumba mlijenga pamoja na yeye alitoa nyingi kuliko wewe, boss utaondoka wewe na wageni/ ndugu zako Labda kama unaongea wale mliowatoa kijijini
 
Ukweli kutoka moyoni kama sio chai unatunywesha hapa ila kama ni kweli basi hapo huna mke rafiki una lipepo ndani , mwanamke ndio alitakiwa awe na roho nzuri kuliko wewe ila kama yeye ndio hawezi kukaa na nduguzo huyo ni mnyama timua mapema sana ataleta shida kubwa na weka ulinzi wa maana juu ya huyo mtoto
 
Umekaribia kumaliza mkuu. Ujinga wa aina hii haupaswi kulelewa. Ni lazima baba asimame kama baba.
 
Hiyo ni dalili unaishi na adui...Kumbuka anavyofanya ashindwi kuwafanyia wanao..
Ngumu sana kumuacha lakini ishi nae kwa tahadhari{Keep my words}
Huyo dogo miaka 8 ni mdogo sana.. Mpeleke walipo ndugu zake alafu peleka matunzo....
Dogo akikisha haji kuwachukia wanao..
 
Huyo mkeo afanyayo anahisi ataishi milele?
Siku akifa yeye watoto wake wafanyiwe vivyo hivyo?
Kamuulize haya maswali.
 
Duh...aibu? Hakuna aibu yoyote ni vile mtu atakavyojichukulia mwenyewe. Nadhani inategemea na kwenu kupoje na jinsi mke alivyolelewa kiuoga uoga.
 
Hilo ndio chaguo lako na ushazaa nae watoto wawili utakapomuacha fikiria mustakabali mzima wa watoto wako na wewe , Kama unaweza mtafutie shule nzuri ya boarding akakae awe anakuja nyumbani likizo tu. Na wewe uanze kuweka mipaka Kwa ndugu zake
Kama chaguo lenyewe halisomeki alipige chini faster, maisha haya hakuna kubembelezana!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…