Umepata mke mwema sana. Piga magoti hapo ulipo na umshukuru Mungu. Ukisikia wenzio mambo wanayopambana nayo huko kwenye ndoa nadhani ungewaomba mods tu waufute uzi huu.
[emoji3591][emoji3591][emoji3591] Kimsingi wanawake wote wanapenda attention sema tu wengi wamejikatia tamaa kwa sababu ya waume zao kutojali. Na wanawake wengi walio katika ndoa wanachapwa nje sana siyo kwa ajili ya pesa bali kwa kupewa attention tu, kusikilizwa, kujaliwa na kuheshimiwa.
Narudia tena: wewe umepata mke mwema na anayekujali na kukupenda. Mhakikishie tu kuwa unampenda sana na kwamba upo kwa ajili yake mpaka kifo. Vizawadi vidogo vidogo na ukipata mwanya huko kazini mpigie...hata kama ni kusema tu "Niko mkutanoni lakini nilitaka tu kukukumbusha kuwa nakupenda sana mke wangu" na kukata simu inatosha. Na siku hiyo kama una kahela mkononi mchukulie kakitafunwa kake akapendako...hata kama ni kipande cha nanasi au chips (ili azidi kuwa bonge zaidi [emoji16][emoji16][emoji16]). Ndoa zinahitaji kazi na una bahati huyo wa kwako angalau unajua anachohitaji ili kuwa na furaha. Wengine (hasa vimbaumbau) ni minuno tu na ghubu kwa kwenda mbele hata tatizo hulijui.
Akiona kuwa unamjali sana; na akawa na uhakika kuwa penzi lako kwake halijapungua; na kwamba huna wengine huko nje hata ukimwambia kuwa waifu leo naomba privacy kidogo nifanye hiki...na kibusu kidogo ukampa au ukamparaza kikofi chokonozi cha takoni - atakuelewa tu...na ukipata mwanya na wakati sahihi unaweza kuongea naye tu kwa ustaarabu kuhusu nawe kuwa na privacy yako sometimes. Atakuelewa...labda awe na matatizo mengine ya kisaikolojia.
Take care of that marriage my man. That's your duty na ukishindwa mabaharia watakusaidia...na wanajua kutoa attention na ku-care hao usiombe....Usiwape hiyo nafasi maadam unajua weakness ya mkeo!