Mke wangu anataka kujiunga na chama fulani cha siasa. Nina hofu sana

Mke wangu anataka kujiunga na chama fulani cha siasa. Nina hofu sana

Mwanamke kuwa muimba Gospel maarufu tu kunasababisha mtiti sembuse huko ambako uongo na usanii ni jadi?.

Mke wangu mimi lazima mimi niwe na final say kwake especially ninaposimamia hoja zinazolinda maslahi mapana ya familia,vinginevyo itabidi aende kwa Mume wake original.

Vipi ikitokea akawa Rais kama Samia. Hutofurahia kuwa First Gentleman?
 
Hamjambo wote!

Hili jambo limekuwa likija na kuondoka katika meza yetu hapa nyumbani. Mwanzoni nilifikiri anazungumza kama sehemu ya utani. Hiyo ni miaka saba iliyopita tena ilikuwa kipindi kile cha uchaguzi wa serikali za mitaa 2019.

Mimi nikajua matani. Lakini kadiri siku na miaka ilivyoenda nikagundua anamaanisha.

Mimi nilimuuliza kwa nini anataka kuingia kwenye siasa. Anataka nafasi ipi!
Yeye akaja na hoja zake za kikatiba na kiitifaki;
Mosi, alisema anataka kuwatumikia wananchi wa bongoland. Nikamwambia kwani huwezi kuwatumikia kwa namna nyingine mpaka uwe mwanasiasa. Unaweza kuwatumikia kwa taaluma yako.

Akaniambia, yeye licha ya kuwa na taaluma yenye hadhi na heshima lakini anataka kutanua huduma yake. Kuwatumikia wananchi katika uongozi. Kama mwanamke shupavu, superwoman na mwenye uwezo anaamini ataweza.

Vipi kuhusu nafasi, akasema yeye atatumia nafasi za viti maaulum kisha atakuwa mbunge na hatimaye kuingia mjengo.

Nikamwambia mke wangu, uamuzi na ndoto yake hiyo ninaiheshimu sana lakini naona kama haipo sahihi na itatuharibia malengo na kuhatarisha maslahi ya familia.

Kwani binafsi kama mume na kichwa cha familia sikuwahi kufikiria na sijajiandaa kuwa na mke mwanasiasa.

Akaanza kutoa hutuba zake. Mamaaa! Nikasema nimekwisha. Alivyokuwa akiongea ni kama mwanasiasa akiwa jukwaani akiwadanganya wananchi wake. Siasa! Siasa! Siasa tupu katika nyumba yangu.

Sasa nitaweka wapi sura yangu. Maana nilihisi fukuto, hasira sio hasira, mwanamke ni kama ameamua moja. Na mimi sitaki tuvunje ndoa na familia yetu. Itakuwa aibu sana.

Aibu huku mtandaoni, aibu mitaani. Yaani nitaweka wapi sura yangu.

Ooh! Mshauri wa mapenzi yamemshinda.
Ooh! Ulikuwa unajidai sana, kimekulamba.
Oooh! Kiko wapi. Tulijua tuu mtaachana.

Kwa kweli aibu nitaificha wapi. Mke anataka kuwa mwanasiasa. Anataka kula pesa za wananchi kwa kupeta tuu mdomo wake. Pyee pyee pyee!

Nikamwambia changamoto za Siasa kwa wanawake anazijua? Akaniambia anazijua na amejiandaa kukabiliana nazo.
Nikamuuliza anitajie changamoto kama Tatu zinazowakabili wanasiasa wanawake hasa chipukizi kama yeye.
Akataja. Alipofika kwenye suala la rushwa ya ngono. Nikahisi kama miguu inalegea. Suvari sio Sukari imeshuka. Presha sio presha.

Lakini anajiamini. Amesoma.
Anadai ni ndoto yake.
Anadai anauwezo.
Nia anayo, uwezo anao, nguvu anazo.

Mimi kwa kweli sijui nifanyaje. Najua wapo mtakuja kunidhihaki. Wapo mtakuja kunitukana na kunicheka. Kunizomea.

Sasa tuassume wewe ndio mkeo anataka kuwa mwanasiasa tena kwa ngazi ya kuwa mbunge. Ungefanyaje?
Ungemruhusu au ungemkatalia?

Mimi nimemaliza.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
AKIPENDA CHA RREEMASSON
NICHEKI MKUU PALE LAZJMA APELEKWE MIEZI SITA ANARUDISHA NEEMA YA FAMILIA
 
KWANZA ROBERT UPO SERIOUS AU UMEAMUA KUTENGENEZA CONTENT!? KAMA NI KWELI ITOSHE TU KUSEMA KAKA MAHUSIANO SIKU HIZI NI KAZI SANA YAANI NI MZIKI HASWA KWA MLIOOA AU MNAODATE NA WANAWAKE WAZURI, IPO HIVI HUYO MWANAMKE KIUFUPI KAONA KAMA HALI YA HAPO NYUMBANI HAITOSHI AKIKOMPEA NA THE WAY ALIVYO, NAJUA UTAJIBU MSOSI NA MAHITAJI YA WASTANI HAYASUMBUI ILA MWENZIO KAONA HAUTOSHI,KWAHIYO HAPO KAKA POLE, TULIZA AKILI HIYO NI CHANGAMOTO HATA NINGEKUA MIMI NINGEVIBRATE KWA SAMPULI YA DEMU MZURI KAMA WAKO. NA HAPO PENGINE KASHACHAT NA COLLEGE MATE WENZIE KADHAA AMBAO PENGINE KWA MUDA HUU WANA NYADHIFA KATIKA VYAMA AU WANATOKA NA VIGOGO KATIKA VYAMA NA HIVYO WANAISHI VIZURI.NA HII NDIYO INAUMIZA MAHUSIANO, MAISHA YA WENGI KUKOMPARE MAISHA YAKO NA YA MWINGINE.
 
Mkuu, ungekuwa wewe ungefanyaje?
 
Back
Top Bottom