Mke wangu anatazama Cartoon kuliko Watoto wetu

bora huyo kuliko wale wa ma tamthilia, baadae wanaanza kutaka maisha ya ki tamthilia
 
Mkuu apo umepata mke,acha aangalie katuni haina shida.Siku ukikuta anaangalia za kikubwa utasaga meno kweupe[emoji23]
 
Mimi nahisi mtu anayeangalia cartoon akiwa mtu mzima au animation au kupendelea kucheza video games kwa sana yaan kupitiliza namuona kama ana utoto mwingi ndani yake mtu30 plus cartoon,animation za nini??!!!!
 
• 😀😀, Naona na avatar yako, ipo active.
• Mkuu kwa hiyo cartoon zote hizo zipo kichwani?
 
Mkuu, nilitamani kujua hili aise, Kwa sababu nilona kama ameathirika na katuni ki design fulani hivi. [emoji848]
Sioni kama kuangalia katuni ni tatizo na uzuri umesema ni mama na mke mzuri nadhani hilo ndio la muhimu zaidi. Muache aangalie ndio furaha yake ilipo.
 
Mimi nahisi mtu anayeangalia cartoon akiwa mtu mzima au animation au kupendelea kucheza video games kwa sana yaan kupitiliza namuona kama ana utoto mwingi ndani yake mtu30 plus cartoon,animation za nini??!!!!
Sasa tuangalie nini rafiki? Yaan kama mimi ndio hunitoi kwenye makatuni
 
Aisee mi ni mpenzi wa Cartoon kinoma halafu ni beard king.Sasa watu wanasema na ndevu zako hizo unaziaibisha kupenda katuni mi napenda kinoma.Hasa hasa Animation.
Tunaitwa watoto eti. Mimi napenda sana makatuni hasa Tom&Jerry hapo ndio hunitoi
 
Kama anatimiza majukumu yake sijaona tatizo lolote, chamsingi anaenjoy Basi.....
 
Huyo ni partner wangu. mimi katuni hazinipiti na wajukuu zangu.

Sababu yangu kubwa ni kuzitazama kwanza na kuelewa kama wanafaa wazitazame au hazifai.

Maana hawa wabarikiwa siku hizi wana brain wash watoto kupitia katuni.

Katuni wanazotazama ni zile nnazo zirekodi tu, kila siku wanaweza kukuta nimewarekodia hata kumi siku ambazo hawana shule. Tenaa nazijuwa kwa serial numbers. Maana wajukuu zangu ni marufuku kuwasha king'amuzi wakiwa peke yao. Mpaka niwepo, hata wazazi wao wanalielewa hilo, hata wao ilikuwa hivyo hivyo utotoni.

Huyo ni mama mwema sana mpe hoingera kutokea kwangu.
 
nachodhani apo labda ww una wivu kwasabbu muda mwingi anatumia kwa watoto kuliko wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…