Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huyo ni partner wangu. mimi katuni hazinipiti na wajukuu zangu.
Sababu yangu kubwa ni kuzitazama kwanza na kuelewa kama wanafaa wazitazame au hazifai.
Maana hawa wabarikiwa siku hizi wana brain wash watoto kupitia katuni.
Katuni wanazotazama ni zile nnazo zirekodi tu, kila siku wanaweza kukuta nimewarekodia hata kumi siku ambazo hawana shule. Tenaa nazijuwa kwa serial numbers. Maana wajukuu zangu ni marufuku kuwasha king'amuzi wakiwa peke yao. Mpaka niwepo, hata wazazi wao wanalielewa hilo, hata wao ilikuwa hivyo hivyo utotoni.
Huyo ni mama mwema sana mpe hoingera kutokea kwangu.
Mkuu, Kumbe kuna katuni zingine ni za hovyo?Sababu yangu kubwa ni kuzitazama kwanza na kuelewa kama wanafaa wazitazame au hazifai.
Mkuu hii ya kuwasha King'amuzi mpaka uwepo wewe, huoni kama wanajisskia hasira, au kwa vile wewe ni Bibi yao ?Maana wajukuu zangu ni marufuku kuwasha king'amuzi wakiwa peke yao
Asante sana mkuu, taarifa zimefikaHuyo ni mama mwema sana mpe hoingera kutokea kwangu.
Yes upo sahihi.Mara mojamoja sio mbaya ila sio unakuwa addicted na cartoon na animations au video games kama thread ilivyojielezea
😂😂😂 Ebu hukoAngalieni Bunge na Malumbano ya hoja.
Habari wana JF, poleni na majukumu ya hapa na Pale [emoji1666].
• Kuhusu hili suala, naona kama ni uraibu wa mke wangu kutazama katuni na watoto kila dakika. "[uende - urudi ni katuni kwenda mbele na michezo ya hapa na pale.] "
• Mke wangu huwa anafurahia sana kutazama na kuimba pamoja na watoto wetu pindi wanapongalia katuni hiyo, na endapo watoto wetu kama watakua hawajaangalia hiyo katuni huwa akiwasimulia hadithi hizo baada ya watoto kuludi kutoka shule au kutoka maeneo yao ya kucheza. Kila nikiangalia hili suala la katuni, naona kabisa kuna kitu hakipo sawa kabisa.
• Kuhusu katika majukumu yake kama mke na mama wa watoto wetu, kwa kweli yupo vizuri sana analea watoto safi kabisa, ila kinachonipa wasiwasi mkubwa ni kuhusu hili suala la kuangalia katuni bila kupumzika. Yani wamegeuza nyumba kuwa nyumba ya katuni. [ uende - urudi ni katuni kwenda mbele ] na michezo ya hapa na pale.
• Kama kutakuwa na njia au namna yeyote ile naomba msaada wa kurekebisha hili tatizo la katuni.
"Nahisi kuna kitu kibaya, maana simuelewi kabisa kuhusu mke wangu, wakati mwingine hata haangalii sinema ninazotaka tuangalie pamoja, isipokuwa tu atajilazimisha kishikaji lakini moyo wake unakua unawaza katuni tu. Hata tukiwa tumekaa kama familia yeye na watoto wetu huendelea kupiga stori za katuni.
• "Mke wangu, mwenye umri wa miaka 33 sasa, anafurahia sana kutazama katuni zaidi kuliko hata watoto wetu. Mvulana wetu wa kwanza ana umri wa miaka 11 hadi wa mwisho ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 4.
• Naona kama mke wangu amepatwa na uraibu wa katuni hivi , wao ni kuimba nyimbo za katuni , kupiga ngoma zao na kujadili mambo ya katuni kila wakati.
• Nimejaribu kumweleza kuwa sipendi kabisa tabia ya kuangalia katuni kila sekunde lakini wapi!!! , silalamiki kwa sababu wanafurahi lakini sielewi uraibu wa mke wangu ni nini hasa?. Hata wakati watoto wakiwa hawapo karibu, yeye ataendelea kutizama filamu za katuni peke yake. Watoto Watakapofika nyumbani , atawasimulia yote aliyoyatazama na hata kuwaonyesha kwa vitendo matukio ya kuchekesha/yenye hisia.
• Tafadhali kumbuka kuwa, ameajiriwa kikamilifu na bado anafanya kazi zake kama mke na mama. Sina tatizo lolote kwa upande huo, je amezoea filamu za katuni au kuna kitu kimejificha? Au nimuache akikua ataacha mwenyewe, Maana sielewi kabisa."
• Je, kitu gani ninaweza kufanya ili kumsaidia mke wangu ? Inanisumbua sana akili yangu kwa namna fulani.
[emoji41]Hii ni story ya kijana Mwenye familia ya watoto wa tatu [emoji3578][emoji3578][emoji3578][emoji3578].
View attachment 2856301View attachment 2856302View attachment 2856303
🤣🤣Mbona unanisema mimi, napenda cartoon
Zinafurahisha...
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Sawasawa 👍Ndio maana akaitwa mwanamke. As long as hakuna madhara. Kuna mambo inabidi U compromise ili maisha yasonge🤔