Mke wangu hanisalimii, anasema salamu ni wajibu wa mwanaume kwa mke au familia yake

Huaga natumia siku 5 za wiki kwenda mahala pakazi yangu na siku 2 za mwisho wa wiki kushinda nyumbani na familia yangu, japo mara nyingine ikalazimu hata hizo siku za wiki naweza kuwa nyumbani.
Hili limezaa tabia mpya unazoona.
 
Hiyo avatar mkuu automatic najikuta nasoma in Yombo's voiceπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ sema namkubali sana jamaa, huwa nakaa najiuliza anatoa wapi maneno ya hovyo kiasi kile halafu kwenye kila clip harudii maneno (labda zile za kuchamba wazinzi)
 
Weka hatua zote tujifunze hapa.
 
Huaga wajibu wakusalimia ni wa mwanaume tu? Hasa pale mnapokuwa mbali na familia zenu?
Mzee Hii haina formula inategemea Tu na Mapenzi yenu. Mimi kuna Jamaa alishangaa nilivyomwambia kuwa kwa Siku moja napigiwa Simu mara TATU Hadi nne kunijulia hali na kuulizwa " utakula nini, au utakula tunda Tu?". Jamaa alishangaa Sana Sana.

Ninachosema ni kwamba, kila familia ina utamaduni wake, huenda huo ukawa ndio utaratibu wenu. Mimi napiga japo huwa simzidi yeye. Hata Sasa hivi saa moja asubuhi amepiga kwakua nimesafiri.....
 
Mimi nilikuwa na kiherehere cha kupiga asubuhi, mara naambiwa namba inatumika.....kuanzia hapo nilifuta namba, sipigi hadi anipigie.....nikiwa na shida natuma msg.....Sasa hivi tunaishi pamoja.
Mtoa mada aseme ukweli kuna kitu anaficha......
 
Wewe mwenye mda wa kujadili hayo na mke wako mwenye hayo majibu kwa kweli ni Mwili mmoja, vumilianeni, maana Tabia za hovyo zinafanana
 
Kiongozi Wala haiwi utamaduni kuwa Mmoja asalimie na mwingine awe wakusalimiwa tu.

Kuonyesha kujali lazima wote muwe na utaratibu wakasalimiana.

Hongera saana, kwahiyo tabia ya huyo uliyenae.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…