Kwani muonekano wako ukoje?Je kabla ya Ndoa ulikua unaonekanaje?Je Mavazi yako yakoje?Je Kipato chako kikoje kwa sasa? Je Umri wako na yeye mmepishana na kama ndio ni kwa kiasi gani?
Labda umeoa sister do na sasa anakuona unamuaibisha .Jaribu kujiweka kile leo, Punguza Kitambi,kama una upara kichwani, nyoa nywele zote usiache upara uukatokea , kama umenenepa jaribu kwenda Gym , tengeneza mwili na kama suala ni kipato , jaribu kwa kila njia kurudisha kipato chako.
Kama yote hayo ni yuko vizuri, basi labda tabia yako unavyo mtreat mbele za watu ni mbaya , labda unamuaibisha ,kumkaripia au kumshusha ukiwa kwenye public au pia ina wezekana hujatulia una michepuko na mkeo kaisha choka, hiyo tabia yako ameshambiwa sana na anaona kichefu chefu akiwa na wewe sababu mashoga zake wana mcheka kwamba kaolewa na Mchepukaji na yeye hawezi toka kweye ndoa kwa sababu kadhaa.jaribu kubadilika labda utaona mabadiliko .