Mimi ni mwanaume wa kawaida, nimejaaliwa kipato cha wastani tu kinachotokana na juhudi za kujihusisha na hiki na kile kwa kupitia kujiajiri.
Mke wangu pia ni mchakarikaji na anaitumikia biashara ya vyombo vya ndani na mapambo ya ndani ambayo kwa pamoja tuliifungua na inafanya vzr sana.
Tumejaaliwa kuwa na gari moja Suzuki modeli mpya ambayo kiukweli aliinunua yeye mwaka Jana January. Kwasasa mimi ni fundi wa mashine za aina mbalimbali ikiwemo majenereta, magreda, kreni n.k. Na kwa kuwa mishe zangu za kiufundi hazihusishi sana matumizi ya gari ya kutembelea kwahyo huwa naitumia mara chache sana.
Baada ya kumfundisha mkewangu kuendesha akawa nayo kuanzia hapo. Mie Nina pikipiki ambayo hunipeleka huku na kule na kunifanikishia mishughukiko yangu yote bila tashwishi . Ninapohitaji gari kwa ajili ya matumizi ya hapa na pale au ninapoonyesha dalili ya kwamba nitatumia gari siku hiyo, papo hapo mke wangu huanza kujiskia karaha na ataanza kuongea maneno ambayo yanatoa ishara kwamba hataki ntumie gari.
Ukweli sipendezwi na hali hiyo maana inaudhi sana. Kwakuwa nimeshamjulia huwa nampuuza afu nachukua gari naenda kwenye kusudi nililolenga lkn furaha yake hutoweka kwa siku hiyo na hukereka kiukweli. Ingawa mie ndo niliyemfundisha kuendesha lkn pia haniamini napoendesha gari na hapendi nimuendeshe na kila wakati anasikika akinikosoa ninapoendesha, yani huwa dereva namba moja wakati aliyeshika usukani ni mimi.
Na kwa vile ameshajua pia nampuuza katika hilo, mara nyingi mke wangu huamua kukaa siti ya nyuma kwa vile haamini udereva wangu na huona kama nitamsababishia ajali akikaa mbele.
Kwa ufupi hapendezwi ninvyoendesha gari na hili jambo linanikera sana.
NAOMBENI USHAURI WENU WA KUNIJENGA KTK HILI.
Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo Mke wako:
1) Ni mchoyo sana Chake chake , chako chetu.
2) Ni Malaya inawezekana hataki mabwana zake wamwone na wewe ndo maana anakaa nyuma, Mke wako lazima akae mbele kwa furaha kama hana makondakonda kama ya mke wako
3) Huyo mama hakupendi ndo maana hataki watu wengine watabuwe kwamba yeye ni mke wako.
4) Inawezekana wewe siyo handsome wa kula naye bata ndo maana anaona choo kuendeshwa na wewe mzee wa spana za mashine muda wote unanuka greese na oil chafu.
5) Huyo mke wako akishapata pesa za kutosha ataomba taraka kwa vile atakuwa na pesa za kumusukuma mwaka mmoja.