Mke wangu hataki niendeshe gari alilonunua. Nakereka sana

Mke wangu hataki niendeshe gari alilonunua. Nakereka sana

Pole Sana Kaka. Pole Sana kwa mkeo kuwa KERO. Wanawake wenzangu tubadilike jamani. Mume wangu siku anataka kutumia gari.... Namuomba mapema kabisa anipeleke usafiri wa bajaji unapopatikana..... naendelea na ratiba zangu kama kawaida. Nikimaliza narudi nyumbani.... Raha mustarehe... Mapenzi Mubashara[emoji23][emoji28]. Mapenzi yana Raha Sana Wanawake wenzangu ... Haya Mambo madogo madogo haya tujifunze kuya-ignore. Tujifunze kujishusha kwenye baadhi ya mambo ambayo tunaweza kufanya na hayasumbui sana.... Kwani utapungukiwa nini? .... Pia Tunapunguza mikwaruzano inayoweza kuepukika. Gari zipo tuu. Cha muhimu Penzi na Raha ya MUME.
Nipe namba nikutumie hata hongera kwa hii comment yako nzuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi ni mwanaume wa kawaida, nimejaaliwa kipato cha wastani tu kinachotokana na juhudi za kujihusisha na hiki na kile kwa kupitia kujiajiri.

Mke wangu pia ni mchakarikaji na anaitumikia biashara ya vyombo vya ndani na mapambo ya ndani ambayo kwa pamoja tuliifungua na inafanya vzr sana.

Tumejaaliwa kuwa na gari moja Suzuki modeli mpya ambayo kiukweli aliinunua yeye mwaka Jana January. Kwasasa mimi ni fundi wa mashine za aina mbalimbali ikiwemo majenereta, magreda, kreni n.k. Na kwa kuwa mishe zangu za kiufundi hazihusishi sana matumizi ya gari ya kutembelea kwahyo huwa naitumia mara chache sana.

Baada ya kumfundisha mkewangu kuendesha akawa nayo kuanzia hapo. Mie Nina pikipiki ambayo hunipeleka huku na kule na kunifanikishia mishughukiko yangu yote bila tashwishi . Ninapohitaji gari kwa ajili ya matumizi ya hapa na pale au ninapoonyesha dalili ya kwamba nitatumia gari siku hiyo, papo hapo mke wangu huanza kujiskia karaha na ataanza kuongea maneno ambayo yanatoa ishara kwamba hataki ntumie gari.

Ukweli sipendezwi na hali hiyo maana inaudhi sana. Kwakuwa nimeshamjulia huwa nampuuza afu nachukua gari naenda kwenye kusudi nililolenga lkn furaha yake hutoweka kwa siku hiyo na hukereka kiukweli. Ingawa mie ndo niliyemfundisha kuendesha lkn pia haniamini napoendesha gari na hapendi nimuendeshe na kila wakati anasikika akinikosoa ninapoendesha, yani huwa dereva namba moja wakati aliyeshika usukani ni mimi.

Na kwa vile ameshajua pia nampuuza katika hilo, mara nyingi mke wangu huamua kukaa siti ya nyuma kwa vile haamini udereva wangu na huona kama nitamsababishia ajali akikaa mbele.

Kwa ufupi hapendezwi ninvyoendesha gari na hili jambo linanikera sana.

NAOMBENI USHAURI WENU WA KUNIJENGA KTK HILI.

Sent using Jamii Forums mobile app
itakuwa kahongwa
 
Wewe achana na gari yake tumia pikipiki yako, mbona wanawake wengi tunapanda mpaka bodaboda japo nyumbani kuna Paso mkuu? Fanya yako wewe tafuta pesa kimya kimya nunua nalo basi siku ukinunua lako na lake ndiyo lina haribika[emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sisi ni watu wa ajabu sana. Hapo gari lingekua la mwanamke angelichukua bila hata kuomba. Na angepewa bila gubu. Shida sisi ni wabinafsi sana.

Sent From Galaxy S9
Kuna uzi fulani mdada mmoja ameuanzisha anadai Wanawake sio wabinafsi ila wewe hapa umethibitisha kuwa,Wanawake ni wabinafsi.
 
Pole kijana ila maisha ndo yalivyo.
Wewe ulimfundisha kuendesha gari hukuchangia kununua gari kwahiyo uwe mpole mpaka utakaponunua gari lako apo mtakuwa salama.
Kuhusu kumpuuza huwezi kujua anakwazika kiasi gani na hajari haina kinga ipo siku utachukua gari akiwa hataki utalibamiza na uo ndio utakuwa mwisho wa ndoa yenu.
Je wakati anajiandaa kununua ulishirikishwa hatua zote?
Je una uhakika pesa alonunulia gari zilitokana na biashara yenu?
Ukinijibu nitaendelea kukushauri.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ushauri wa kipumbavu sana. Kwani hawa si mke na mume? Si mwili mmoja? Acheni kuwafanya watu kama vile ni majirani wakati ni mwili mmoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole Sana Kaka. Pole Sana kwa mkeo kuwa KERO. Wanawake wenzangu tubadilike jamani. Mume wangu siku anataka kutumia gari.... Namuomba mapema kabisa anipeleke usafiri wa bajaji unapopatikana..... naendelea na ratiba zangu kama kawaida. Nikimaliza narudi nyumbani.... Raha mustarehe... Mapenzi Mubashara[emoji23][emoji28]. Mapenzi yana Raha Sana Wanawake wenzangu ... Haya Mambo madogo madogo haya tujifunze kuya-ignore. Tujifunze kujishusha kwenye baadhi ya mambo ambayo tunaweza kufanya na hayasumbui sana.... Kwani utapungukiwa nini? .... Pia Tunapunguza mikwaruzano inayoweza kuepukika. Gari zipo tuu. Cha muhimu Penzi na Raha ya MUME.
Vizuri sana wanawake mnaojitambua na kujua kwamba haya mambo ni ya kupita.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu wangu, kila hatua alinihusisha na ninataka nikuhakikishie kwamba pesa za manunuzi zilitokana na biashara na hiyo biashara ni yetu. Naiita ni yetu kwa mantiki mimi ndiye mtoa mtaji kwa 100% na nikamkabidhi kama ajira yake lkn kitega uchumi cha familia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo ni limbukeni. We tumia gari tu akileta tena ujinga ng'oa kifaa muhimu ukakifiche mahali na kumuwekea kile feki halafu gari ikikaa sana unaenda kukitafuta na kumwambia umeamua kumnununlia hicho kifaa ili gari isije oza. Kama atanunua mwenyewe kile unakiuza halafu gari endelea kuliendesha. Mkeo mshamba sana. Lakini pole kwa yote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anajenga, side effect ipo lkn sio kubwa
Hapana for me, I don't think it's an appropriate approach kwasasa. Cha msingi akae nae chini amwambie kuhusu hali anayokuwa nayo mke wake pale anapohiitaji gari lililonunuliwa kwa mtaji wake. Hiyo statement inaweza ikazaa mengine ambayo yanaweza yakamfanya mwanaume ang'amue kwanini mwanamke anakuwa hivyo
 
wanawake wote wangkuwa sawa sawa na haya maneno yako bas tisingezijutia ndoa zetu daima...
Pole Sana Kaka. Pole Sana kwa mkeo kuwa KERO. Wanawake wenzangu tubadilike jamani. Mume wangu siku anataka kutumia gari.... Namuomba mapema kabisa anipeleke usafiri wa bajaji unapopatikana..... naendelea na ratiba zangu kama kawaida. Nikimaliza narudi nyumbani.... Raha mustarehe... Mapenzi Mubashara[emoji23][emoji28]. Mapenzi yana Raha Sana Wanawake wenzangu ... Haya Mambo madogo madogo haya tujifunze kuya-ignore. Tujifunze kujishusha kwenye baadhi ya mambo ambayo tunaweza kufanya na hayasumbui sana.... Kwani utapungukiwa nini? .... Pia Tunapunguza mikwaruzano inayoweza kuepukika. Gari zipo tuu. Cha muhimu Penzi na Raha ya MUME.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ndoa zina shughuli pana kamaa yangu mmona yeye haruhusiwe endesha gari na mke wake, mke yupo radhi atafute mtu mwingine aendeshe na si mume wake...
 
Back
Top Bottom