Mke wangu hataki niendeshe gari alilonunua. Nakereka sana

Mke wangu hataki niendeshe gari alilonunua. Nakereka sana

Mwanamke mara nyingine anaweza kuhamishia hasira sehemu zingine lakini alikoipata ni kwingineee..




Unamkojoza vizuri?? Au unakojoza hiyo mitambo kazini tu..


Tuanzie hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimejikuta nawachukia sana watu wanaotoa siri za wapenzi wao hadharani, hivi unadhani nani anajali? inatusaidia nini>? Jifunze kumheshimu mke au mume wako, social media kamwe haiwezi kukusaidia matatizo yako zaidi utaishia kupata majanga zaidi
ndo maana ya fake id's kaka
 
Pole Sana Kaka. Pole Sana kwa mkeo kuwa KERO. Wanawake wenzangu tubadilike jamani. Mume wangu siku anataka kutumia gari.... Namuomba mapema kabisa anipeleke usafiri wa bajaji unapopatikana..... naendelea na ratiba zangu kama kawaida. Nikimaliza narudi nyumbani.... Raha mustarehe... Mapenzi Mubashara[emoji23][emoji28]. Mapenzi yana Raha Sana Wanawake wenzangu ... Haya Mambo madogo madogo haya tujifunze kuya-ignore. Tujifunze kujishusha kwenye baadhi ya mambo ambayo tunaweza kufanya na hayasumbui sana.... Kwani utapungukiwa nini? .... Pia Tunapunguza mikwaruzano inayoweza kuepukika. Gari zipo tuu. Cha muhimu Penzi na Raha ya MUME.
[emoji849][emoji849][emoji849][emoji849][emoji134][emoji134]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
(1)mke wako amekuchulia poa sna ...wewe ni baba lazima uwe chuma ktk familia kuwa hata mkali sna anapoonesha vitabia vya kipumbavu.
( 2)mkalishe chini mwelekeze jinsi upendezewi na tabia zake za kujinunisha.

(3)fikilia kugawana mali uachane kama hatokuwa tayari kubadika kitabia....lasiivyo usipokuwa strong utakuja kuwa kichaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Gari kanunuliwa na Mume mwenzako bro so anapigwa mkwara mwenyewe akikuona nalo jipange Nunua lako
 
Mimi ni mwanaume wa kawaida, nimejaaliwa kipato cha wastani tu kinachotokana na juhudi za kujihusisha na hiki na kile kwa kupitia kujiajiri.

Mke wangu pia ni mchakarikaji na anaitumikia biashara ya vyombo vya ndani na mapambo ya ndani ambayo kwa pamoja tuliifungua na inafanya vzr sana.

Tumejaaliwa kuwa na gari moja Suzuki modeli mpya ambayo kiukweli aliinunua yeye mwaka Jana January. Kwasasa mimi ni fundi wa mashine za aina mbalimbali ikiwemo majenereta, magreda, kreni n.k. Na kwa kuwa mishe zangu za kiufundi hazihusishi sana matumizi ya gari ya kutembelea kwahyo huwa naitumia mara chache sana.

Baada ya kumfundisha mkewangu kuendesha akawa nayo kuanzia hapo. Mie Nina pikipiki ambayo hunipeleka huku na kule na kunifanikishia mishughukiko yangu yote bila tashwishi . Ninapohitaji gari kwa ajili ya matumizi ya hapa na pale au ninapoonyesha dalili ya kwamba nitatumia gari siku hiyo, papo hapo mke wangu huanza kujiskia karaha na ataanza kuongea maneno ambayo yanatoa ishara kwamba hataki ntumie gari.

Ukweli sipendezwi na hali hiyo maana inaudhi sana. Kwakuwa nimeshamjulia huwa nampuuza afu nachukua gari naenda kwenye kusudi nililolenga lkn furaha yake hutoweka kwa siku hiyo na hukereka kiukweli. Ingawa mie ndo niliyemfundisha kuendesha lkn pia haniamini napoendesha gari na hapendi nimuendeshe na kila wakati anasikika akinikosoa ninapoendesha, yani huwa dereva namba moja wakati aliyeshika usukani ni mimi.

Na kwa vile ameshajua pia nampuuza katika hilo, mara nyingi mke wangu huamua kukaa siti ya nyuma kwa vile haamini udereva wangu na huona kama nitamsababishia ajali akikaa mbele.

Kwa ufupi hapendezwi ninvyoendesha gari na hili jambo linanikera sana.

NAOMBENI USHAURI WENU WA KUNIJENGA KTK HILI.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wana u-selfish kiwango cha fly over, tumia pik yako kwa mishe zako na ikiwa kuna ulazima wa gari,kodisha. Jiweke mbali na vitu vyake muache ahangahike navyo weee hadi achoke mwisho atahisi umesusa ndipo atakuuliza, mjibu hayo matakataka yooote tunayohangahika nayo ni ya kupita tu siku wote tunakufa tunayaacha kwa hiyo niliona nisikupe tabu sana endelea na vitu vyako vikusaidie. Fanya yako tu watu wa namna hiyo huwa wanaishia kufeli vibaya ni suala la muda tu.
 
Nimejikuta nawachukia sana watu wanaotoa siri za wapenzi wao hadharani, hivi unadhani nani anajali? inatusaidia nini>? Jifunze kumheshimu mke au mume wako, social media kamwe haiwezi kukusaidia matatizo yako zaidi utaishia kupata majanga zaidi
Akijiua utakuwa wa kwanza kuwa kwa nini hakuomba ushauri,akiomba ushauri unachukia,binadamu bwana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ha ha umenikumbusha kipindi hicho kuna demu akaniganda tubadilishane simu [emoji3][emoji3]..
Nimpe Note 4 yeye anipe kitecno chake, niliwaza sana akili ya hawa watu!
Na akinunua zuri zaidi ya alilo nalo mke wake atataka wabadilishane.
 
Back
Top Bottom