Mke wangu hataki niendeshe gari alilonunua. Nakereka sana

Mimi ni mwanaume wa kawaida, nimejaaliwa kipato cha wastani tu kinachotokana na juhudi za kujihusisha na hiki na kile kwa kupitia kujiajiri.

Mke wangu pia ni mchakarikaji na anaitumikia biashara ya vyombo vya ndani na mapambo ya ndani ambayo kwa pamoja tuliifungua na inafanya vizuri sana.

Tumejaaliwa kuwa na gari moja Suzuki modeli mpya ambayo kiukweli aliinunua yeye mwaka Jana January. Kwasasa mimi ni fundi wa mashine za aina mbalimbali ikiwemo majenereta, magreda, kreni n.k. Na kwa kuwa mishe zangu za kiufundi hazihusishi sana matumizi ya gari ya kutembelea kwahyo huwa naitumia mara chache sana.

Baada ya kumfundisha mke wangu kuendesha akawa nayo kuanzia hapo. Mie Nina pikipiki ambayo hunipeleka huku na kule na kunifanikishia mishughukiko yangu yote bila tashwishi. Ninapohitaji gari kwa ajili ya matumizi ya hapa na pale au ninapoonyesha dalili ya kwamba nitatumia gari siku hiyo, papo hapo mke wangu huanza kujiskia karaha na ataanza kuongea maneno ambayo yanatoa ishara kwamba hataki nitumie gari.

Ukweli sipendezwi na hali hiyo maana inaudhi sana. Kwakuwa nimeshamjulia huwa nampuuza afu nachukua gari naenda kwenye kusudi nililolenga lkn furaha yake hutoweka kwa siku hiyo na hukereka kiukweli. Ingawa mie ndo niliyemfundisha kuendesha lkn pia haniamini napoendesha gari na hapendi nimuendeshe na kila wakati anasikika akinikosoa ninapoendesha, yani huwa dereva namba moja wakati aliyeshika usukani ni mimi.

Na kwa vile ameshajua pia nampuuza katika hilo, mara nyingi mke wangu huamua kukaa siti ya nyuma kwa vile haamini udereva wangu na huona kama nitamsababishia ajali akikaa mbele.

Kwa ufupi hapendezwi ninvyoendesha gari na hili jambo linanikera sana.

NAOMBENI USHAURI WENU WA KUNIJENGA KATIKA HILI.

Sasa ukisikia msemo kuwa Mwanamke akiwezeshwa Anaweza ndio huu unauishi wewe. Huyu mkeo akifanikiwa sana atatafuta wengine wamuwezeshe.
 
Aisee umenifurahisha sana kumbe tuko wengi kwenye hii kadhia [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Mimi mke wangu nimemfundisha gari mwenyewe alikua hajui a wala be mpaka amekua dereva na leseni nikamtafutia. Ni zaidi ya miaka mi 5 sasa tangu aanze kuendesha gari. Katika kipindi chote hicho, yeye ameshagonga gari, kukwangua, kupasua taa, vioo, kugonga miti, mageti, nk mara zisizohesabika. Mimi sijawahi kugonga hata inzi!

Cha ajabu sasa nikiwa naendesha mimi utasikia "eh, punguza mwendo bana unakimbia sana" (hapo niko speed 30), "ongeza mwendo, we huoni hilo semetrela nyuma..? Au paki kwanza lipite!", "hii kona umekatia mbali sana", "unaona hiyo gari mbele, unaona..?", "washa indiketa tunaingia pale...", "mpigie honi huyo bodaboda utamvaa", "washa full bana mimi sioni mbele..", "mbona umeovatekia karibu hivyo?"... yaani mi hua saa nyingine naishia kucheka tuu..[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Pole Sana Kaka. Pole Sana kwa mkeo kuwa KERO. Wanawake wenzangu tubadilike jamani. Mume wangu siku anataka kutumia gari.... Namuomba mapema kabisa anipeleke usafiri wa bajaji unapopatikana..... naendelea na ratiba zangu kama kawaida. Nikimaliza narudi nyumbani.... Raha mustarehe... Mapenzi Mubashara😂😅.

Mapenzi yana Raha Sana Wanawake wenzangu ... Haya Mambo madogo madogo haya tujifunze kuya-ignore. Tujifunze kujishusha kwenye baadhi ya mambo ambayo tunaweza kufanya na hayasumbui sana.... Kwani utapungukiwa nini? .... Pia Tunapunguza mikwaruzano inayoweza kuepukika. Gari zipo tuu. Cha muhimu Penzi na Raha ya MUME.
Natangaza harambee upewe mitano tena...

BTW sanamu yako unataka tuiweke wapi?
 
Nimejikuta nawachukia sana watu wanaotoa siri za wapenzi wao hadharani, hivi unadhani nani anajali? inatusaidia nini>? Jifunze kumheshimu mke au mume wako, social media kamwe haiwezi kukusaidia matatizo yako zaidi utaishia kupata majanga zaidi
Kiukweli kabisa, kosa sio la mwanamke. Kosa ni la huyu mwanaume mzembe...
 
Mimi ni mwanaume wa kawaida, nimejaaliwa kipato cha wastani tu kinachotokana na juhudi za kujihusisha na hiki na kile kwa kupitia kujiajiri.

Mke wangu pia ni mchakarikaji na anaitumikia biashara ya vyombo vya ndani na mapambo ya ndani ambayo kwa pamoja tuliifungua na inafanya vizuri sana.

Tumejaaliwa kuwa na gari moja Suzuki modeli mpya ambayo kiukweli aliinunua yeye mwaka Jana January. Kwasasa mimi ni fundi wa mashine za aina mbalimbali ikiwemo majenereta, magreda, kreni n.k. Na kwa kuwa mishe zangu za kiufundi hazihusishi sana matumizi ya gari ya kutembelea kwahyo huwa naitumia mara chache sana.

Baada ya kumfundisha mke wangu kuendesha akawa nayo kuanzia hapo. Mie Nina pikipiki ambayo hunipeleka huku na kule na kunifanikishia mishughukiko yangu yote bila tashwishi. Ninapohitaji gari kwa ajili ya matumizi ya hapa na pale au ninapoonyesha dalili ya kwamba nitatumia gari siku hiyo, papo hapo mke wangu huanza kujiskia karaha na ataanza kuongea maneno ambayo yanatoa ishara kwamba hataki nitumie gari.

Ukweli sipendezwi na hali hiyo maana inaudhi sana. Kwakuwa nimeshamjulia huwa nampuuza afu nachukua gari naenda kwenye kusudi nililolenga lkn furaha yake hutoweka kwa siku hiyo na hukereka kiukweli. Ingawa mie ndo niliyemfundisha kuendesha lkn pia haniamini napoendesha gari na hapendi nimuendeshe na kila wakati anasikika akinikosoa ninapoendesha, yani huwa dereva namba moja wakati aliyeshika usukani ni mimi.

Na kwa vile ameshajua pia nampuuza katika hilo, mara nyingi mke wangu huamua kukaa siti ya nyuma kwa vile haamini udereva wangu na huona kama nitamsababishia ajali akikaa mbele.

Kwa ufupi hapendezwi ninvyoendesha gari na hili jambo linanikera sana.

NAOMBENI USHAURI WENU WA KUNIJENGA KATIKA HILI.
Pole sana mkuu,ukishaoa ndio kuna hivyo vituko,ombea amani ya nyumba yako...
 
Aisee umenifurahisha sana kumbe tuko wengi kwenye hii kadhia 😂😂😂😂😂😂

Mimi mke wangu nimemfundisha gari mwenyewe alikua hajui a wala be mpaka amekua dereva na leseni nikamtafutia. Ni zaidi ya miaka mi 5 sasa tangu aanze kuendesha gari. Katika kipindi chote hicho, yeye ameshagonga gari, kukwangua, kupasua taa, vioo, kugonga miti, mageti, nk mara zisizohesabika. Mimi sijawahi kugonga hata inzi!

Cha ajabu sasa nikiwa naendesha mimi utasikia "eh, punguza mwendo bana unakimbia sana" (hapo niko speed 30), "ongeza mwendo, we huoni hilo semetrela nyuma..? Au paki kwanza lipite!", "hii kona umekatia mbali sana", "unaona hiyo gari mbele, unaona..?", "washa indiketa tunaingia pale...", "mpigie honi huyo bodaboda utamvaa", "washa full bana mimi sioni mbele..", "mbona umeovatekia karibu hivyo?"... yaani mi hua saa nyingine naishia kucheka tuu..🤣🤣🤣🤣
Hivo hivo tu kaka, hi kama wanaume tuichukue tu kama changamoto ya kusihi na hawa viumbe. Kwa ufupi uliyasema yote na kwangu yapo hivo hivo hadi watoto huaga wanamindi mama yao
 
Aisee umenifurahisha sana kumbe tuko wengi kwenye hii kadhia [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Mimi mke wangu nimemfundisha gari mwenyewe alikua hajui a wala be mpaka amekua dereva na leseni nikamtafutia. Ni zaidi ya miaka mi 5 sasa tangu aanze kuendesha gari. Katika kipindi chote hicho, yeye ameshagonga gari, kukwangua, kupasua taa, vioo, kugonga miti, mageti, nk mara zisizohesabika. Mimi sijawahi kugonga hata inzi!

Cha ajabu sasa nikiwa naendesha mimi utasikia "eh, punguza mwendo bana unakimbia sana" (hapo niko speed 30), "ongeza mwendo, we huoni hilo semetrela nyuma..? Au paki kwanza lipite!", "hii kona umekatia mbali sana", "unaona hiyo gari mbele, unaona..?", "washa indiketa tunaingia pale...", "mpigie honi huyo bodaboda utamvaa", "washa full bana mimi sioni mbele..", "mbona umeovatekia karibu hivyo?"... yaani mi hua saa nyingine naishia kucheka tuu..[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Ha ha ha ha ha

Daah nimecheka sana

Hata mi Huwa na hizi tabia ila sio nzuri hata kidogo[emoji2960][emoji2960][emoji2960][emoji848][emoji851][emoji851]
 
Umeanza lini hiyo tabia. Enzi zetu mbona hukuwa na tabia hiyo?
 
Kuna baadhi ya mambo ni hulka za wanawake karibu wote some ni tabia binafsi za huyo mkeo; mfano hiyo ya ukosoaji wa namna yako ya kuendesha gari is almost wanawake wengi wapo hivyo, mke wang as well hadi watoto wake hua wanamkosoa na yeye anabakia kucheka tu. Kuna binti mmoja nilikua napiga nae show mara kadhaa, nimeacha baada ya yeye kuolewa, one day nilichukua gari lake nikaenda niliko kwenda, wakati namrudishia akaniomba nimsindikize sehemu, yeye nae kama wife tu, full kukosoa kosoa na wanawake wengine wengi tu. Kikubwa mkuu, tafuta pesa ununue gari lako, wanawake hawakuumbwa kulea mwanaume, wameumbwa kulelewa na mwanaume. Nataka kusema hivi, siku ukijaaliwa ukanunua gari lako, hiyo ya kukosolewa namna yako ya driving itaendelea, mengine anaweza kuyaacha but hiyo ya kukosolewa itaendelea tu hadi mnazeeka
Hehehehehe[emoji23][emoji16][emoji41][emoji41]
 
Ha ha ha ha ha

Daah nimecheka sana

Hata mi Huwa na hizi tabia ila sio nzuri hata kidogo[emoji2960][emoji2960][emoji2960][emoji848][emoji851][emoji851]
I wish i kudu be Hai Jipiii (IGP) kumbe mnatumaindisha tukiendesha magari yenu jamani women mtatuua! Maelekezo kibao kama traffic wa vehicle😅😅😅
 
Tegemea kuombwa talaka muda wowote hapo huna mke kashakua matawi ya juu. Wanawake wengi akishajiona anaongoza kipato kikubwa anatamani awe huru Kama hauamini chunguza marafiki alionao sasa angalia Wana tabia gani
 
Back
Top Bottom