Mangungo II
JF-Expert Member
- Jul 6, 2012
- 18,133
- 26,766
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mimi ni mwanaume wa kawaida, nimejaaliwa kipato cha wastani tu kinachotokana na juhudi za kujihusisha na hiki na kile kwa kupitia kujiajiri.
Mke wangu pia ni mchakarikaji na anaitumikia biashara ya vyombo vya ndani na mapambo ya ndani ambayo kwa pamoja tuliifungua na inafanya vzr sana.
Tumejaaliwa kuwa na gari moja Suzuki modeli mpya ambayo kiukweli aliinunua yeye mwaka Jana January. Kwasasa mimi ni fundi wa mashine za aina mbalimbali ikiwemo majenereta, magreda, kreni n.k. Na kwa kuwa mishe zangu za kiufundi hazihusishi sana matumizi ya gari ya kutembelea kwahyo huwa naitumia mara chache sana.
Baada ya kumfundisha mkewangu kuendesha akawa nayo kuanzia hapo. Mie Nina pikipiki ambayo hunipeleka huku na kule na kunifanikishia mishughukiko yangu yote bila tashwishi . Ninapohitaji gari kwa ajili ya matumizi ya hapa na pale au ninapoonyesha dalili ya kwamba nitatumia gari siku hiyo, papo hapo mke wangu huanza kujiskia karaha na ataanza kuongea maneno ambayo yanatoa ishara kwamba hataki ntumie gari.
Ukweli sipendezwi na hali hiyo maana inaudhi sana. Kwakuwa nimeshamjulia huwa nampuuza afu nachukua gari naenda kwenye kusudi nililolenga lkn furaha yake hutoweka kwa siku hiyo na hukereka kiukweli. Ingawa mie ndo niliyemfundisha kuendesha lkn pia haniamini napoendesha gari na hapendi nimuendeshe na kila wakati anasikika akinikosoa ninapoendesha, yani huwa dereva namba moja wakati aliyeshika usukani ni mimi.
Na kwa vile ameshajua pia nampuuza katika hilo, mara nyingi mke wangu huamua kukaa siti ya nyuma kwa vile haamini udereva wangu na huona kama nitamsababishia ajali akikaa mbele.
Kwa ufupi hapendezwi ninvyoendesha gari na hili jambo linanikera sana.
NAOMBENI USHAURI WENU WA KUNIJENGA KTK HILI.
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu unakosea Sana, yani umpe mke biashara aendeshe halafu usifuatilie mapato?Mkuu wangu, kila hatua alinihusisha na ninataka nikuhakikishie kwamba pesa za manunuzi zilitokana na biashara na hiyo biashara ni yetu. Naiita ni yetu kwa mantiki mimi ndiye mtoa mtaji kwa 100% na nikamkabidhi kama ajira yake lkn kitega uchumi cha familia.
Sent using Jamii Forums mobile app
Pole mkuu..hilo gari sio lake..yeye ni kivuli tu cha alionalo,atakua kuna mtu aliweka fungu lake kubwa ili amfanikishie anunue hilo gari ndo maana anaona jau ukiwa unataka kuliendesha usijepishana na mwenye nalo..yeye kukaa nyuma anahifia mkionwa pamoja..maana ukionwa wewe pekeako anaweza sema wewe ni mfanyakazi wao alikutuma..
Kama si hivyo nnavyofikiria tofauti na hapo huyo mwanamke ana roho ya uchoyo sana..
Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaha unataka mkewe avimbe na kupasuka kwa kihoro cha wivu?Achana na Gari yake, ww fanya safar zako bila gari yake ila hakikisha ukirudi sifia Demu aliekupa lift kuwa ana roho ya huruma na ubinadam sana.
Wakati mwingine mwambie kuna rafiki ako wa kike atakuazima gar yake ili yeye asikose kitoka na gari yake
Kwani huyu jamaa unamfahamu yeye na mkewe?Au unaongelea wale unaowafahamu?Nimejikuta nawachukia sana watu wanaotoa siri za wapenzi wao hadharani, hivi unadhani nani anajali? inatusaidia nini>? Jifunze kumheshimu mke au mume wako, social media kamwe haiwezi kukusaidia matatizo yako zaidi utaishia kupata majanga zaidi
Mimi nilichoonaMkuu wangu, kila hatua alinihusisha na ninataka nikuhakikishie kwamba pesa za manunuzi zilitokana na biashara na hiyo biashara ni yetu. Naiita ni yetu kwa mantiki mimi ndiye mtoa mtaji kwa 100% na nikamkabidhi kama ajira yake lkn kitega uchumi cha familia.
Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe unawafahamu mleta uzi na mke we?Nimejikuta nawachukia sana watu wanaotoa siri za wapenzi wao hadharani, hivi unadhani nani anajali? inatusaidia nini>? Jifunze kumheshimu mke au mume wako, social media kamwe haiwezi kukusaidia matatizo yako zaidi utaishia kupata majanga zaidi
Huyu mwamba amechemka sana.Mkuu unakosea Sana, yani umpe mke biashara aendeshe halafu usifuatilie mapato?
Wewe ndiye unapaswa uamue matumizi ya mapato sio yeye kujiamulia.
Leo amenunua gari kwa jina lake kesho atajenga nyumba kwa jina lake kitakachofuata hapo ndipo Utajua mke sio ndugu.
Hiyo gari NI kifuta jasho baaada ya kutumikia kazi Fulani akiwa kama alivyozaliwa kuwa makiniMimi ni mwanaume wa kawaida, nimejaaliwa kipato cha wastani tu kinachotokana na juhudi za kujihusisha na hiki na kile kwa kupitia kujiajiri.
Mke wangu pia ni mchakarikaji na anaitumikia biashara ya vyombo vya ndani na mapambo ya ndani ambayo kwa pamoja tuliifungua na inafanya vzr sana.
Tumejaaliwa kuwa na gari moja Suzuki modeli mpya ambayo kiukweli aliinunua yeye mwaka Jana January. Kwasasa mimi ni fundi wa mashine za aina mbalimbali ikiwemo majenereta, magreda, kreni n.k. Na kwa kuwa mishe zangu za kiufundi hazihusishi sana matumizi ya gari ya kutembelea kwahyo huwa naitumia mara chache sana.
Baada ya kumfundisha mkewangu kuendesha akawa nayo kuanzia hapo. Mie Nina pikipiki ambayo hunipeleka huku na kule na kunifanikishia mishughukiko yangu yote bila tashwishi . Ninapohitaji gari kwa ajili ya matumizi ya hapa na pale au ninapoonyesha dalili ya kwamba nitatumia gari siku hiyo, papo hapo mke wangu huanza kujiskia karaha na ataanza kuongea maneno ambayo yanatoa ishara kwamba hataki ntumie gari.
Ukweli sipendezwi na hali hiyo maana inaudhi sana. Kwakuwa nimeshamjulia huwa nampuuza afu nachukua gari naenda kwenye kusudi nililolenga lkn furaha yake hutoweka kwa siku hiyo na hukereka kiukweli. Ingawa mie ndo niliyemfundisha kuendesha lkn pia haniamini napoendesha gari na hapendi nimuendeshe na kila wakati anasikika akinikosoa ninapoendesha, yani huwa dereva namba moja wakati aliyeshika usukani ni mimi.
Na kwa vile ameshajua pia nampuuza katika hilo, mara nyingi mke wangu huamua kukaa siti ya nyuma kwa vile haamini udereva wangu na huona kama nitamsababishia ajali akikaa mbele.
Kwa ufupi hapendezwi ninvyoendesha gari na hili jambo linanikera sana.
NAOMBENI USHAURI WENU WA KUNIJENGA KTK HILI.
Sent using Jamii Forums mobile app
Pole Sana Kaka. Pole Sana kwa mkeo kuwa KERO. Wanawake wenzangu tubadilike jamani. Mume wangu siku anataka kutumia gari.... Namuomba mapema kabisa anipeleke usafiri wa bajaji unapopatikana..... naendelea na ratiba zangu kama kawaida. Nikimaliza narudi nyumbani.... Raha mustarehe... Mapenzi Mubashara[emoji23][emoji28]. Mapenzi yana Raha Sana Wanawake wenzangu ... Haya Mambo madogo madogo haya tujifunze kuya-ignore. Tujifunze kujishusha kwenye baadhi ya mambo ambayo tunaweza kufanya na hayasumbui sana.... Kwani utapungukiwa nini .... Pia Tunapunguza mikwaruzano inayoweza kuepukika. Gari zipo tuu. Cha muhimu Penzi na Raha ya MUME.
Huko ni kuokoa ndoa gani wataishi hivyo mpaka lini? Amani kwake itakuwepo daima? Wauze hilo gari linunuliwe lingine liwe chini ya mume halafu awe anamwachia mkewe,siku akilihitaji anachukua na kutumia. Au wabaki bila gari mana muda si mrefu ataanza kuambiwa unajua pesa ya kununua hili gari ilivyopatikana?Fanya kitu kimoja jizuie kabisa kuanzia leo kupanda gari ilo mkitaka kwenda maali tafuta gari kwa rafiki ili uokoe ndoa.
Sent using Jamii Forums mobile app