Mke wangu hawezi kuandaa milo mitatu kwa wakati na hataki msaidizi wa ndani

Si ulioa mwenyewe silaikwini tako ndebendebe

Ila mkuu si dini inaruhusu muongezee mke mwenza
 
Kwni kipindi mnafanya uchumba hiyo tabia ya uvivu hukuiona.?
Mkuu sikufanya uchumba nae kabisa tulipeleka posa tukapangiwa mahare, tukalipa wazazi wakapanga sherehe pande zote, haikua rahisi kugundua kwamba hajui kusonga ugali au anachelewa kuanda chakula.
 
Ugali pia sio chakula muhimu sana kujua kupika, matajiri wengi hawali ugali.
Mimi sio tajiri mkuu ugali ni chakula muhimu kwetu, usipo jua kuupika unaumiza familia nzima.
 
Si ulioa mwenyewe silaikwini tako ndebendebe

Ila mkuu si dini inaruhusu muongezee mke mwenza
Mkuu hiyo sio issue kwahiyo ntakua nimetatua tatizo hilo.
 
Mimi sio tajiri mkuu ugali ni chakula muhimu kwetu, usipo jua kuupika unaumiza familia nzima.
Ishi kitajiri mkuu, jizoeze kula wali, chapati, ndizi, viazi. Acha kulalamika ugali sio mtamu siju haujaiva.
 
Kimjini mjini sasa milo 2 tu mkuu....hiyo saa 5 au 6 inaitwa brunch...chai/lunch moja kwa 2.....tgen usiku ukiwa vijana kama 4 plus nyie 2 utanishukuru baadae sana.....piga hiyo .....watoto 10yrs to 27yrs wanafukia weee usisikie...wapigishe style hiyoooo
 
Kwahiyo nisubiri atabadilika akiwa amezeeka tayari tumekaa nae zaidi ya miaka 7 sioni mabadiliko yoyote kuhusu hilo.
Mkuu acha mzaha,,Mimi nipo ndani ya ndoa kwa miaka 30 na nimevumilia mapungufu yake na yeye kavumilia yangu.....Mimi sijaiona sababu ya msingi kutoka kwako ya kutomvumilia mke uliyenaye....angekua mke wako ni mshirikina, mzinifu, anatoa siri za ndani, hakupi ushauri katika maisha yenu ninhekuambia moja kwa moja muache.....

Ila kama wewe ni muislam nakushauri uanzishe mfumo wa vyama vingi utasaidia.

Zaidi ya hapo mvumilie, badili fikra zako,,,kama umeweza kuishi nae kwa miaka saba..unaweza kuishi nae mingine saba.
UBARIKIWE NA NAKUTAKIA KILA LA HERI KATIKA NDOA YAKO.
 
Heeee Mungu akusaidie aisee
Yaani na kumsaidia unamsaidia lkn Bado mnachelewa kula?

Hata ugali issue?khaaπŸ™Œ

Hayuko serious au we kaka mpole sn?πŸ˜³πŸ™„
 
Nakuambia mkuu hapa ni kuuziana mbuzi kwenye gunia, na ukimuacha ukapata mgine unaweza kupata mwenye udhaifu zaidi ya huo, wanawake wanaudhaifu mwingi sanaa.
Hapana ni huyo wako tu mkuu, wengine ni madhaifu ya kawaida
Primarily kazi za mwanamke ni pamoja na kupika inakuaje hajui na hapiki kwa wakati?
 
Huyo ni chaguo lako mvumilie tu ndo mapungufu yake wewe mwenyewe una mapungufu yako anakavumilia
 
Dume, maisha ya kisasa ni 50-50, msaidie mkeo!
 
Yani mkuu umeamua kuja kumuanika mkeo huku? Lile somo la wanaume kuwa na friji zinazohandisha hukulisoma?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…