Unamuonea wivu mdogo wake mkeo. Boss wewe ni hatari. Jokes!!
Mimi naona huyo jamaa amepata treatment nzuri sana ambayo labda hajawahi kupata katika maisha yake, mfn mazingira ya hapo home, upendo, vyakula, nidhamu, townlife, kuthaminiwa, uhuru nk. Sasa hivi vitu ni kama vinamfanya arudhishe fadhila, ama niseme kucompensate ili aonekane ni mtu wa faida, ndio maana utamuona ana give back upendo, anatamani afue, apike, aoshe vyombo nk. Hii yote ili asionekane mzigo hapo home na pia aonekane si lelemama. Ni wanaume wa mkoani hua wapo hivyo boss.
Pia nahisi mke wako anakujali sana kukwambia upunguze kitambi uwe kama hilo lijitu, hii ni kwa afya yako, ila kwasababu tayari umeshamchukia lijitu, unaona km vile upo insulted. Kiuhalisia mkeo yupo sahihi sana, jivunie boss kua na mke anaependa ndugu wa kila aina, km mkeo angekua hovyo hayo yote unayoyasema kuhusu hilo lijitu yangefanyika kwa siri mno.