Mke wangu mtarajiwa hataki mtoto wake aliyempata kabla hatujakutana atumie ubini wangu

Mke wangu mtarajiwa hataki mtoto wake aliyempata kabla hatujakutana atumie ubini wangu

Mnasema tu sababu hayajawakuta,hivi unawezaje kuishi na mtoto ambaye unatumia jina la mwingine huku wewe ukimuhudumia kila kitu??
Acha Kutuuliza Maswali Ya ajabu ajabu......aliyekwambia Uvamie Kiwanja Chenye Migogoro ni Nani?

Wewe Hudumia bao la Mwanaume mwenzio...Halafu Huyo mama anamsubiria mtoto wake Apate tu Akili....Akipata tu Akili Atamwambia Huyu Sio Baba Yako ,...Baba Yako Halisi ni Yuleeeee..!
Bro hilo litakuuma kupita Kiasi na ndio Ushamlipia Ada na huduma Zingine...!
 
Wewe na singo maza wako wote mmekosea.

Tukianza na wewe ni kweli unahudumia mtoto, ila hukupaswa kubadilisha ubini bila kukaa na mwenzio mkakubaliana. ULIKOSEA KUFANYA MAAMUZI PEKE YAKO.

Tuje kwa singo maza wako, HAJIHESHIMU NA HAKUHESHIMU, ni kweli ulimkwaza na kumkosea ila ilitakiwa akwambie bila kutumia maneno makali kama "zaa wa kwako"

Kumuacha inawezekana ni sahihi au sio sahihi, hayo majibu yake yanatia mashaka.

Kusomesha mtoto na kufanya kila kitu, FANYA KAMA UNAMLEA YATIMA NA USITARAJIE LOLOTE, UKISHINDWA KUFANYA HIVYO NI BORA UACHE KABISA MAANA UTAUMIA ZAIDI YA HAPO.

Ni mimi singo maza mstaafu.
 
Ingekua tupo kijiweni unatupa hii stori ningekulamba vibao vya kutosha asee una bahati sana

Kuishi na singo mama ni laana labda awe amefiwa mume wake ila huyo ambae bwanaake yupo we unaishi nae wa nn sasa? Yan kamshinda mwanaume mwenzako tena alianza nae akiwa hana mtoto we unaenda kujibebesha limwanamke shindikanaa likiwa na mtoto kabisa?$
 
Safi sana. Kiherehere chako hicho unaona sasa?

Hapo wewe ndo mwenye kosa. Mambo hayo ni muhimu muongee muelewane mapema hata kabla hamjaenda sana kwenye mahusiano ili mnapoingia, kila mtu anajua mipaka yake.

Hapo wewe ulichukulia kwamba kwa kuwa unampenda mama yake na una malengo naye, unaona bora uzike utambulisho wa mtoto ili umuasili moja kwa moja, hili ni jambo jema lakini mjadala mpana unahitajika kabla ya kuja na vitendo.

Huyo mtoto utakuta kwenye cheti chake cha kuzaliwa anatumia ubini wa baba yake sasa wewe unataka kuvuruga.

Upande wa pili pia kuna shida, jifunze kitu hapo, kwa hilo biti na maelezo ya huyo mpenzi wako, naweza kukuambia huna mke hapo. Utakuja kulia chooni na kuendelea kumuhudumia huyo mtoto ni kujipendekeza tu.

Hapo uamue kusuka au kunyoa lakini kichwa kibaki.
 
Wewe na singo maza wako wote mmekosea.

Tukianza na wewe ni kweli unahudumia mtoto, ila hukupaswa kubadilisha ubini bila kukaa na mwenzio mkakubaliana. ULIKOSEA KUFANYA MAAMUZI PEKE YAKO.

Tuje kwa singo maza wako, HAJIHESHIMU NA HAKUHESHIMU, ni kweli ulimkwaza na kumkosea ila ilitakiwa akwambie bila kutumia maneno makali kama "zaa wa kwako"

Kumuacha inawezekana ni sahihi au sio sahihi, hayo majibu yake yanatia mashaka.

Kusomesha mtoto na kufanya kila kitu, FANYA KAMA UNAMLEA YATIMA NA USITARAJIE LOLOTE, UKISHINDWA KUFANYA HIVYO NI BORA UACHE KABISA MAANA UTAUMIA ZAIDI YA HAPO.

Ni mimi singo maza mstaafu.
Umeandika kila nilichokuwa nafikiria mkuu...barikiwa
 
Braza upo vyema kichwani kweli ama ni Afande Swila ndio anaandika hapa? Unampiga chini kisa kakuambia ukweli utachukuaje jina la kwako ukampe mtoto wa mwanaume mwenzio? Ningekuwa mimi ndio ingekuwa fursa ya kuacha mpaka kutoa huduma na kumlipia ada huyo Kelvin. Zaa wa kwako.
 
Back
Top Bottom