Mke wangu mtarajiwa hataki mtoto wake aliyempata kabla hatujakutana atumie ubini wangu

Mke wangu mtarajiwa hataki mtoto wake aliyempata kabla hatujakutana atumie ubini wangu

We m- sverge ikke godt for I gor
Hyo ni dhambi hata kama baba amemtelekeza. Ulipaswa ujadili nae kabla
 
Toa mbegu upate mtoto wa ubini wako. Hilo ndio Jambo la msingi. Huyo mtoto wa kibaka yupo na muache.... Hakuhusu kiasi cha kumbadilisha jina lake la ukoo.
Amefanya la maana kumpiga chini mapemaaa ili arudi huko kwa aliyemzalisha, namshauri asiguse tena single mothers ni pasua kichwa.
 
We m- sverge ikke godt for I gor
Hyo ni dhambi hata kama baba amemtelekeza. Ulipaswa ujadili nae kabla
Hon är dumhet jag gör vad som helst för henne och hennes barn,hon är hjär tlös
 
Huna mbegu za kumzalisha mtoto wa kumwita ubini wako? Acha ubinafsi uliopindukia.

Piga chini ndio. Mwanamke amefanya maamuzi sahihi kabisa. Wanaume wapo tuu.... Tena wa kutosha kwa wanawake wanaojielewa.
Umejibu kirahisi Sana. Sasa kama baba yake yupo kwa Nini analipiwa ada, nguo, madaftari, malazi, matibabu n.k na baba wa kambo?
Na pia kila mtu hukosea Ila majibu ndiyo yanaonesha mtu huyu anafaa au hafai.
 
Mimi Nashauri hivi;
jamaa usimuache mwanamke unaempenda kwasababu ya UBINI wa baba yao.
Kuchana madaftari, hakumaanishi kwamba demu anampenda jamaa aliyezaa nae.
Upendo unanguvu ya kuvuka mipaka ya ukomo mliojiwekea ktk kutoa huduma kwa wanajamii wenu.

Namaanisha, Upendo wako usiwe na mipaka.
Hata ndugu wa huyo mtoto wanaweza kuja kumsalimu kijana wao wakipenda.
Kubadili jina ama ubini wa mtoto kuna taratibu zake, japo si vizuri kubadili ubini wa mtoto kama baba wa kumzaa yupo hai au anajulikana na jamii inayo wazunguka.
Siku moja, atajua kwamba wewe si baba yake mzazi, ataonyeshwa mahali ukoo wake upo,,,,,,, hakika itakusumbua sana.
KIROHO,,,,,,,, ikiwa zitatokea changamoto za kiroho,,,,, mambo ya mizimu na matambiko,,,,,,,,mambo ya kiimani, hakika utapata shida mpaka utakapo mrudisha ktk ukoo wake halisi.

USIMUACHE MDADA,,,,,,,,,, MPENDE NA MUHUDUMIE MWANAE PASIPO KUBADILI JINA LAKE LA UBINI.
Huu ni ushauri mbovu kabisa ...
Ukiendeshwa na hisia za mapenzi badala ya kutumia akili kinachofuata nimaumivu tu !
 
"Kachana madaftrai yote kwa hasira", "zaa wa kwako"
mkuu mtu 7nayedeal nae hapa no hatari kwa maisha yako ya mahusiano na ndoa..

Watu wamepoteza maisha au kuharibikiwa kwakujihusihsa na mahusiaono mabaya..

Umefanya jambo la msingi kuachana nae ..

Now inabidi upate binti mdogo aliyetulia ambaye hajadanga sana na kukubuhu!
 
Misaada tunayowapa watu bila masharti ni misaada yenye scenario za kawaida sana, hata mimi hua ninawasaidia sana watu wenye uhitaji tena bila masharti yoyote lakini

Hii issue ya huyu jamaa ni sensitive sana, naona watu wanaongea tu juu juu kurahisisha mambo, kama jamaa yupo tayari kumsomesha mtoto kuna ugumu gani mtoto kutumia jina lake?
Baba mtoto si yupo hai ana umuhimu gani wa mtoto kutumia jina lake ikiwa wajibu wake unatekelezwa na mwanaume mwingine.

Kwa hiyo nyie mnaona ni vigumu mtoto kubadilisha jina kuliko utayari wa jukumu la kumsomesha alilojipa jamaa?

Kama issue ya kupata watoto wake ni suala la muda la jamaa kulitekeleza, ila ni shida hata watoto wengine wakipatikana tayari wakakuta familia ina matabaka, huyu mtoto anatumia ubini huu, wao wanatumia huu, halafu kwa dalili hizo za huyo mama mtu usikute jamaa atakatazwa hata kumcharaza mtoto bakora kisa sio wake.

Mtoa maada, badilisha jina huyo mtoto then msomeshe, kama mama mtu hataki akamwambie mwenye ubini anaoutetea alete ada.
Kwa mama mwenye uelewa na umuhimu wa elimu asingekukatalia ila hadi anakataa usikute bado anampenda baba wa huyo mtoto na pengine bado wanawasiliana na kushauriana namna ya kukuona wewe boya.
Nazidi kukazi Kama anataka mtoto wa kumpa ubini wake , akazane kupiga mashine,kubadili ubini wa mtoto asiye damu yako kwa kigezo Cha kumlipia vijisenti vya Ada Ni upumbavu wa kiwango Cha lami,nampongeza mwanamke kwa kuwa mwelevu.

Mimi hapa Hadi napata kazi nimesomeshwa na wasamalia wema kwa asilimia 98 lakini hakuna hata mmoja aliyetaka nibadili ubini wangu eti kisa ananilipia gharama za masomo.
 
Natarajia kuoa hivi karibuni na mke mtarajiwa ana mtoto wa miaka 5. Huyu mtoto namhudumia kwa kila kitu na namuonesha upendo wote kama baba yake mzazi.

Kuna shida imejitokeza baada ya kumpeleka mtoto aanze shule (nursery school ). Katika kujiandikisha nikampa jina langu la ukoo (Eg. Ngwengwe) madaftari full mkoba jina nimeandika Kelvin Ngwengwe.

Bhana eeh, mama yake alivyoona madaftari amechana chana, kumuuliza kisa nini mbona umechana madaftari ya mtoto?? Jibu alilonipa limeniacha hoi.

Namnukuu "Huyu mtoto baba yake yupo hai kwanini usitumie jina la ubini wa baba yake mzazi badala yake umetumia jina la ubini wa kwenu! Zaa mtoto wako umuite jina la kwenu"

Maamuzi niliyochukua ni kumpiga chini tu
Takataka huyo mwanamke hana shukrani! Mkuu nimeona hekima yako ya dhati, Hutakiwi kupepesa macho mpige chini aende kwa huko baba wa mtoto alie hai...
 
Nazidi kukazi Kama anataka mtoto wa kumpa ubini wake , akazane kupiga mashine,kubadili ubini wa mtoto asiye damu yako kwa kigezo Cha kumlipia vijisenti vya Ada Ni upumbavu wa kiwango Cha lami,nampongeza mwanamke kwa kuwa mwelevu.

Mimi hapa Hadi napata kazi nimesomeshwa na wasamalia wema kwa asilimia 98 lakini hakuna hata mmoja aliyetaka nibadili ubini wangu eti kisa ananilipia gharama za masomo.
Vijisenti vya ada? Mbona baba mzazi wa mtoto kashindwa kuvilipia?
Kalelewa mtoto wake toka ana mwaka 1 mpaka sasa hivi anayo 5

Halafu bado mnasema vijisenti
 
Vijisenti vya ada? Mbona baba mzazi wa mtoto kashindwa kuvilipia?
Kalelewa mtoto wake toka ana mwaka 1 mpaka sasa hivi anayo 5

Halafu bado mnasema vijisenti
Amwache hivyo hivyo wapo wenye Nia ya kusaidia watu bila mashariti ya ajabu ajabu,nyie ndo huwa mnasaidiwa watu wa jinsia ya kike baadae mnawataka huduma ya ngono!!!
 
Ukiangalia kwa jicho la 3

Mama mtu uwezo wa kukataa kumpa ubini wako mtoto wake hana, hata kama anao ila wema uliomtendea wa kumlea mtoto toka ana mwaka 1 kwa moyo wa mwanamke lazima asingegoma

Why anagoma?

Lazima bado anawasiliana na baba mtoto wake, na huyo baba mtoto wake kamwambia chonde chonde mtoto wangu asibadilishwe jina (wakati huo hajui hata kula ya mtoto, matibabu, wala kuishi ya mtoto wake), ajabu huyo mwanamke ana m protect

Why ana m protect

Bado ana m protect kwa sababu bado huenda anampenda au ana hisia nae, na kitendo cha ku m protect ni indicator moja wapo kua huenda jamaa bado hua anakula mali yako.

Lazima ujifunze ku reason vitu, haiwezekani from no where tu mwanamke akakukatalia tena kwa reaction kubwa hivyo ya kuchana hadi daftari.

Huenda picha ipo hivi unless labda mtoa uzi useme kama baba mtoto yupo hai, au amefariki au ana changamoto yoyote
 
Amwache hivyo hivyo wapo wenye Nia ya kusaidia watu bila mashariti ya ajabu ajabu,nyie ndo huwa mnasaidiwa watu wa jinsia ya kike baadae mnawataka huduma ya ngono!!!
nyie ndo huwa mnasaidiwa watu wa jinsia ya kike baadae mnawataka huduma ya ngono!!!

[emoji115] >> [emoji3][emoji3][emoji3]

Sina neno cause I know who I am, ila kama umeandika kwa kuamini, basi nikujulishe kua sipo hivyo kabisa.

Sema tumefofautiana tu mtizamo na mawazo na kitu ambacho sio dhambi
 
Natarajia kuoa hivi karibuni na mke mtarajiwa ana mtoto wa miaka 5. Huyu mtoto namhudumia kwa kila kitu na namuonesha upendo wote kama baba yake mzazi.

Kuna shida imejitokeza baada ya kumpeleka mtoto aanze shule (nursery school ). Katika kujiandikisha nikampa jina langu la ukoo (Eg. Ngwengwe) madaftari full mkoba jina nimeandika Kelvin Ngwengwe.

Bhana eeh, mama yake alivyoona madaftari amechana chana, kumuuliza kisa nini mbona umechana madaftari ya mtoto?? Jibu alilonipa limeniacha hoi.

Namnukuu "Huyu mtoto baba yake yupo hai kwanini usitumie jina la ubini wa baba yake mzazi badala yake umetumia jina la ubini wa kwenu! Zaa mtoto wako umuite jina la kwenu"

Maamuzi niliyochukua ni kumpiga chini tu
dah pole sana. Baba ake yupo na huduma anatoa
 
Back
Top Bottom