Mke wangu mtarajiwa hataki mtoto wake aliyempata kabla hatujakutana atumie ubini wangu

Baba mzazi wa mtoto yupo hai ,uyu mwanamke mwnyewe anatambua familia ya jamaa ilikataa mimba kwa kigezo cha kabila/mila ..sio baba mtoto wala familia hakuna yotote aliyewahi kutoa hata senti kwa ajili ya mtoto wao.. baada ya kuniambia madhira hayo hivyo nikajiongeza kwa vile mtoto walimkataa nikaona si mbaya akatumia jina langu la ukoo
 
Sasa unataka atumie jina lako umem- adopt??? Vyeti vya kuzaliwa vimeandikwa ubini gani???

Embu usitake kumchanganya huyo mtoto bila sababu ya msingi. Kama ungekuwa na akili na unaona ni jambo la msingi mtoto kutumia jina lako (for whatever reason 😏😏) then ulipaswa kujadiliana na mama yake kabla ya kujipa mamlaka ya kumpatia jina lako.
 
Ni dhambi kubwa sana kubadili ubini wa mtoto asiye wako,nadhani hata ukisoma biblia,katika agano la kale Kama kijana alioa na akafa bila ya kuzaa na mke wake ilibidi ndugu yake wa damu amchukue huyo mke ili azae naye na mtoto huyo alipaswa kuitwa kwa ubini wa Marehemu ,hii yote ilikuwa na Nia ya kuendeleza uhai wa Marehemu,Yani kumfanya aendelee kuishi kiroho.

Hebu chukulia Leo hii wewe una watoto chini ya miaka minne na kwa bahati mbaya unaaga dunia dheni aje mwanamme wa mawazo ya kipuuzi Kama ya mtoa hoja eti ili awasaidie watoto aliomkuta mkeo anao Basi wabadili ubini,naamini huyo mke kwa upande wangu atapatwa na laana kubwa sana, watoto kuendelea kuitwa kwa ubini wa mwanamme Ni baraka katika ulimwengu wa roho.
 
Baba mzazi wa mtoto yupo hai ,uyu mwanamke mwnyewe anatambua familia ya jamaa ilikataa mimba kwa kigezo cha kabila/mila ..sio baba mtoto wala familia hakuna yotote aliyewahi kutoa hata senti kwa ajili ya mtoto wao.. baada ya kuniambia madhira hayo hivyo nikajiongeza kwa vile mtoto walimkataa nikaona si mbaya akatumia jina langu la ukoo.
Familia yao imemkataa kwa kigezo cha kabila na mila kuna sababu ya mtoto kutumia ilo jina?
 
Huyo mwanamke mamsifu kwa ujasiri wake. HiviI huna hata aibu kung'ang'ania mtoto asiye wako?

Huyo mwanamke amekupa changamoto umtungishe Mimba mwanamke ili akuzalie kama una meno wala sioni sababu ya wewe kukasirika.
 
Ha
Sasa unalalamika nini? Kumkataa hakuondoi ukweli kuwa sio damu take.
 
Zaa wa kwako,Tena nakuasa usijaribu kitu Kama hicho,Kama unataka mtoto wa ubini wako piga mashine na Kama huna uwezo wa kuzalisha Basi nenda vituo vya kulelea watoto yatima huko Kuna watoto ambao baba zao na mama zao hawajulikani hivyo utakuwa huru kumpa mtoto ubini wako[emoji849][emoji849]
 
MREJESHO
Jana ugomvi ulikuwa mkubwa ila nilitumia busara nilikaa kimya sikusema chochote alienda mbali zaidi akasema tuachane kimoyo moyo nikasema umeisha.
Leo asubuhi amekuja na mama yake mzazi kusuluhisha ugomvi binti amekiri kuwa amekosa zilikuwa ni hasira tu.
Maamuzi niliyochukua sikupepesa macho nilimwambia mama kuwa siwezi kuendelea na binti yako pia mahari niliyoitoa nimesahmee.
Mpaka sasa simu yangu ina missed call 80 ,sms 30
 
Alichosema mwanamke ni sahihi ila njia iliyotumika sio sahihi shukuru mungu hilo limetokea mapema
 
Ubini wa baba wa kambo sijawahi sikia. Ubini ni wa baba mzazi au kama hajamkomboa ni wa babu mzaa mama, kama unataka mkubaliane umu adopt rasmi kisheria au kimila siyo kiholela kwa kujiamulia.
 
[emoji1666][emoji1666] mkuu popote ulipo agiza chochote kwa bili yangu, Upo sahihi.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
kwahiyo asimlipie ada wala mtoto asimuite baba..
Kumlipia Ada sio kigezo Cha kubadili ubini wa mtoto ambaye ana baba yake halali,Kama anataka mtoto wa bure ili ampe ubini wake aende vituo vya kulelea watoto yatima .
 
Usimlipie ada
Akikuita baba mwambie Mimi sio baba yako
Usimpe zawadi
Mtie mimba,mama yake
Kweli vijana wengine hawana akili kweli Baba mtoto yupo hai kimbelembele cha kumlipia Ada kina kujaje? Kwanin asisomeshe watoto yatima wapo wengi wenye huitaji
 
Wewe bado mtoto mdogo Sana kifikira, narudia Tena zaa mtoto wako umpe ubini wako sio kung'ang'ana na sperm za wanaume wenzako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…