Mke wangu mtarajiwa hataki mtoto wake aliyempata kabla hatujakutana atumie ubini wangu

Mke wangu mtarajiwa hataki mtoto wake aliyempata kabla hatujakutana atumie ubini wangu

Natarajia kuoa hivi karibuni na mke mtarajiwa ana mtoto wa miaka 5. Huyu mtoto namhudumia kwa kila kitu na namuonesha upendo wote kama baba yake mzazi.

Kuna shida imejitokeza baada ya kumpeleka mtoto aanze shule (nursery school ). Katika kujiandikisha nikampa jina langu la ukoo (Eg. Ngwengwe) madaftari full mkoba jina nimeandika Kelvin Ngwengwe.

Bhana eeh, mama yake alivyoona madaftari amechana chana, kumuuliza kisa nini mbona umechana madaftari ya mtoto?? Jibu alilonipa limeniacha hoi.

Namnukuu "Huyu mtoto baba yake yupo hai kwanini usitumie jina la ubini wa baba yake mzazi badala yake umetumia jina la ubini wa kwenu! Zaa mtoto wako umuite jina la kwenu"

Maamuzi niliyochukua ni kumpiga chini tu

MREJESHO
Jana ugomvi ulikuwa mkubwa ila nilitumia busara nilikaa kimya sikusema chochote alienda mbali zaidi akasema tuachane kimoyo moyo nikasema umeisha.

Leo asubuhi amekuja na mama yake mzazi kusuluhisha ugomvi binti amekiri kuwa amekosa zilikuwa ni hasira tu.

Maamuzi niliyochukua sikupepesa macho nilimwambia mama kuwa siwezi kuendelea na binti yako pia mahari niliyoitoa nimesahmee.
Mpaka sasa simu yangu ina missed call 80, sms 30

Mtoto kama unamlea wewe inamaana we ndo baba yake. Utambulike kila legal father. Huyo atakusumbua snaa kaka
 
Umechukua maamuzi sahihi.

Ulifanya kosa kuingiza timu uwanjani wakati ubao unasoma 1-0 dhidi yako. Ila nafurahi kuona ukashtuka katikati ya safari na kufanya maamuzi sahihi.

Wanawake wengi huwa wanaolewa na wanawaume ambao hawawapendi, ila ndo wanaume ambao wamekutana nao wakiwa tayari kuoa na ndoa ni ya mwanamke sio ya mwanaume.

Kwa hiyo huyo anampenda huyo aliyembebea mimba, na huyo mtoto ni alama ya huo upendo. Kwako wewe kafuata pesa tu.
 
Wote wawili wana makosa. Kosa la kwanza, kuishi na mwanamke ambaye ametelekezwa na mwanaume wake tena mtoto akiwa na mwaka mmoja tu. Kama ungetaka kumsaidia ungemsaidia bila kuishi naye. Pili, kutaka kubadilisha jina bila makubalianao. Kisheria huwezi badilisha jina la mtoto bila kufuata utaratibu. Mwanamke hana mapenzi ya kweli, alikuwa anatafuta hifadhi tu . Unatelekezwa na mtoto mwaka mmoja unakuwa na ujasiri gani wa kuishi na mwanaume mwingine? Pia hakutumia busara kuchana daftari na kutoa lugha chafu. Uamuzi ni wako, kusuka au kunyoa. Kama unampenda mkae mjadiliane kuhusu jina la mtoto na jinsi ya kumlea. Pia usimlazimishe kuzaa mtoto mwingine ili hali hamjafunga ndoa maana anaogopa kuwa single mother squire.
 
Baba anahudumia? Ili mradi awe na ubini tu wa baba ake sio
Suala ni hili jamaa amekubali kulea mtoto ambaye sio wakwake, na anajua fika baba yake na mtoto yupo, sasa kuna ulazima gani wakuweka ubini wako ili hali unajua kabisa mtoto si wakwako na umemkuta tayari amekwisha zaliwa?
huo ni ugomvi wakujitakia tu
angalau mwanamke akitelekezwa akiwa mjamzito kisha ukawa umemchukua kidogo hata kuweka ubini wako inakuja ili kwa ajili yakulinda heshima tu ya ndoa na familia kwa ujumla.
mwanaume alipaswa wake chini na mwanamke ili wajadiliane kwanza
japo ashukuru Mungu bomu lililolipuka limemwepusha na majanga 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂
 
Ulikuwa unatafuta sababu ya kumwacha tu.
Ashakum si matusi. Yaani katika watu maboya wewe unaongoza. Unajua wazi kuwa mtoto syo wako na unakiri umemkuta, Sasa unamwandikisha kwa jina la kwenu ili iweje? Halafu hata huyo mama yake hukumshirikisha usikie atasema nini.
Hata kama ingekuwa baba mzazi wa mtoto hamhudumii bado huna uhalali wa kumwita ubin wa kwenu.
Fanya bidii umpate wako Kama alivyokushauri mama mwenye mtoto/mkeo
A woman is not going to respect you

If she can throw you off of your purpose

By sex and tantrum

Retain and learn to control your urges
 
Wanaume tunatofautiana sana hivi hizo nguvu za kumuita mtoto wa wawatu jina lako ulizitoa wapi,kitu ambacho inatakiwa ujue before u alikuwepo mwanaume anapendwa na ata zaidi yako na kumpata huyo mwanamke ni sababu yule aliyekuwa anampenda alimtelekeza..kwahyo usijipe majukumu yasiyo yako cha msingi we mzalishe watoto wako ata sita watatosha kuitwa kwa jina lako Full stop.
 
Ulitaka ubambikiwe second hand material mtumba kwisha kazi.
Mwambie akwendre na litoto lake. Single mothers ni special Kama michepuko tu sio ndoa.
Mwenye kusikia wosia huu anitumie vocha
 
Hongera sana jamaa umefanya Jambo la busara sana na nashangaa watu mnaomtetea huyo Dada,baba sio kuzalisha baba ni kuhudumia.Nitatoa mfano kwangu baba yangu alimuoa mama yangu akiwa na mtoto tena nadhani wa miaka mitatu Mimi nlizaliwa wakati huyo Dada yangu amefika miaka sita kwa maana tumeachana miaka sita huyo Dada yangu alikua anatumia jina la baba yangu ambaye ndo alimlea Kama mleta mada hapo,na baada ya hapo wakapata watoto wengine wawili mbali na Mimi kwa hiyo tukawa wanne,hamuwezi amin nilikuja kujua huyu sister sio baba yake mzee wangu nikiwa form 3 tena kutokana na shangazi zangu kunitambulishaga kuwa Mimi mtoto wa kwanza kwa Kaka yao,na hiyo imetufanya tupendane na Dada yetu mno kwa kuwa mzee hakuwahi kutubagua na pia cha kushangaza huyo sister yangu anampenda sana mzee kuliko mama, hakuwahi kutaka kumjua baba yake wala familia ya huo ukoo wao.
 
Back
Top Bottom