Mkeo aliwahi kukulaza lock up, baada ya kutoka maisha yalikuwaje?

Shemeji yako ni dhaifu sana,
Wagombane alafu baba mwenye nyumba ndio anakimbia mji, hii ni huzuni
 
Nitachukua huo ushauri kama tunaishi nyumba ya kupanga,lakini kuacha nyumba niliyojenga ni ngumu
 
Mbona makosa yamekua ya wife tena? Kiukweli hapo we ndo umezingua.

Ila sometimes hawa wamama wanakera
Kosa kubwa mashosti.....hapo ndoa inakufa taratibuu.....ukute kumpiga kuna uhusiano na mashosyi.....mbaya kabisa....wameshamuuza huyo.....yaani unawakuta counter na mashosti huyo mke wako au hawala wa mrtaani..??
 
Epuka kupigana na mkeo ili ushinde hoja ,jaribu kupata muda wa kusiliza hoja zake kisha mwambie akupe muda wa kufikiria na kesho mkiwa mmetulia mpe jibu kwa nini unaona wewe uko sahihi,baada ya kipigo na polisi hamwez
 
Sasa wewe umempiga yeye kakulaza ndani, si umsamehe maisha yasonge.
Maan hata wewe pia ulikua na kosa mwanamke ukumzaa, hukumbebea mimba iweje umpige.

Kwani kwenye vikao vya wanaume hamfunzani mwanamke anapigwa na nin duh.
Rudi nyumbani achana na ushauri wa mabachela humu ambao hawajui hata mahari zinalipwaje.
 
Halafu baada ya kutoka huko mahabusu unategemea Kuna ndoa hapo?
 
Huyo sio wakusamehe mzeya
 
Potea miezi mitatu net dunia imfunze hakikisha hauna mawasiliano nae kabisa ila tumia njia za kiinteligensia kujua maendeleo ya watoto wako.. hakikisha hauna huruma kabisa mwache dunia imfunze kwanza na ukirudi usiwe na time nae kabisa ishi nae kama unaishi na adui yeye ndo ateseke kutafuta uwepo wako. Hakikisha ukirudi usiwe tena mwema kama ulivyokua mwanzo ajue kabisa yeye ndo source ya wewe kubadilika fanya hivyo kwa miezi mingine mitatu alafu tulia. Ukilegeza kamba daima lockup ndo itakua nyumbani kwako .
 
Kwani kama ndoa imekufa na uhai umekufa.
Kinachonishangaza kwa wanawake (Sina maana ya wewe) ni jinsi wanavyozitafuta na kuzitafuta ndoa Lakini wakato huohuo hawako tayari kuzingatia yale ya ndoa. Yaani ndoa Haina maana yoyote kwako Lakini wanakesha kwa manabii na mitume na novena kibao kutafuta ndoa hiyo hiyo ambayo hata km ikifa na uhai haufi.
 
Mimi nilimshushia kipigo wife tar 2 Dec, akaenda kukata RB halaf akawakataza askari wasinikamate ila anatembea na RB, kisha siku nipo kazini kabeba wanangu na hati ya nyumba na kadi ya gari akakimbilia kwao.
Akanifungulia kesi gender desk polisi kisha baraza la kata anadai taraka. Kwakifupi hapo ndio kakamatia gia. Divorce.
 
Mkuu ndoa ni masikilizano baina ya wawili,Ndoa ni furaha ndoa ni kujishusha,kusameheana na kitu ambacho Wanaume wengi hawana wao ni ubabe.
 
Mkuu ndoa ni masikilizano baina ya wawili,Ndoa ni furaha ndoa ni kujishusha,kusameheana na kitu ambacho Wanaume wengi hawana wao ni ubabe.
Uko sahihi Lakini kwa kiasi Fulani TU. Kila taasisi (ya ndoa ikiwemo) Ina masharti yake. Mwanafunzi (shule) Ina masharti au taratibu zake, kabisa, msikiti, chama Cha siasa, familia, nk nk zote hizi Zina taratibu zake. Ndoa (muunganiko wa watu wawili) nayo Ina taratibu zake na kwa asili yake na Mila na desturi za mahali, mwanaume ni mtawala wake. Ukikuta mwanaume anampiga mkewe ni kwa sbb taratibu za ndoa zimevunjwa (unless huyo mwanaume ana changamoto ya afya ya akili) na dawa ya kupigwa na mme sio polisi kwa kuwa kufanya hivyo ni sawa na kuivunjilia mbali taasisi hiyo. Mimi si muumini wa mapigano ktk ndoa Lakini najua vita hivyo hutokana na kutojitambua
 
GBV haikubaliki popote pale shukuru umetolewa nchi zingine ungeisoma namba haijalishi ni mke wako wa ndoa au lah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…