Mkeo aliwahi kukulaza lock up, baada ya kutoka maisha yalikuwaje?

Si wanasema hayashauriki? Sasa leo nakushauri baba yangu mzazi aliwahi kuniambia ,mkeo ikitokea kakulaza ndani ukitoka awe kashaondoka . Na kwa scenario yako inaonekana hao mashoga zake walimpa chachandu la kutosha akajaa hana akili huyo mkeo kashikiwa na mashoga zake ,ukisamehe haraka umeisha watajiona washindi cha kufanya dengua mwanzo mwisho ,anzisha visa visa ongea maneno mazito na mashoga piga marufuku , sasa jidai ooooh baby wawoooooh im sorrrey honeeey ,

Mamaqe sorry ya nyokwe
Kwahiyo baba yako ni malaika, halafu wazee wanafiki kama huyo ndiyo hao unakuta hata watoto anaosema wake wanakuwaga ni walezi tu kujifanya ubabe
 
Hapo wote muna makosa kikubwa unapofanya maamuzi tumia hekima na busara ikuongoze mkuu watu humu wanashauri ushauri tofauti wengine wanasema muachane tafuta mke mwingine la asha halmashauri na maisha yako ww ndio unajua umwache au msameeane maisha yaendelee kingine ushauri unaopewa chuja si kila anayeshauri basi ufate ushauri wake maisha ni yako mkuu akili kichwani mwako
 
Hali zenu?

Wakuu, siku ya jumatano majira ya saa 1 jioni nikiwa nimefika nyumbani kutoka mihangaikoni, kulitokea kutokuelewana na wife,nikajikuta napandwa na hasira nikamshika nikachomoa mkanda wangu wa suruali nikamtandika nao hatari alivyopata upenyo akakimbilia nje.

Kumbe mashosti zake wakawa wamemshauri akimbilie kushtaki polisi, akaenda kituo cha police kushtaki,baada kama ya lisaa hivi nikasikia nagongewa na balozi wa nyumba kumi akiwa kaambatana na Askari polisi wawili, wakaniambia nahitajika kituo cha police kwani mke wangu kaenda kushtaki kuwa nimempiga.

Sikuwa mbishi nikawaomba nibadili nguo na niweke mazingira ya nyumba sawa kwani watoto na dada wa kazi hawapo.

Basi bana nikafika kituo cha police pale kaunta nikamkuta wife kakaa yuko na mashosti zake kama wawiili nikachukuliwa maelezo yangu kisha nikafunguliwa kesi ya shambulio la kudhuru mwili, nikaingizwa lock up, kwa sababu ilikua usiku afande mmoja hivi akaniambia kosa linadhaminika kama kuna jamaa zangu wako around niwacheck waje wanidhamini

Lakini pia akanishauri kwa jinsi anavyoona nina hasira bora nilale tu mle lock up kuepusha madhara kwani nikisema nitoke usiku ule ningeweza kumdhuru zaidi wife na pale lock up ni sehemu salama zaidi. Basi nikawa nimemuelewa yule afande nikatulia mpaka asubuhi,kulivyokucha nikaomba simu yangu pale kaunta nikawapigia jamaa zangu wakaja wakaniwekea dhamana.

Hapa nilipo toka nitoke lock up nimeona nikae kwanza kwa jamaa angu kujiepusha na huyo mwanamke,ameisha enda police mwenyewe kuwaambia hana nia ya kuendelea na hiyo kesi hivyo anaomba ifutwe, Askari kama kawaida wamemtoa pesa kidogo.

Sasa toka jana naona ananitumia watu kuja kumuombea msamaha kuwa alikosea kunilaza lock up.

Hapa niko stranded nimsamehe au nimfanyaje na baada ya kumsamehe maisha yetu hapo ndani yatakuwaje?

Kama kuna yeyote amewahi kupitia hii changamoto anisaidie mawazo.
Yaweza tafsiriwa kuwa amekosea n ..Ila umekosea pia mzee.

Ambacho amefanya kimeweza kukushtua pia kuwa uwe na mipaka...

Kaka, kuua ni Jambo linaloweza tokea kwa haraka Sana...na naamin ulipokuwa lock up ulitafakari mengi...ule ugumu wa kuwa lock up kwa masaa machache Nina Imani kabisa utaogopa kurudia makosa ya hivyo...

Ya Kupiga yanatokea...haipaswi kuwa Sana.
 
Msamehe. Itisheni kikao kitachoongozwa na watu mnaowaheshimu kwa lengo moja tu la kuombana msamaha na kusameheana. Una makosa kwa kumshambulia mkeo, haifai. Wewe ni chanzo cha yeye kwenda polisi. Omba msamaha kwa kipigo usione haya. Kisha muendelee mbele sahau yaliyopita. uzuri wanaume friji zetu kubwa na zinagandisha, huwezi hata kuweka kinyongo ukisha aamua kusahau
Aombe msamaha mwanaume! haupo sawa wewe.
Vikao vya ndoa havijawahi kuimarisha ndoa.
Hapo wawili wakutane wao peke yao,wajadiliane kama kuna haja ya kuendelea na ndoa ama la.
Wakiona.faida za kuendelea na ndoa waanze upya,wakiona hawawezi kudhibiti hasira zao kila mtu aendelee na maisha yake.
 
Yaweza tafsiriwa kuwa amekosea n ..Ila umekosea pia mzee.

Ambacho amefanya kimeweza kukushtua pia kuwa uwe na mipaka...

Kaka, kuua ni Jambo linaloweza tokea kwa haraka Sana...na naamin ulipokuwa lock up ulitafakari mengi...ule ugumu wa kuwa lock up kwa masaa machache Nina Imani kabisa utaogopa kurudia makosa ya hivyo...

Ya Kupiga yanatokea...haipaswi kuwa Sana.
Kuna wanawake bila kubondwa akili hazikai pahala pake.
 
Aombe msamaha mwanaume! haupo sawa wewe.
Vikao vya ndoa havijawahi kuimarisha ndoa.
Hapo wawili wakutane wao peke yao,wajadiliane kama kuna haja ya kuendelea na ndoa ama la.
Wakiona kuna faida za kuendelea na ndoa waanze upya,wakiona hawawezi kudhibiti hasira zao kila mtu aendelee na maisha yake.
 
Wewe ndo mwenye maamzi mkuu na unajua ukweli wa na uzito wa hicho kipigo ulicho mpiga.

Je kosa lilikuwa kubwa sana hadi ukampiga? ni mara ngapi una mpiga?.
Mimi siwezi kumpiga ni kitendo cha kumwambia fata fimbo lala nikuadhibu kama njia ya kujutia kosa lake akigoma huna mke make plan nyingine.

Mwanamke akokosea huwa chini sana kukubali shaishe lakini wewe ulimshambulia tena kwa mkanda.Laza chini tandika fimbo5 halafu simamia ukucha
 
Wewe ingekuwa mi ndo huyo mkeo, ningempa na buku 10 poti akushughulikie vizuri ili ukirudi uraiani uwe raia mwema. Huna adabu, unapigaje mkeo na mkanda ukimuua??

Mwambie mkeo anitumie namba nimtumie pesa ya soda, kanifurahisha sana’aaa.!! 😹🤣
 
Kwa hiyo yeye alivyompiga mwenzie sio kosa safi sana kwa huyo bibie iwe funzo kwa wenzie🐒,Kwanza ulimshushia kipigo kikali sana mpaka akakupeleka police na huenda ndio tabia yako kumpiga ila siku hiyo ulizidisha dozi hata ningekuwa mimi ningekulaza Selo dadekii.
Huyu ilitakiwa achapike vidole vivimbe km virungu vya bendi hata kutype kutupa habari ashindwe 😹😹😹

Hii story yake ilitakiwa atupe baada y’a mwaka, baada ya kupona 🤣
 
Msa
Hali zenu?

Wakuu, siku ya jumatano majira ya saa 1 jioni nikiwa nimefika nyumbani kutoka mihangaikoni, kulitokea kutokuelewana na wife,nikajikuta napandwa na hasira nikamshika nikachomoa mkanda wangu wa suruali nikamtandika nao hatari alivyopata upenyo akakimbilia nje.

Kumbe mashosti zake wakawa wamemshauri akimbilie kushtaki polisi, akaenda kituo cha police kushtaki,baada kama ya lisaa hivi nikasikia nagongewa na balozi wa nyumba kumi akiwa kaambatana na Askari polisi wawili, wakaniambia nahitajika kituo cha police kwani mke wangu kaenda kushtaki kuwa nimempiga.

Sikuwa mbishi nikawaomba nibadili nguo na niweke mazingira ya nyumba sawa kwani watoto na dada wa kazi hawapo.

Basi bana nikafika kituo cha police pale kaunta nikamkuta wife kakaa yuko na mashosti zake kama wawiili nikachukuliwa maelezo yangu kisha nikafunguliwa kesi ya shambulio la kudhuru mwili, nikaingizwa lock up, kwa sababu ilikua usiku afande mmoja hivi akaniambia kosa linadhaminika kama kuna jamaa zangu wako around niwacheck waje wanidhamini

Lakini pia akanishauri kwa jinsi anavyoona nina hasira bora nilale tu mle lock up kuepusha madhara kwani nikisema nitoke usiku ule ningeweza kumdhuru zaidi wife na pale lock up ni sehemu salama zaidi. Basi nikawa nimemuelewa yule afande nikatulia mpaka asubuhi,kulivyokucha nikaomba simu yangu pale kaunta nikawapigia jamaa zangu wakaja wakaniwekea dhamana.

Hapa nilipo toka nitoke lock up nimeona nikae kwanza kwa jamaa angu kujiepusha na huyo mwanamke,ameisha enda police mwenyewe kuwaambia hana nia ya kuendelea na hiyo kesi hivyo anaomba ifutwe, Askari kama kawaida wamemtoa pesa kidogo.

Sasa toka jana naona ananitumia watu kuja kumuombea msamaha kuwa alikosea kunilaza lock up.

Hapa niko stranded nimsamehe au nimfanyaje na baada ya kumsamehe maisha yetu hapo ndani yatakuwaje?

Kama kuna yeyote amewahi kupitia hii changamoto anisaidie mawazo.
Msamehe tuu maana sio tukio la kupeana talaka hili ...lakin je Kwan moyo wako hausemi samehe??
 
Back
Top Bottom