Econometrician
JF-Expert Member
- Oct 25, 2013
- 16,879
- 31,253
Kwahiyo baba yako ni malaika, halafu wazee wanafiki kama huyo ndiyo hao unakuta hata watoto anaosema wake wanakuwaga ni walezi tu kujifanya ubabeSi wanasema hayashauriki? Sasa leo nakushauri baba yangu mzazi aliwahi kuniambia ,mkeo ikitokea kakulaza ndani ukitoka awe kashaondoka . Na kwa scenario yako inaonekana hao mashoga zake walimpa chachandu la kutosha akajaa hana akili huyo mkeo kashikiwa na mashoga zake ,ukisamehe haraka umeisha watajiona washindi cha kufanya dengua mwanzo mwisho ,anzisha visa visa ongea maneno mazito na mashoga piga marufuku , sasa jidai ooooh baby wawoooooh im sorrrey honeeey ,
Mamaqe sorry ya nyokwe
Yaweza tafsiriwa kuwa amekosea n ..Ila umekosea pia mzee.Hali zenu?
Wakuu, siku ya jumatano majira ya saa 1 jioni nikiwa nimefika nyumbani kutoka mihangaikoni, kulitokea kutokuelewana na wife,nikajikuta napandwa na hasira nikamshika nikachomoa mkanda wangu wa suruali nikamtandika nao hatari alivyopata upenyo akakimbilia nje.
Kumbe mashosti zake wakawa wamemshauri akimbilie kushtaki polisi, akaenda kituo cha police kushtaki,baada kama ya lisaa hivi nikasikia nagongewa na balozi wa nyumba kumi akiwa kaambatana na Askari polisi wawili, wakaniambia nahitajika kituo cha police kwani mke wangu kaenda kushtaki kuwa nimempiga.
Sikuwa mbishi nikawaomba nibadili nguo na niweke mazingira ya nyumba sawa kwani watoto na dada wa kazi hawapo.
Basi bana nikafika kituo cha police pale kaunta nikamkuta wife kakaa yuko na mashosti zake kama wawiili nikachukuliwa maelezo yangu kisha nikafunguliwa kesi ya shambulio la kudhuru mwili, nikaingizwa lock up, kwa sababu ilikua usiku afande mmoja hivi akaniambia kosa linadhaminika kama kuna jamaa zangu wako around niwacheck waje wanidhamini
Lakini pia akanishauri kwa jinsi anavyoona nina hasira bora nilale tu mle lock up kuepusha madhara kwani nikisema nitoke usiku ule ningeweza kumdhuru zaidi wife na pale lock up ni sehemu salama zaidi. Basi nikawa nimemuelewa yule afande nikatulia mpaka asubuhi,kulivyokucha nikaomba simu yangu pale kaunta nikawapigia jamaa zangu wakaja wakaniwekea dhamana.
Hapa nilipo toka nitoke lock up nimeona nikae kwanza kwa jamaa angu kujiepusha na huyo mwanamke,ameisha enda police mwenyewe kuwaambia hana nia ya kuendelea na hiyo kesi hivyo anaomba ifutwe, Askari kama kawaida wamemtoa pesa kidogo.
Sasa toka jana naona ananitumia watu kuja kumuombea msamaha kuwa alikosea kunilaza lock up.
Hapa niko stranded nimsamehe au nimfanyaje na baada ya kumsamehe maisha yetu hapo ndani yatakuwaje?
Kama kuna yeyote amewahi kupitia hii changamoto anisaidie mawazo.
Aombe msamaha mwanaume! haupo sawa wewe.Msamehe. Itisheni kikao kitachoongozwa na watu mnaowaheshimu kwa lengo moja tu la kuombana msamaha na kusameheana. Una makosa kwa kumshambulia mkeo, haifai. Wewe ni chanzo cha yeye kwenda polisi. Omba msamaha kwa kipigo usione haya. Kisha muendelee mbele sahau yaliyopita. uzuri wanaume friji zetu kubwa na zinagandisha, huwezi hata kuweka kinyongo ukisha aamua kusahau
Kuna wanawake bila kubondwa akili hazikai pahala pake.Yaweza tafsiriwa kuwa amekosea n ..Ila umekosea pia mzee.
Ambacho amefanya kimeweza kukushtua pia kuwa uwe na mipaka...
Kaka, kuua ni Jambo linaloweza tokea kwa haraka Sana...na naamin ulipokuwa lock up ulitafakari mengi...ule ugumu wa kuwa lock up kwa masaa machache Nina Imani kabisa utaogopa kurudia makosa ya hivyo...
Ya Kupiga yanatokea...haipaswi kuwa Sana.
Usingeandika tusingejua kiwango cha ujinga wako.Kwahiyo baba yako ni malaika, halafu wazee wanafiki kama huyo ndiyo hao unakuta hata watoto anaosema wake wanakuwaga ni walezi tu kujifanya ubabe
Aombe msamaha mwanaume! haupo sawa wewe.
Vikao vya ndoa havijawahi kuimarisha ndoa.
Hapo wawili wakutane wao peke yao,wajadiliane kama kuna haja ya kuendelea na ndoa ama la.
Wakiona kuna faida za kuendelea na ndoa waanze upya,wakiona hawawezi kudhibiti hasira zao kila mtu aendelee na maisha yake.
Kila lakheri mwakinyo, utakuja baini kuwa ngumi sio suluhisho ukiwa umechelewa pengine ushauwa wakati huoKuna wanawake bila kubondwa akili hazikai pahala pake.
asante mpigania haki ya jinsiaKila lakheri mwakinyo, utakuja baini kuwa ngumi sio suluhisho ukiwa umechelewa pengine ushauwa wakati huo
Yeye alivyo mpiga mwenzie hajanzigua
Daaa, hilo nalo neno kinga ni bora kuliko tibakazingua sana hafai kuendelea nae kama anathubutu kufanya hayo ipo siku atashauriwa akutilie sumu.
Huyu ilitakiwa achapike vidole vivimbe km virungu vya bendi hata kutype kutupa habari ashindwe 😹😹😹Kwa hiyo yeye alivyompiga mwenzie sio kosa safi sana kwa huyo bibie iwe funzo kwa wenzie🐒,Kwanza ulimshushia kipigo kikali sana mpaka akakupeleka police na huenda ndio tabia yako kumpiga ila siku hiyo ulizidisha dozi hata ningekuwa mimi ningekulaza Selo dadekii.
Alete lipa namba namie nna kisalio hapaWewe ingekuwa mi ndo huyo mkeo, ningempa na buku 10 poto akushughulikie vizuri ili ukirudi uraiani uwe raia mwema. Huna adabu, unapigaje mkeo na mkanda ukimuua??
Mwambie mkeo anitumie namba nimtumie pesa ya soda, kanifurahisha sana’aaa.!! 😹🤣
Msamehe tuu maana sio tukio la kupeana talaka hili ...lakin je Kwan moyo wako hausemi samehe??Hali zenu?