Mkeo ni wa kundi gani kati ya haya?

Mkeo ni wa kundi gani kati ya haya?

.....................Sikuwahi kuchunguza sana kuhusu mabadiliko niliyokuja kuyaona miaka michache baada ya ndoa but nachokumbuka mwanzo ama akini-ectia ama ni mabadiliko tu yalitokea ila alikuwa smart sana kwenye maamuzi na uelewa (sisemi kwamba sasa hivi hayupo smart) ila amenifanya nizidi kuishi nae kwa akili sana.

Nachoweza kusema na kwa experience yangu ndani ya ndoa miaka 8 sasa ni kwamba kadiri mnavyoongeza familia ndivyo na tabia za mkeo zinavyoanza kubadilika,(haijalishi ni understanding au non-understanding)hakuna siku atakutukana ila baadhi ya huduma ulizokuwa ukipewa zamani bila kuuliza itakubidi wewe mwenyewe uanze kujifanyia na wala usithubutu kuuliza omba uwe na hekima ya kujua mapema maana ya mabadiliko hayo lah hukujua utaitumbukiza ndoa kwenye vurugu,personally miaka ya mwanzo akinitengea maji ya kuoga,kuninyooshea nguo,kunipakulia chakula nikirudi home anapokea kama mkononi nina kimfuko au bag atakuja kupokea ila baada ya kupata mtoto wa kwanza hiyo ya kuwekewa maji ya kuoga na kuandaliwa nguo zilikufa nikabaki na favor mbili,kupokewa mzigo mwenyewe nilikataa nikaona kama utumwa sasa tuna watoto wawili hii ya kupakuliwa chakula muda wowote naona itakufa.

Obviously malalamiko mengi ya wanaume kwenye ndoa hutokana na huduma fulani kukatwa ghafla na majibu yasiyotegemewa kutoka kwa wake zao pale wanapouliza sababu,nilichogundua;anakuwa busy zaidi na watoto so hawezi kuacha kumlisha mtoto akakuandalie wewe maji ya kuoga,hawezi kuacha kumnyonyesha mtoto au kumuandaa mtoto awahi school bus akakunyooshee nguo also hawezi kuacha kumuogesha mtoto akakupakulie chakula mezani sasa ukiwa macho juu juu utataka kuhoji “inakuwaje zamani ukifanya hiki na hiki mbona sasa hivi hunifanyii” jibu utakalopewa hapo ndo litakaloamua hatma ya ndoa yenu,binafsi nachoshukuru niliweza ku-match na mabadiliko haya mapema na nachowashauri mnaotaka kuingia kwenye ndoa jueni mke siyo kwa ajili ya kukuhudumia wewe kwa kila kitu wanaopaswa kuhudumiwa kwa kila kitu na yeye wewe pia ukishiriki ni watoto wenu mtakaowazaa.

Well.....vurugu zipo na ieleweke tukubali au tukatae wanawake % kubwa wanafanana akili awe amesoma au hakusoma hakuna mwanamke anayekataa au anayekubali kosa kizembe,ni “kuishi nao kwa akili tu” ukiijua sentence hii na ukakubali ikuongoze kwenye arguments na mkeo ndoa utaiona tamu tofauti na hapo ni pigo.
Ndoa inahitaji hekima na busara na sio upendo tu peke yake.

Umenena vyema.
 
Wale tunaotumaga msg ndefuuuuuuuu za malalamiko tuko kundi lipi?
Ina maana huoni kabisa hapo, wazee wa magazeti dawa yenu majibu mafupi mafupi tu. Ok!...Sawa!...Poa! huwa yanapendeza sana.
 
  • Thanks
Reactions: amu
Mke wangu kundi la pili.
Hawezi kukiri kosa hata kama sababu zipo wazi kama kakosea. Kuomba msamaha sikumbuki ni mwaka gani na anachotaka yeye ukimshauri kinyume chake fahamu mada itabadilika na utaonekana mkosaji. Kususa na kuchukia jambo dogo tu ni kawaida saaana. Ila nikimwambia ntakuacha atalia huyo hadi umuonee huruma hahahaha.
Binafsi kuna baadhi ya mambo yupo sawa sana na huwa sioni taabu ya vitabia vyake.
Ila ndio vile nshamzoea na maisha yanasonga.
Mkeo ni kama mbilimbi 🤣🤣🤣 mchachu ila akipikwa mtamu.
 
Dawa yao wa kundi la pili kuwaonesha ulichofanya ukiwashirikisha jambo kabla unaleta mvurugano.
Eeh nafikiria ni approach nzuri zaidi, aoneshwe matokeo tu sio process maana anaweza kukukatisha tamaa.
 
Ukweli sijui kama kuna wanaume wapo wanaopenda hao kundi la pili? maana hao ni kipengele.
Hao namba 2 ubaya wao wengi ni impostors at first sight.

Ukianzana nae anakuwa kama namba 1 ila mkishafika mbali sana anakuchenjia gia angani anaanza kuishi katika tabia zake halisi ambazo ni za namba 2!

Hapo ndio utajua hujui kudadadeki😂😂😂!!!
 
Back
Top Bottom