moj6
JF-Expert Member
- Nov 2, 2017
- 3,354
- 4,985
hahaaa upo namba 2 hapo my?
Wale tunaotumaga msg ndefuuuuuuuu za malalamiko tuko kundi lipi?
[/QUOT
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wale tunaotumaga msg ndefuuuuuuuu za malalamiko tuko kundi lipi?
[/QUOT
Ukiwa tayari kuolewa, nichekiNiko namba 1 hapo ila ndo mpaka unikojo...... ukichelewa naswitch no 2 hii hata Mi mwenyewe najiogopaga sometimes
Lakini kwa ujumla maisha yangu ya mahusiano asilimia nyingi naishi kwenye moja,
HahahahaNipo kote
Umefurahi mwenyeweHahahaha
Safi ,sometimes yes ,sometimes noUmefurahi mwenyewe
Ndoa inahitaji hekima na busara na sio upendo tu peke yake......................Sikuwahi kuchunguza sana kuhusu mabadiliko niliyokuja kuyaona miaka michache baada ya ndoa but nachokumbuka mwanzo ama akini-ectia ama ni mabadiliko tu yalitokea ila alikuwa smart sana kwenye maamuzi na uelewa (sisemi kwamba sasa hivi hayupo smart) ila amenifanya nizidi kuishi nae kwa akili sana.
Nachoweza kusema na kwa experience yangu ndani ya ndoa miaka 8 sasa ni kwamba kadiri mnavyoongeza familia ndivyo na tabia za mkeo zinavyoanza kubadilika,(haijalishi ni understanding au non-understanding)hakuna siku atakutukana ila baadhi ya huduma ulizokuwa ukipewa zamani bila kuuliza itakubidi wewe mwenyewe uanze kujifanyia na wala usithubutu kuuliza omba uwe na hekima ya kujua mapema maana ya mabadiliko hayo lah hukujua utaitumbukiza ndoa kwenye vurugu,personally miaka ya mwanzo akinitengea maji ya kuoga,kuninyooshea nguo,kunipakulia chakula nikirudi home anapokea kama mkononi nina kimfuko au bag atakuja kupokea ila baada ya kupata mtoto wa kwanza hiyo ya kuwekewa maji ya kuoga na kuandaliwa nguo zilikufa nikabaki na favor mbili,kupokewa mzigo mwenyewe nilikataa nikaona kama utumwa sasa tuna watoto wawili hii ya kupakuliwa chakula muda wowote naona itakufa.
Obviously malalamiko mengi ya wanaume kwenye ndoa hutokana na huduma fulani kukatwa ghafla na majibu yasiyotegemewa kutoka kwa wake zao pale wanapouliza sababu,nilichogundua;anakuwa busy zaidi na watoto so hawezi kuacha kumlisha mtoto akakuandalie wewe maji ya kuoga,hawezi kuacha kumnyonyesha mtoto au kumuandaa mtoto awahi school bus akakunyooshee nguo also hawezi kuacha kumuogesha mtoto akakupakulie chakula mezani sasa ukiwa macho juu juu utataka kuhoji “inakuwaje zamani ukifanya hiki na hiki mbona sasa hivi hunifanyii” jibu utakalopewa hapo ndo litakaloamua hatma ya ndoa yenu,binafsi nachoshukuru niliweza ku-match na mabadiliko haya mapema na nachowashauri mnaotaka kuingia kwenye ndoa jueni mke siyo kwa ajili ya kukuhudumia wewe kwa kila kitu wanaopaswa kuhudumiwa kwa kila kitu na yeye wewe pia ukishiriki ni watoto wenu mtakaowazaa.
Well.....vurugu zipo na ieleweke tukubali au tukatae wanawake % kubwa wanafanana akili awe amesoma au hakusoma hakuna mwanamke anayekataa au anayekubali kosa kizembe,ni “kuishi nao kwa akili tu” ukiijua sentence hii na ukakubali ikuongoze kwenye arguments na mkeo ndoa utaiona tamu tofauti na hapo ni pigo.
Na mume bora nae anatoka wapi?Mke bora anatoka kwa Bwana..hahahaha, # 1
Mkeo ni kama mbilimbi 🤣🤣🤣 mchachu ila akipikwa mtamu.Mke wangu kundi la pili.
Hawezi kukiri kosa hata kama sababu zipo wazi kama kakosea. Kuomba msamaha sikumbuki ni mwaka gani na anachotaka yeye ukimshauri kinyume chake fahamu mada itabadilika na utaonekana mkosaji. Kususa na kuchukia jambo dogo tu ni kawaida saaana. Ila nikimwambia ntakuacha atalia huyo hadi umuonee huruma hahahaha.
Binafsi kuna baadhi ya mambo yupo sawa sana na huwa sioni taabu ya vitabia vyake.
Ila ndio vile nshamzoea na maisha yanasonga.
Hao namba 2 ubaya wao wengi ni impostors at first sight.Ukweli sijui kama kuna wanaume wapo wanaopenda hao kundi la pili? maana hao ni kipengele.
Wewe unatakiwa uishi na mimi,nitakubadilisha na kuwa kundi namba moja.Japo wameulizwa wanaume ila ngoja mimi nimuwakilishe wa kwangu.... nipo namba mbili