Mawazo yangu binafsi
Watu wanakejeli eti waliohudhulia huo mkesha ni wajinga na wanamtajirisha Mwamposa, lakini najaribu kuwaza, tatizo nikutoa kwa Mwamposa au nikwasababu wanatoa wengi? Maana hata wewe ambaye hujahudhulia, huko unakoabudu bado unatoa pesa, hata Kama uitafutie majina mazuri namna gani lakini bado unatoa pesa. Mwamposa amebarikiwa kuwa na Mvuto au kibali Cha watu, huenda wakati wake ukapita, lakini atabaki kwenye kumbukumbu za waamini Mungu kuwa, Mwamposa alikuwa na kibali. Mafundisho yake yapo OPEN Sana, anakuambia ukweli kabisa, kwamba, kuendesha kipindi Cha Tv LIVE kwenye station, ni gharama, anakuomba, Kama unaweza, changia elf 50, 20 au 10, lakini hakulazimishi Wala hakusimangi kwanini hujatoa. Wote wanaotoa, wanatoa kwa hiari yao. Na kusema ukweli tu, watu wanaotoa sadaka,popote, iwe msikitini, kanisani au kwa waganga ndiyo wanaofanikishwa zaidi, maskini ndiye mwenye tabia zakuona anaibiwa na bado hata hafanikiwi pamoja na ubahili wake.
Hayo ni maoni yangu binafsi