Mkidharauliwa na ndugu huwa mnachukua hatua gani?

Mkidharauliwa na ndugu huwa mnachukua hatua gani?

cold water

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2021
Posts
238
Reaction score
954
Morning wapendwa,

Hivi kwa mfano haujaanza maisha kutokana labda na kusoma upo nyumbani unasubiri matokeo yako ili uendelee kuangalia mikakati mingine ya kimaisha hapo nyumbani unaishi na ndugu na wadogo zako baada ya muda wadogo zako wanaanza kukudharau, mfano kuna dogo hapa home kaninunua mwezi wa tatu sasa bila sababu yeyote ile kuna mda anaimba nyimbo za mafumbo na kuziimbisha akijisikia.

Dogo anasoma chuo veta yupo likizo, iko chuo nilimtafutia mwenyewe, na kila akirudi likizo namchambulia nguo ambazo sizivai,yani ananinunia huku kakobeka nguo nilizompaga uko nyuma, na muangalia simmalizi dogo,nawaza nikipata kazi nimgawie zote zilizobaki Mimi nianze upya

Bado anasoma najua anaweza akabanwa na ratiba za kununua nguo,kama mnavyojua wazazi Mara nyingi wanakupa ada na ela ya kula, lakini Leo ananidharau, na ana kazi ya kuficha vitu Mara afiche sabuni Mara sukari Mara mboga, chakula kikibaki anakubali kumpa mtu wa baki lakini anajua Mimi bado sijala, ananiharibu kisaikolojia siku nikipata kazi nikimuoneshea roho ngumu atasema kaka hanisaidii au atasemaje kutokana na izi tabia anazonioneshea saizi.

Kuna mda najishusha namchukulia kama dogo kama kumpa nilichonacho, lakini bado anaendelea na ratiba zake zile zile za kujinunisha, nakaaga nawaza siku Mungu akinisaidia kupata ajira au kuwa na kipato chochote kitakacho niingizia ela nije nimsaidie ata mahitaji ya shule lakini naona ananitengenezea mazingira ya kumchukia na kutotaka kumsaidia huko mbeleni kutokana na kiburi na jeuri zake.

Kuna mda napata hasira nasema akijaribu kunijibu chochote namkata vibao, nimeamini usipokuwa na ela ata ndugu yako wa damu anakuchukia tu bila sababu, ungekuwa wewe ungefanyaje?
 
Morning wapendwa,iv kwa mfano haujaanza maisha kutokana labda na kusoma upo nyumbani unasubir matokeo yako ili uendelee kuangalia mikakati mingine ya kimaisha hapo nyumbani unaishi na ndugu na wadogo zako baada ya muda wadogo zako wanaanza kukudharau,mfano kuna dogo hapa home kaninunua mwezi wa tatu sasa bila sababu yeyote ile kuna mda anaimba nyimbo za mafumbo na kuziimbisha
Hivi kwa nini hampendani hapo kwenu? Vumilia ila kazana kutafuta ajira kwa maombi kwa Mungu.Usimchukie anayekununia.
 
Morning wapendwa,iv kwa mfano haujaanza maisha kutokana labda na kusoma upo nyumbani unasubir matokeo yako ili uendelee kuangalia mikakati mingine ya kimaisha hapo nyumbani unaishi na ndugu na wadogo zako baada ya muda
Usi endekeze ujinga mkuu, Dunia ya sasa sio ya kulea ujinga huyo chapa makofi au fukuza
 
Hiyo ni tuition anapewa na mkubwa hapo
Kama ni kweli,huyo mkubwa anayemfundisha huo ujinga anatengeneza bomu kubwa sana.Mlipuko wake wataupata pale ambapo watoto wataanza kujitegemea na familia zao.Hawatakuwa na mwisho mwema kwa sababu huyo mkubwa ameanza kubaini kuchukiwa kwa kosa la kukosa ajira ambazo hazipo.
 
Usi endekeze ujinga mkuu, Dunia ya sasa sio ya kulea ujinga huyo chapa makofi au fukuza
Huoni kwamba ataongeza tatizo hapo nyumbani kwao kwa kuonekana kachanganyikiwa kwa kukosa ajira?Na hana mamlaka ya kumfukuza mtu.Hapo ni kwao wote.Yaani ni kwa wazazi/ndugu.Aishi hapo nyumbani kwa akili nyingi na utulivu.
 
Morning wapendwa,

Hivi kwa mfano haujaanza maisha kutokana labda na kusoma upo nyumbani unasubiri matokeo yako ili uendelee kuangalia mikakati mingine ya kimaisha hapo nyumbani unaishi na ndugu na wadogo zako baada ya muda wadogo zako wanaanza kukudharau, mfano kuna dogo hapa home kaninunua mwezi wa tatu sasa bila sababu yeyote ile kuna mda anaimba nyimbo za mafumbo na kuziimbisha akijisikia.

Dogo anasoma chuo veta yupo likizo, iko chuo nilimtafutia mwenyewe, lakini Leo ananidharau, na ana kazi ya kuficha vitu Mara afiche sabuni Mara sukari Mara mboga, chakula kikibaki anakubali kumpa mtu wa baki lakini anajua Mimi bado sijala, ananiharibu kisaikolojia siku nikipata kazi nikimuoneshea roho ngumu atasema kaka hanisaidii au atasemaje kutokana na izi tabia anazonioneshea saizi.

Na mda najishusha namchukulia kama dogo kama kumpa nilichonacho, lakini bado anaendelea na ratiba zake zile zile za kujinunisha, nakaaga nawaza siku Mungu akinisaidia kupata ajira au kuwa na kipato chochote kitakacho niingizia ela nije nimsaidie ata mahitaji ya shule lakini naona ananitengenezea mazingira ya kumchukia na kutotaka kumsaidia huko mbeleni kutokana na kiburi na jeuri zake.

Kuna mda napata hasira nasema akijaribu kunijibu chochote namkata vibao ungekuwa wewe ungefanyaje.
Amini usiamini huyo dogo atatusua maisha kuliko wewe haijalishi umemtafutia nafasi ya masomo huko veta lakini atakuja kujiona mjanja na atasahau kuwa wewe ndo umemtengenezea hayo mazingira. Nahisi wewe utakuwa mtoto wa kwanza kwenye hiyo familia pambana kivyako sisi watoto wa kwanza ni daraja la kuwavusha wenzetu wakishavuka wanatuacha tunachakaa. Pambana na maisha yako wasaidie ndugu zako na usitamani urudishiwe fadhila hata siku moja nafanya hivyo na ndio maana nikajiita kakamkubwa
 
Ashike lipi?Aishi kwa imani kwamba mdogo wake atayapatia maisha kwa sababu yeye ni mkubwa au azidishe juhudi ya kutafuta kipato na akajitegemee?
 
Hayo mbona ni ya kawaida sana kwenye Jamii.

Kikubwa ni kumuomba Mungu akupe subra, na pale utakapofanikiwa kamwe wala usiwaze kulipiza kisasi bali ndio iwe nafasi ya kumuonesha inavyopaswa kuwa...Mungu hutoa thawabu kwa yaliyo mema tu na sio visasi au uhasama.
 
Kama hukuumbwa na roho mbaya huwezi ukawa na roho mbaya. Mpotezee tu. Ukimmind shetani atakuzibia kila njia
 
Back
Top Bottom