Mkoa wa Iringa utolewe Nyanda za Juu Kusini na kupelekwa Kanda ya Kati iwe Pamoja na Dodoma na Singida

Mkoa wa Iringa utolewe Nyanda za Juu Kusini na kupelekwa Kanda ya Kati iwe Pamoja na Dodoma na Singida

Hasara wanayopata wana Iringa kuwa nyanda za juu kusini ni ipi?
Faida watakayopata wana Iringa wakihamia kanda ya Kati ni ipi?
 
Kwani unavyotoka Iringa au Morogoro kuitafuta Dodoma unashuka au unapanda?
Kutoka iringa kwenda Dom unakuwa unashuka mpaka unaikuta mtera dam, ndio level moja mpaka Dom

Moro to Dom ni normal tu...zote with almost the same height from sea level.

Iringa ipo mwinukoni mno,ukitoa kipande cha daraja la ruaha to unapoianza kitonga.
 
Kama issue ni Milima basi Morogoro au Kilimanjaro au Arusha zote zingekuwa Nyanda za Juu..

Nakwambia Muingiliano wa Kijamii ni mkubwa Dom kuliko Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini..

Watu wa Iringa vipi mnakataa ndugu zenu? Nendeni Dom huko
Kilimanjaro na Arusha zinaweza kuwa nyanda za juu,ila sio za juu "kusini".

Hapa tunaongelea nyanda za juu kusini
 
Kilimanjaro na Arusha zinaweza kuwa nyanda za juu,ila sio za juu "kusini".

Hapa tunaongelea nyanda za juu kusini
Sasa kama ni ishu ya kuin,Iringa haipo Kusini bali central ,kwani hujaona ramani?
 
Namba 3 naipinga
Kwa hiyo Iringa sio Semi Arid si ndio? Kwamba apart from Mafinga kwingine huko kumejaa ukame ndio maana mumejenga vijumba vya udongo everywhere kama Dom tuu..
 
By the way Iringa ni Mkoa pekee maalumu wenye ambao Mkoa wote una kabila mmoja tu-Wahehe tofauti na Mikoa mingine ambapo unakuta kuna mchanganyiko wa makabila mengi.
 
Mikoa 26 ya Tanzania Bara imegawanywa kwenye Kanda 7 za Kiutawala.

Mkoa wa Iringa Kwa Sasa uko Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.

Ingefaa Kwa Serikali kuiondoa Iringa Nyanda za Juu Kusini na kuihamishia Kanda ya Kati Kwa sababu zifuatazo

1.Sababu za Kijiografia.

Mkoa wa Iringa u ko jirani na Dodoma Makao Makuu ya Nchi na Kanda ya Kati kuliko Mbeya(Makao Makuu ya Nyanda za Juu Kusini).
Kutoka Iringa Hadi Dodoma ni km 260 vs Iringa Mbeya km 350.As we speak Iringa na Dodoma Ina Muingiliano mkubwa wa Watu via usafiri kuliko Iringa na Mbeya,so ni sahihi Kwa Iringa kuwa included Central Zone.

2.Sababu za Kijamii(Muingiliano wa Kikabila)

Kabila la Wagogo ambao ndio kabila kuu la Mkoa wa Dodoma pia linapatikana Kwa Baadhi ya maeneo ya Iringa hasa Wilaya ya Iringa hivyo Muingiliano wa Kijamii na Kitamaduni ni mkubwa baina ya Iringa na Dodoma kuliko Iringa na Mbeya..Aidha Kabila la Wahehe pia wapo Dodoma..

3.Sababu za Kimazingira.

Iringa Ina Haki ya hewa ya semi -Arid (Nusu jangwa) sawa sawa kabisa na hali ya Dodoma au Kanda ya Kati kiukumla.
Ukitoa Wilaya ya Mufindi na Baadhi ya maeneo ya Kilolo ,Iringa yote ni Semi Arid..

4.Sababu ya Kiuchumi/Biashara na Kijamii.

Mkoa wa Iringa unategemea Huduma zake nyingi kutoka Dodoma na Dar lakini sio Mbeya kutokana na kuwa jirani na Dodoma..

Sasa Kwa sababu hizo ni Wazi Iringa inafaa iwe Kanda ya Kati badala ya kuwa Nyanda za Juu.

Kwenye Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ni Iringa Pekee ambako unaweza Kuta nyumba za udongo na nyasi ambazo zinapatikana Kwa wingi Dodoma,Singida na maeneo ya Kanda ya Ziwa na Pwani huko..View attachment 2657397
Itasaidia nini labda iwekwe kati ya Emirates za Arab tena iwe imeungana na Dubai
 
Ruti za Mbeya Iringa ni nyingi mara 4 ya Dodoma Iringa
 
Back
Top Bottom