Mkoa wa Iringa utolewe Nyanda za Juu Kusini na kupelekwa Kanda ya Kati iwe Pamoja na Dodoma na Singida

Mkoa wa Iringa utolewe Nyanda za Juu Kusini na kupelekwa Kanda ya Kati iwe Pamoja na Dodoma na Singida

Tafuta kwanini eneo lile la Iringa,Ruvuma,Mbeya pamoja na Rukwa iliitwa nyanya za juu kusini.
 
Binafsi huwa naona kosa kubwa lililofanyika ni kuitenga Iringa na njombe tu!
Bora wangehamisha ofisi ya mkuu wa mkoa ikae eneo lenye uwiano!

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
zamani ilikuwa sahihi kwasababu wilaya ya ludewa, njombe na makete ambazo zote zipo mkoa wa njombe, zimesambaa hadi kusini na upande mwingine kuungana na mbeya. lkn sasaivi, iringa inaishia tu pale mafinga kurudi nyuma. ukiondoa Kilolo (dabaga) iringa ni kavu kama singida na dodoma tu. sio mbaya kama wataiondoa kusini. pamoja na kwamba utakuwa umewatenga sana na watumwa wao (wabena, wakinda na wapangwa). kihistoria, wabena, wakinga na wapanga hawana historia ya kutawala, wao walikuwa subordinates tu wa Mkwawa hadi usangu huko. na wameendelea kujifanya wahehe hadi kesho kwasababu kwao kuitwa mhehe ndio anatambulika zaidi kuliko akijiita mbena au mkinga.
Iringa haiishii mafinga! Labda ungesema nyigo mpakani

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Hii Kanda Ya ziwa ndo ili kaa kimkakati zaidi waliweka eneo sahihi la makao makuu ya Kanda nyanda za juu kusini bado Kuna shida ndo maana Kuna baadhi ya huduma mikoa imeanza kujitenga mfano msd imeweka Kanda ya iringa Ina hudumia iringa na njombe pia Kuna Kanda ya mbeya inahudumia mbeya na songwe bado ishu ya maonyesho ya nane nane mkoa WA ruvuma una UNGANA na mikoa ya kusini ya Lindi na Mtwara bado kusiuply material mikoa ya iringa ,ruvuma, njombe bidhaa nyingi wanategemea dsm
FB_IMG_16769576241954978.jpg
 
Basi morogoro na nayo iwe kanda ya kati muingiliano
Na ukaribu vipo karibu pia tabora manake ipo jirani sana na singida

Viwe kanda ya kati tabora ikashakuwa kanda ya kati katavi pia manake katavi na tabora muingiliano mkubwa sana

Na iringa ikiwa kanda ya kati njombe msiache


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilivoona baadhi ya maeneo ya dodoma yana wahehe ni sawa kabisa iringa iende kanda ya kati ili kubalance kanda ile iwe na mikoa mitatu, kiutawala itakaa vizuri zaidi ili nyanda za juu kusini iwe na mikoa mitatu pia yaani njombe, mbeya na ruvuma
Na maneo ya njombe pia yana wahehe sana vipi iwe ka da ya kati?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kanda ziligawanywa kwa kigezo kikubwa cha mfano wa wa kimazingira baina ya mikoa

Sifa ya singida na dodoma kimazingira zipo sawa kwa zaid ya 90%


Kanda ya pwani kadhalika
Kimazingira zinafanana kwa kiasi kikubwa

Juu kusini na zing8nezo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We ngumbaru una shida Kwa kweli.

Makao Makuu yapo ndio maana Huwa unasikia Hospital za Kanda,Ofisi za Kanda za Huduma Fulani nk ila sio rasmi kwamba Kuna Mkuu wa Kanda wa Serikali hapana ila Meneja wa Kanda wa banks, kampuni nk wapo.
Bank wao wanaweza ku operate kikanda bila kufata mpangilio wa Kiserikali, Wao wanaangali urahisi wa Ku operate wanaweza kugawa Zones kwa Kuamua wao wenyewe
 
Hii inaonyesha nyanda za juu kusini jinsi inavo wiana kwa vitu vingi mambo ya ardhi nk na wamejumuisha na sehemu ya morogoro ambayo ni ifakara mbeleni huko nao utakuwa mkoa note msitu wa Sao hill umeenda hadi wilaya ya mlimba moro
The-Southern-Highlands-of-Tanzania-illustrating-the-mixed-land-use-occurring-in-this(0).jpg

47-Figure1-1(1).jpg
 
Bank wao wanaweza ku operate kikanda bila kufata mpangilio wa Kiserikali, Wao wanaangali urahisi wa Ku operate wanaweza kugawa Zones kwa Kuamua wao wenyewe
Sasa Kwa taarifa wengi wao wanafuata
 
Ni kweli kabisa una point, na huu muingiliano ulipaswa uwe wa muda mrefu sana ila ubovu wa barabara ya Iringa - Dodoma ilichangia kipindi hiko kwenda Dodoma mpaka upitie morogoro vinginevyo jiandae kula vumbi tofauti na sasa, wengi wanatokea mkoa mmoja kwenda mwingine kutafuta maisha
 
Rukwa ni Nyanda za Juu Kusini pure maana inafanana mazingira,utamaduni na aina za shughuli za kiuchumi na Nyanda za Juu Kusini.

Mfano upande wa Magharibi ni Mikoa ya joto kuanzia Tabora,Kigoma na Katavi wakati Rukwa ni Mkoa wa Baridi sababu ya Milima.

Makao Makuu ya Kanda ya Magharibi Yako Kigoma,huo umbali wa km 600 nani anataka wakati Kwenda Mbeya ni km 330 tuu..

Mwisho ukiacha Arusha-moshi,Mbeya-Tunduma na Morogoro -Dar ,hakuna Mkoa mwingine una route nyingi za Mabasi kushinda Mbeya -Sumbawanga tena panda zote Huku Juu ufipani na kule chini Bonde la Ziwa Rukwa..
Ouk sawa.
 
Back
Top Bottom