Si ndio hapo mkuu, nilisha wambia watu hapa kwamba China iliwahi kupigana vita na Merikani ana kwa ana na matokeo hayakuwa mazuri kwa upande wa jeshi la Amerika lilivurumishwa vikali mpaka likarudishwa nyuma - mwanzo US ilidharau jeshi la China lakini walipo pambana ana kwa ana walipata kisago cha nguvu hawakurudia tena kudharau jeshi la China - kiongozi wa jeshi la Merikani aliadhilika katika operation hiyo kwa aibu kaomba idhini ya Rais wa Merikani wa wakati huo Harry Truman ili amuruhusu kutumia mabom ya Nuclear dhidi ya China lakini Truman alimkatalia mpaka wakafikia hatua ya kufarakana, akatimuliwa kazi unceremoniously. That was almost 70 years ago, je,
hivi sasa jeshi la China limekwisha piga hatua gani in terms of science na teknolojia kwenye medani za uundaji wa silaha za kisasa kabisa na space exploration - Wachina si wanadamu wa kuchukulia poa hata kidogo.