Yes siku zote, dawa ya deni ni kulipa, kwa vile Madaraka Nyerere ni mtoto wa Mwalimu Nyerere, na Mwalimu alichukia rushwa, hivyo it is expected Madaraka hawezi kutoa rushwa yoyote.
Kilichotokea ambacho Madaraka hakukisema, ni baada ya kujaza fomu kuomba ubunge, mmoja wa wajumbe akamfuata na kumweleza ukweli wa mambo kuwa bila kunyoosha mkono, kutoa kidogo dogo, huwezi kupita, hivyo Madaraka akauliza kama kiasi gani kwa mjumbe, jamaa akamjibu 50,000. Madaraka akakubali na kumpa 50,000 ili ateuliwe, ila akamwambia, usipoteuliwa nitakurudishia.
Kitu ambacho Madaraka hakujua, ni hiyo 50,000 ni kwa kila mjumbe!. Yeye katoa kwa mtu mmoja tuu!. Matokeo yake ni moja ya zile kura mbili ndio 50,000 yake!. Hiki ni kiendacho kwa mganga!.
Madaraka hakutakiwa hata kulisemea hili!.
Jimbo la Kawe kuna watu wametoa hadi 500,000 kwa kila mjumbe!. Wajumbe wako 400!.
Kuna mtu namfahamu, katoa TZS 10,000,000 kila kata, Kawe ina kata 10, kaambulia kura 1!. Alipouliza vipi, akaambia wewe unatoa kwenye kata, wenzio wanawawekea watu mifukoni!.
Yaani Madaraka ni mtu wa kuilizia hiyo 50,000 wakati ndio kiwango cha short time mitaa fulani!.
P