Mkopo alioutoa Madaraka Nyerere wamuhamisha mtu nchi

Mkopo alioutoa Madaraka Nyerere wamuhamisha mtu nchi

Yes siku zote, dawa ya deni ni kulipa, kwa vile Madaraka Nyerere ni mtoto wa Mwalimu Nyerere, na Mwalimu alichukia rushwa, hivyo it is expected Madaraka hawezi kutoa rushwa yoyote.

Kilichotokea ambacho Madaraka hakukisema, ni baada ya kujaza fomu kuomba ubunge, mmoja wa wajumbe akamfuata na kumweleza ukweli wa mambo kuwa bila kunyoosha mkono, kutoa kidogo dogo, huwezi kupita, hivyo Madaraka akauliza kama kiasi gani kwa mjumbe, jamaa akamjibu 50,000. Madaraka akakubali na kumpa 50,000 ili ateuliwe, ila akamwambia, usipoteuliwa nitakurudishia.

Kitu ambacho Madaraka hakujua, ni hiyo 50,000 ni kwa kila mjumbe!. Yeye katoa kwa mtu mmoja tuu!. Matokeo yake ni moja ya zile kura mbili ndio 50,000 yake!. Hiki ni kiendacho kwa mganga!.
Madaraka hakutakiwa hata kulisemea hili!.

Jimbo la Kawe kuna watu wametoa hadi 500,000 kwa kila mjumbe!. Wajumbe wako 400!.
Kuna mtu namfahamu, katoa TZS 10,000,000 kila kata, Kawe ina kata 10, kaambulia kura 1!. Alipouliza vipi, akaambia wewe unatoa kwenye kata, wenzio wanawawekea watu mifukoni!.
Yaani Madaraka ni mtu wa kuilizia hiyo 50,000 wakati ndio kiwango cha short time mitaa fulani!.
P
Madaraka boya sana
 
IMG-20220130-WA0000.jpg
 
Ulitaka usikie madaraka Nyerere ni waziri wa fedha au ulinzi ndio ufurahi?
Nyerere angetata iwe hivyo ingewezekana na asingekuwepo wa kuhoji.
Mu7 mwanae ni Lt. General, mkuu wa jeshi la ardhini.
Labda ingekuwa hivyo na kwa Nyerere ndo wengine wangeridhika.
 
Jimbo la Kawe kuna watu wametoa hadi 500,000 kwa kila mjumbe!. Wajumbe wako 400!.
Kuna mtu namfahamu, katoa TZS 10,000,000 kila kata, Kawe ina kata 10, kaambulia kura 1!. Alipouliza vipi, akaambia wewe unatoa kwenye kata, wenzio wanawawekea watu mifukoni!.
Yaani Madaraka ni mtu wa kuilizia hiyo 50,000 wakati ndio kiwango cha short time mitaa fulani!.
Teh teh teh teh 😂😂😂😂 haya maneno yamenifurahisha sana haaaa 😂😂😂😂....maana huyo mtu ninamfahamu.....

Ila siasa ni biashara inayolipa vizuri ila inahitaji uwekezaji mkubwa sana, mpaka mtu atoe 500,000 kwa watu 400?....

Ila najiulize huyo aliteoa million 100 hakuona hata uelekeo wa upepo kabla ya kuchezea pesa yake?
 
Back
Top Bottom