Mkristo kufunga mwezi wa Ramadhan haikubaliwi ni mpaka aukubali uislamu kwanza: Uliza swali lolote kuhusu Ramadhan nitakujibu

Ikiwa unawapa pesa kwa mnasaba wa ngono pesa hiyo ni haramu, lakini ikiwa unawapa kwa mnasaba wa kibinaadamu hakuna tatizo.
 
Shekh wanawake walio wengi hapa jijini Dar hawajaolewa na wanahudumiwa na wanaume ambao sio wa ndoa kwa hiyo unapo sema pesa wanayopokea ni ya halamu basi wengi wanasindikiza mwezi tu
 
Mkuu umesoma andiko vizuri lakini
Mussa aliambiwa amlinganie firauni kwa upole

Mtume tabia zake pekee tu bila kusema chochote kuhusu dini zilitosha kuwafanya wengine wakaingia katika uislamu

Wewe unaanza thread kwa kuwakebehi wakristo waliufunga na kuweka picha makusudi, kilichokuudhi na hao wakristo kujumika na uislamu.

wewe si aina ya watu ya kuwavutia watu katika uislamu hata kuliangania huwezi kwa sababu una jazba, hauna subra, hekma, busara, utulivu
 
kwanini mnakula asubuhi kabla ya kudanganya watu kuwa mmefunga
Wakati wa kula daku ni baina ya usiku wa manane na alfajiri. Inakuwa ni vizuri zaidi kuichelewesha (yaani, karibu zaidi ya alfajiri kwa kadri inavyowezekana). Daku ni mlo uliobarikiwa, hivyo usiupuuze japo kwa fundo la maji,
 
Katika kuwasilisha hoja yako mleta mada wakati unamtaja mtume uliweka maneno yaliyo fungwa ya Rehema na amani ziwe nae.

Swali langu la kwanza ni kwamba pomoja na kazi zote za mtume kueneza uislamu, kule kuwe kwake karibu na Mungu na malaika wa Mungu ni kwamba hapo alipo kwa sasa hana amani?

Kwamba hakujaliwa kupata Rehema kutoka kwa Mungu moja kwa moja mpaka aombewe Rehema na amani kutoka kwa wafuasi wake?

Kama mtume amepungukiwa na Rehema na amani hali yeye ni mkuu kuliko mja yeyote, kuliko nabii na mtume mwingine yoyote, vipi kwa sisi ambao tunatakiwa kumuamini tuta pata Rehema kweli na amani?
 
Mussa aliambiwa amlinganie firauni kwa upole

Mtume tabia zake pekee tu bila kusema chochote kuhusu dini zilitosha kuwafanya wengine wakaingia katika uislamu....
Ahsante, picha hiyo imeshaondolewa, lakini haikua na maana yoyote katika kuudhi ukristo wala kukebehi. Samahani sana kwa hilo, na pole sana kwa kukuumiza kihisia. Natanguliza msamaha juu ya hilo.
 
Katika kuwasilisha hoja yako mleta mada wakati unamtaja mtume uliweka maneno yaliyo fungwa ya Rehema na amani ziwe nae...
Tunaamini kuwa kila anapotajwa Mtume ni lazima tuitikie swalallahu alayhi wa aalihi wa salam (s.a.w.w).
Hii inatokana na agizo la MUNGU pale ambapo yeye mwenyewe anatangaza wazi kuwa humtakia rehema Mtume, pale aliposema;

“Hakika Allah na Malaika wake wanamtakia Rehema Mtume. Enyi ambao mmeamini mtakieni rehema juu yake na Msalimuni kwa (uzuri) wa Salamu.” (33:56).

Kumrehemu Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni miongoni mwa ibada bora na tukufu ambazo kwayo mtu anaweza kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu Mtukufu amefaradhisha hayo kwa waja wake walioamini.
 
Ahsante, picha hiyo imeshaondolewa, lakini haikua na maana yoyote katika kuudhi ukristo wala kukebehi. Samahani sana kwa hilo, na pole sana kwa kukuumiza kihisia. Natanguliza msamaha juu ya hilo.
Kila kitu binadamu tunafanya kwa nia, kuanzia ulivyoiona ile picha ukachukia ndio ikawa kusudio lako kuiweka wewe ukitamani hiyo mkristo hapo kwenye futari asiwepo.

Mimis sijaumizwa bali nimechukizwa na hiyo tabia yako

Kwanini huangalii ukajifunza maisha yote ya mtume, maisha yake yote ni kiigizo. Usibaki kwenye Fiqh, Seera, Quraan, Tawheed tu. Hata alivyoishi na watu pia na jamii. upole, busara, hekima na akhlaaq zingine

Nimemaliza nakutakia usiku mwema
 
Kila kitu binadamu tunafanya kwa nia, kuanzia ulivyoiona ile picha ukachukia ndio ikawa kusudio lako kuiweka wewe ukitamani hiyo mkristo hapo kwenye futari asiwepo...
Barikiwa sana, nimepokea nasaha na mashauri yako katika kujenga. Muwe na usiku mwema hapo nyumbani.
 
Bahati nzuri ni kwamba sijawahi kujua mwandamo wa mwezi unakuwa vip so siwezi kujua ramadhan inaanza ama kuisha lini.
 
Dini zilitakiwa kutuleta pamoja lakini baadhi yetu wamewekeza nguvu nyingi kuzitumia kututenganisha.

Wasio na dini wana upendo wa kweli sana. Hawabagui huyu mkristo sijui huyu muislamu wote kwao ni Binadamu.
 
Ovyo sanaaa

Matika jamboa la kushangaza sasa iko ivi gangia miaka yote .. kwaresma huwa haibadiliki wa kristu kila mwaka ifikapo mwanzo mwa mwezi wa 3 huanza kipindi cha kwaresma ambapo huadhimisha mateso ya yesu kristo

Ila iyo ramadhani sasa ndio haipo stable mara itaanza mwezi wa 4 mara mweziwa 3 mara may, yaam ni mpaka . Mwezi uje uonekane
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…