Yaani wewe Uuwe, Uibe, Uzini na mengineyo, halafu aje umbebeshe zambi zako Yesu ambaye hata kuiba au kuuwa na kuzini hajawi? inaingia akilini kweli? tena auwawe kwa mateso makubwa, Haiwezekani hata kidogo
Mungu wa Ibrahimu aliongea na Nabii Danieli na kumpa majuma 70 ambapo Kati ya majuma hayo , juma la 62 Masihi atakatiliwa mbali na watu wake( Masihi atauwawa), kimaandiko Mungu alimoa Danieli miaka 490 tokea Mfalme Cyrus atangaze ujenzi wa Hekalu na kurudi Kwa Wayahudi kama ilivoandikwa:
Danieli 9:24-27
[24]Muda wa majuma sabini umeamriwa juu ya watu wako, na juu ya mji wako mtakatifu, ili kukomesha makosa, na kuishiliza dhambi, na kufanya upatanisho kwa ajili ya uovu, na kuleta haki ya milele, na kutia muhuri maono na unabii, na kumtia mafuta yeye aliye mtakatifu.
Seventy weeks are determined upon thy people and upon thy holy city, to finish the transgression, and to make an end of sins, and to make reconciliation for iniquity, and to bring in everlasting righteousness, and to seal up the vision and prophecy, and to anoint the most Holy.
[25]Basi ujue na kufahamu, ya kuwa tangu kuwekwa amri ya kutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu hata zamani zake masihi aliye mkuu; kutakuwa na majuma saba; na katika majuma sitini na mawili utajengwa tena pamoja na njia kuu zake na handaki, naam, katika nyakati za taabu.
Know therefore and understand, that from the going forth of the commandment to restore and to build Jerusalem unto the Messiah the Prince shall be seven weeks, and threescore and two weeks: the street shall be built again, and the wall, even in troublous times.
[26]Na baada ya yale majuma sitini na mawili, masihi atakatiliwa mbali, naye atakuwa hana kitu; na watu wa mkuu atakayekuja watauangamiza mji, na patakatifu; na mwisho wake utakuwa pamoja na gharika, na hata mwisho ule vita vitakuwapo; ukiwa umekwisha kukusudiwa.
And after threescore and two weeks shall Messiah be cut off, but not for himself: and the people of the prince that shall come shall destroy the city and the sanctuary; and the end thereof shall be with a flood, and unto the end of the war desolations are determined.
[27]Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu; na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu.
And he shall confirm the covenant with many for one week: and in the midst of the week he shall cause the sacrifice and the oblation to cease, and for the overspreading of abominations he shall make it desolate, even until the consummation, and that determined shall be poured upon the desolate.
Hivyo tokea mwaka ambapo Mfalme Cyrus wa Persia aanze kujenga mpaka Masihi aliyechaguliwa na Mungu auwawe ilikuwa miaka 434 na hivyo ilipaswa mwaka wa 33 A.D mwezi wa kwanza wa Kiyahudi ya Nisani, Masihi awe ameuwawa kadiri ya Malaika Gabrieli alivomwambia Nabii Danieli, na tarehe 14 mwezi wa Nisani mwaka wa 33 A.D Yesu Kristo kwa amri ya Pilato aliuwawa pale msalabani Kalvari( kama ilivoelezwa na wanahistoria Yosefus Flavius na Tacitus) na kutimiza unabii ambao Malaika Gabriel alimpa Danieli miaka mingi iliyopita.
Na unabii wa Danieli unaendelea kusema baada ya kufa kwa Masihi huyu, miaka ya baadaye Mfalme mmoja atakuja kuharibu Hekalu Takatifu na mji wa Wayahudi na hilo lilitimia kwa Tito Mrumi ambaye baadaye alikuwa Mfalme wa Dola Kuu ya Rumi kuharibu Hekalu Takatifu mwaka wa 70 hivi.
Hivyo kadiri ya Maandiko ilikuwa lazima mtu atakayebeba majukumu ya Masihi afe na hilo alilitimiza Yesu Kristo kwa kufa tarehe, siku na mwaka sahihi kama ilivotabiriwa.
Na Nabii Isaya alitabiri haya kuhusu Masihi huyu:
Isaya 53:2-12
[2]Maana alikua mbele zake kama mche mwororo,
Na kama mzizi katika nchi kavu;
Yeye hana umbo wala uzuri;
Na tumwonapo hana uzuri hata tumtamani.
For he shall grow up before him as a tender plant, and as a root out of a dry ground: he hath no form nor comeliness; and when we shall see him, there is no beauty that we should desire him.
[3]Alidharauliwa na kukataliwa na watu;
Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko;
Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao,
Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu.
He is despised and rejected of men; a man of sorrows, and acquainted with grief: and we hid as it were our faces from him; he was despised, and we esteemed him not.
[4]Hakika ameyachukua masikitiko yetu,
Amejitwika huzuni zetu;
Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa,
Amepigwa na Mungu, na kuteswa.
Surely he hath borne our griefs, and carried our sorrows: yet we did esteem him stricken, smitten of God, and afflicted.
[5]Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu,
Alichubuliwa kwa maovu yetu;
Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake,
Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.
But he was wounded for our transgressions, he was bruised for our iniquities: the chastisement of our peace was upon him; and with his stripes we are healed.
[6]Sisi sote kama kondoo tumepotea;
Kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe;
Na BWANA ameweka juu yake
Maovu yetu sisi sote.
All we like sheep have gone astray; we have turned every one to his own way; and the LORD hath laid on him the iniquity of us all.
[7]Alionewa, lakini alinyenyekea,
Wala hakufunua kinywa chake;
Kama mwana-kondoo apelekwaye machinjoni,
Na kama vile kondoo anyamazavyo
Mbele yao wakatao manyoya yake;
Naam, hakufunua kinywa chake.
He was oppressed, and he was afflicted, yet he opened not his mouth: he is brought as a lamb to the slaughter, and as a sheep before her shearers is dumb, so he openeth not his mouth.
[8]Kwa kuonewa na kuhukumiwa aliondolewa;
Na maisha yake ni nani atakayeisimulia?
Maana amekatiliwa mbali na nchi ya walio hai;
Alipigwa kwa sababu ya makosa ya watu wangu.
He was taken from prison and from judgment: and who shall declare his generation? for he was cut off out of the land of the living: for the transgression of my people was he stricken.
[9]Wakamfanyia kaburi pamoja na wabaya;
Na pamoja na matajiri katika kufa kwake;
Ingawa hakutenda jeuri,
Wala hapakuwa na hila kinywani mwake.
And he made his grave with the wicked, and with the rich in his death; because he had done no violence, neither was any deceit in his mouth.
[10]Lakini BWANA aliridhika kumchubua;
Amemhuzunisha;
Utakapofanya nafsi yake kuwa dhabihu kwa dhambi,
Ataona uzao wake, ataishi siku nyingi,
Na mapenzi ya BWANA yatafanikiwa mkononi mwake;
Yet it pleased the LORD to bruise him; he hath put him to grief: when thou shalt make his soul an offering for sin, he shall see his seed, he shall prolong his days, and the pleasure of the LORD shall prosper in his hand.
[11]Ataona mazao ya taabu ya nafsi yake, na kuridhika.
Kwa maarifa yake mtumishi wangu mwenye haki
Atawafanya wengi kuwa wenye haki;
Naye atayachukua maovu yao.
He shall see of the travail of his soul, and shall be satisfied: by his knowledge shall my righteous servant justify many; for he shall bear their iniquities.
[12]Kwa hiyo nitamgawia sehemu pamoja na wakuu,
Naye atagawanya nyara pamoja nao walio hodari;
Kwa sababu alimwaga nafsi yake hata kufa,
Akahesabiwa pamoja na hao wakosao.
Walakini alichukua dhambi za watu wengi,
Na kuwaombea wakosaji.
Therefore will I divide him a portion with the great, and he shall divide the spoil with the strong; because he hath poured out his soul unto death: and he was numbered with the transgressors; and he bare the sin of many, and made intercession for the transgressors.
Na Mfalme Daudi aliandika Zaburi kuhusu huyu Masihi ya kuwa atafufuliwa na Mungu wa Ibrahimu, mwili wa Yesu Kristo haukuharibika na Mitume waliokuwa wamemuona na watu karibia 500 ni mashahidi, Daudi alisema hivi
Zaburi 16:10
[10]Maana hutakuachia kuzimu nafsi yangu,
Wala hutamtoa mtakatifu wako aone uharibifu.
For thou wilt not leave my soul in hell; neither wilt thou suffer thine Holy One to see corruption.
Hivyo Yesu Kristo alitimiza yote aliyoandikiwa kuhusu Yeye na Mungu amempa heshima kubwa ya kwamba yeyote atakayemuamini atahesabiwa Haki kwa Imani katika Yesu Kristo.