Nilifika shule mmoja mi na mwenzangu kuanza kazi ya kufundisha, tulikuta wenyeji wetu wakatupokea tukawa tunaachiana zamu kupika wawili wawili. Mchana tukawa tunapikiwa na wanafunzi wa kike wakubwa wawili. Walimu wawili walihama kambi tukabaki wawili na utaratibu wetu wa kupikiwa mchana na kuchotewa maji. Mwisho nilibaki mwenyewe nikaona isije kuwa balaa nikaachana na utaratibu wa kuhudumiwa na wanafunzi tena wanafunzi wenyewe wa kike wamekamilika kila idara miilini mwao. Pamoja na ku sense danger na kuachana kuwatumia wanafunzi lilipangwa jaribio la kunipakazia kuwa nawachakata wanafunzi hao, hao hao wanafunzi wakipangwa watoe ushaidi mbele ya school baraza. Ilikuwa nipakaziwe kashfa ya kulabua wanafunzi ila kashfa hiyo ilipanguliwa kwa nguvu zote na wanafunzi wenzao walioona nafanyiwa njama kwa chuki tu toka kwa walimu wenzangu niliowazidi kufundisha kwa weledi mpaka wanafunzi wakanipenda ikawa wivu