KERO Mkurugenzi Garda World jitafakari, wafanyakazi tumekuchoka

KERO Mkurugenzi Garda World jitafakari, wafanyakazi tumekuchoka

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Unanikumbusha zenji nimeka zangu lindo kisiwani kaja boti man wa kisiwa na boti kaipaki nje. Kuja ndani tunapiga hesabu za mafuta ndani ya dakika 15 tu, kutoka nje boti haipo 😂
Kazi ya Ulinzi ni ya Kiboya sana yaani kwanza Walinzi wanaonekana wana afya mgogoro na njaa kibao yaani kama sio mtu wa kujiongeza mtaani huko kwenye lindo utakuwa fala sana.
 
WANA madudu mengi sana eti wenyewe wanakwambia mlinzi hapaswi kupata overtime ya night allowance wao wanamchukulia mlinzi kama mtu ambae ni lazima afanye kazi usi tena bila kulipwa night allowance hii mijamaa ina madudu mengi ambayo ukiandika hapa jamii haito elewa ila kwa kifupi...kampuni bora inayo zingatia maslahi ya wafanya kazi ni WS Insight pekee kwa Tanzania
Kweli? Enh sasa hapo WS insight nafanyaje mkuu nizamepo
 
Mshahara mdogo lakin wanakula bange na gongo vibaya sana. Miksa stress hujui kesho yako.. ulinzi sio kaz walahi
Mkuu Mimi nilienda kuomba nafasi ya control room ndio nikatupwa lindo kwanza lakini nilikuwa na ishu zingine kabisa lengo la.kwenda kuomba pale niwe na uhakika wa kipato niombe mkopo sehemu. Lakini sasa ndio.nilikuja kugundua Ulinzi kwenye Kampuni za Kitanzania ni Upuuzi mtupu. Ma Supervisor nilikuwa nazinguana nao sana mpaka Zone Manager alishawahi kuniletea itikadi za kingese nilichomfanyia aisee hakuamini mpaka akajua Mimi ni Geti jeusi 🤣🤣🤣
 
Miungu watu kwenye maofisi ni wengi Sanaa
Kuna NGO moja iko Moshi jamani Yule boss ni kizunguzungu anapenda kuabudiwaaa anapelekesha watu kama kawazaa ye ye. Hataki mfanyakazi aambaye yuko na akili huru

Mwanamke wake ambaye hata elimu yake haieleweki ndo anampandisha cheo daily wakati kwenye ukaguzi wa wafanyakazi yule demu ndo anafanya vibaya Sana.

Mwenyekiti wa body amemuweka mahali ambapo anammudu.

We baba Kiama yako inakuja mda si mrefu
Boss kama mungu inaboa sana. Kun shirika flan Tanzania linaongoz kufanya marketing Tanzania nalo lina bos kichefchef kam huyo. Ni balaa tupu
 
Salute.

Naomba niende kwenye maada mimi kama askari (mlinzi) wa kampuni binafsi wa Garda world nimeamua kutumia platform hii kuleta kero ya kiongozi wetu mkuu wa kampuni ya ulinzi Garda world.

Kiukweli kiongozi wetu LuQmay tangu umepata kazi kwenye kampuni yetu sisi kama walinzi upande wa ultimate zamani kiukweli umekuwa tatizo kubwa na ni kero katika ufanyaji kazi.

Kwanza tangu umepata nafasi ya kuendesha kampuni ukitokea tigo hujawahi kuitisha kikao ujue wafanyakazi wako wanapitia shida gani na Nini malengo yako katika kampuni badala yake umekuwa (MUNGU MTU).

Naomba nieleze hapa kampuni ya ultimate kabla yakuwa Gardaworld imepitia mikononi mwa wamiliki wengi na Kila walipokuwa wanaamua kuuza kampuni Kwa mmiliki mwingine tulikuwa tuitwa kinafanyika kikao tunaeleweshwa na karibu hao maboss wote watu Ziballa & shivva nk.

Walikuwa wanafanya press tunajulishwa Kila kitu na walitoa pesa ya Asante nakumbuka nilipokea 1.2m maana nilifanya kazi Kwa miaka kumi na kipindi hicho chote tukiwa ultimate Kila baadae ya miezi sita.

Mkurugenzi aliitisha kikao tukasema kero zetu na zikafanyiwa kazi sasa tangu kampuni ya ultimate iuzwe na kuchukuliwa na Garda world.

Kiufupi tunaona tunaendeshwa kihuni hivi inakuwaje tunaenda kumuona mkuu wa mkoa mh chalmila hatupati ugumu wa kumuona iweje kwako Mkurugenzi ndugu luQmay utuwekee uzibe tusikuone kuleta kero zetu.

Pli kampuni imeuzwa mmiliki ambao ni wazungu wamekupa fedha wafanyakazi walipwe kama fidia ya kubadili mikataba Yao kutoka ultimate kwenda Garda world lakini kutokana na roho yako mbaya unataka kutuzima kinguvu Ili fungu uchukue na ni pesa nyingi ukiweza kutuzima tunaamini utatajirika sana tatu week mbili nyuma umenitisha kikao tumekuja kwenye kikao umetuwekea spika ndani ya ukumbi Yani wewe na team yako ya upigaji munaongea bila kuonekana sisi tunasikia tu kwenye spika mtu hatumuoni it's ok hata kama mmeamua kutufanya wajinga lakini sio Kwa level hiyo kikao.

Kilivyoshindikana ukapanga kikao tarehe Saba ulivyosikia na sisi tunakuja na wanasheria wetu mkaahirisha kikao Kwanini kiongozi LuQmay usijifunze

Kwa wenzio akina Eliuta mwanjawike walikuwa wanakula na kipofu alikuwa hakimbiii wafanyakazi mwisho usifikiri utatuendesha kirahisi kama unavyodhani..

Pia sisi tulidhani wewe mtu mweusi uwe mkombozi wetu Kwa hao wazungu lkn wewe ndio umekuwa mwiba kwetu hata kama ukifanikiwa kutudhurumu it's tutakuombea hata Dua mbaya tu maana mahakamini tukipekeleka kesi tukishinda unakuja kuappeal then uinaweka kapuni na kutishia kufukuza kazi wafanyakazi.

Ila Kwa hili la malipo ya mikataba tutaenda hata ubalozi wa Canada kushinikiza waiitwe wamiliki wa kampuni mwisho jifunzeni G4s na SGA uone kampuni zinavyoendeshwa.

Hivi mwanaume unashindwa tafuta eneo zuri ukaweka matunda na Mboga Mboga ujapata faida ya 10,000 kwa siku mpaka ufanye kazi Garda World kama mlinzi?

Akili tegemezi ni mzigo!

Angalizo:

Ukiamua kuajiriwa umeamua kuwa mtumwq, mnafiki na mtu wa kujipendeza ( and either mshirikina sana au mtu wa ibada sana)
 
Say No to GARDAWADA.
Jeshi la Polisi ambao mnasajili kampuni za Ulinzi take this note kama redflag ya uhalifu ujao.
Wadau/wateja epukeni hii kampuni soon Walinzi/wafanyakazi wataanza kufanya hujuma kulipa kisasi.
Tia kwenye dustbin hii kampuni wakose wateja

Heee! Sasa si kampuni itakosa mishahara, Tena this time huyu mkurugenzi boya ataitisha kikao kwa kutumia sauti iliyorekodiwa kwenye flash!
 
Umenikumbusha katika harakati za maisha, nikiwa na degree yangu, niliwahi kufanya kazi ya ulinzi KK Security. Nasikia nayo imechukuliwa na Gardaworld. Kazi ya ulinzi siyo ya kitoto. Unayemlinda anahisi wewe ni mtu baki kumbe hata elimu inawezakuwa unamzidi. Naamini ujumbe ameupata huyo mkurugenzi mpya kutoka Tigo.
 
Say No to GARDAWADA.
Jeshi la Polisi ambao mnasajili kampuni za Ulinzi take this note kama redflag ya uhalifu ujao.
Wadau/wateja epukeni hii kampuni soon Walinzi/wafanyakazi wataanza kufanya hujuma kulipa kisasi.
Tia kwenye dustbin hii kampuni wakose wateja
Kabisa kabisa asee
 
.......umetuwekea spika ndani ya ukumbi Yani wewe na team yako ya upigaji munaongea bila kuonekana sisi tunasikia tu kwenye spika mtu hatumuoni it's ok hata kama mmeamua kutufanya wajinga lakini sio Kwa level hiyo kikao.....

Hivi hata akikaa pekeyake anajisikiaje

Anaitisha kikao huku anakula nyeto hahahah nyie si ham muoni? Wazee wa speaker kwa speaker hahahahah watu wanadharau hii nchi!
 
Hivi mwanaume unashindwa tafuta eneo zuri ukaweka matunda na Mboga Mboga ujapata faida ya 10,000 kwa siku mpaka ufanye kazi Garda World kama mlinzi?

Akili tegemezi ni mzigo!

Angalizo:

Ukiamua kuajiriwa umeamua kuwa mtumwq, mnafiki na mtu wa kujipendeza ( and either mshirikina sana au mtu wa ibada sana)
Mkuu,

Tafadhali tueleweshe pima katika hili zonge!!!

Inasemekana Gardaworld imenunua KK Security na Ultimate Security na kuanzisha kampuni kwa usajili wa Tanzania iitwayo Gardaworld West. Lakini cha ajabu mchakato wa kuwabadilisha kutoka kampuni za zamani unafanyika kwa kampuni ya Ultimate Security pekee na kwamba hao ndio watalipwa wengine inadaiwa walishamalizana nao!
Je, kuna ukweli kiasi gani kuhusu mchakato huo kwamba KK Security na Gardaworld West wenyewe sio sehemu ya kulipwa? uttoh2002 Extrovert OKW BOBAN SUNZU Kalaga Baho Nongwa
Wakilipwa, Ultimate Security na KK Security wakaachwa ni halali na mahusiano kati ya walinzi wa kampuni hizo mfilisi zitakuwa katika hali gani na hujuma zikakosekana?
Elimu au ushauri unaotolewa na wataalamu wa kukodi una tija kwa kampuni na wafanyakazi au ni utumbuaji wa posho ambazo laiti watu wote wangelipwa wangepunguza gharama na hasara baada ya zoezi kukamilika kisha kesi nyingi kufunguliwa na baadhi yao wakidai kutoridhishwa na uendeshaji wa zoezi la uhamishaji ajira?
 
Mkuu mm sina utaalam sana na jambo hili mana sijawah kuwa mfanyakaz wa senior level katika kampuni. Lakin inawezekana hili likafanywa katika ngaz ya chini ili kuficha vitu vingi kutetea maslahi ya kampuni na kuipigania faida
 
Mkuu,

Tafadhali tueleweshe pima katika hili zonge!!!

Inasemekana Gardaworld imenunua KK Security na Ultimate Security na kuanzisha kampuni kwa usajili wa Tanzania iitwayo Gardaworld West. Lakini cha ajabu mchakato wa kuwabadilisha kutoka kampuni za zamani unafanyika kwa kampuni ya Ultimate Security pekee na kwamba hao ndio watalipwa wengine inadaiwa walishamalizana nao!
Je, kuna ukweli kiasi gani kuhusu mchakato huo kwamba KK Security na Gardaworld West wenyewe sio sehemu ya kulipwa? uttoh2002 Extrovert OKW BOBAN SUNZU Kalaga Baho Nongwa
Wakilipwa, Ultimate Security na KK Security wakaachwa ni halali na mahusiano kati ya walinzi wa kampuni hizo mfilisi zitakuwa katika hali gani na hujuma zikakosekana?
Elimu au ushauri unaotolewa na wataalamu wa kukodi una tija kwa kampuni na wafanyakazi au ni utumbuaji wa posho ambazo laiti watu wote wangelipwa wangepunguza gharama na hasara baada ya zoezi kukamilika kisha kesi nyingi kufunguliwa na baadhi yao wakidai kutoridhishwa na uendeshaji wa zoezi la uhamishaji ajira?

We fanya kazi; ukiona umechoka wacha, achana na uharakati kwenye kazi za watu, Sifa ya kuajiriwa ni Kuwa mnafikiri, mvumilivu, Mmbeya na mtu wa kujipendekeza
 
We fanya kazi; ukiona umechoka wacha, achana na uharakati kwenye kazi za watu, Sifa ya kuajiriwa ni Kuwa mnafikiri, mvumilivu, Mmbeya na mtu wa kujipendekeza
Boss uttoh2002
Mawazo na maoni ya mwingine yaheshimiwe
Eti mfanyakazi ajivike sifa za
1. Unafiki
2. Kuvumilia
3. Kujipendekza
4. Mmbeya (mtu wa kutia chumvi au kuongeza maji mengine) kuondoa au kukoleza ladha ya sifa au lalamiko wakati anateseka na kuogelea kwenye viashiria vya umasikini kwa mshahara wa kula bia kuweka akiba kwa maendeleo binafsi?
 
Back
Top Bottom