Mkurugenzi Geita afunga safari china kujifunza kuendesha wilaya hiyo kwa pesa kwa pesa za halmashauri

Mkurugenzi Geita afunga safari china kujifunza kuendesha wilaya hiyo kwa pesa kwa pesa za halmashauri

Mtu anakuwaje mkurugenzi mara mbili hyo si ndio mkurugenzi wa geita gold inakuwaje tena anakuwa na vyeo viwili kwa pamoja wataalam mnasemaje hapo bora hata angesema anaenda kujifunza kuendesha geita gold kidogo inge make sense.
we umerogwa amini nayo kwambia
 
we umerogwa amini nayo kwambia
Da zuhura tuachie geita yetu nenda ukasimamie ujenzi wa uwanja wa geita gold au ndio umeenda kuleta nyasi kwa hela za halmashauri.
 
Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Geita amefunga Safari kwenda China kujifunza namna ya kuendesha mji huo, jambo ambalo limeleta maswali mengi kwa wananchi kwa matumizi mabaya ya Pesa za walipa kodi ambao kimsingi ndio wananchi.

Hata hivyo Mkuu wa wilaya ya Geita Mh. Cornell Magembe ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani humo kuchunguza Fedha zilizotolewa na halmashauri hiyo ya mji wa Geita, kumpeleka Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Bi. Zuhura Michuzi kwenda China kwa ziara ya kujifunza namna ya kuendesha halmshauri hiyo ya mji wa Geita.
Ndio shida ya Vyeo vya kupeana Kwa connection
 
Hako kabinti ni miongoni mwa vidada vilivyo kula shavu vikiwa havijui lolote kiutendaji,yaani kalimaliza tu Degree UDOM kakapewa Ukurugenzi Wilaya ya Chemba kisha kakahamishiwa huko Geita,ni katoto ka Muhidin Issa Michuzi
Usije kushangaa DC ndio akatumbuliwa 😂😂
 
Sasa kwanini kwenye syllabus waliondoa topic kama fishing in Japan hawaoni kama ni makosa na matokeo ni haya

Sasa huyu pimbi huko china anaenda kusomeshwa nini ambacho kitaleta mabadiliko katika mkoa wake.Hii nchi kazi ipo sio shetani au Mungu anayeelewa tunachofanya
 
27 November 2023
Geita, Tanzania

Cornel Magembe - Baraza la madiwani msiache mitambo hii kuoza


View: https://m.youtube.com/watch?v=QAmCMCDw_l8

Mkuu wa wilaya ya Geita, DC Cornel Magembe alitaka baraza la madiwani kutafuta fungu la fedha kufufua mitambo ya kuchonga barabara ambayo imetelekezwa, lakini hawastuki...

DC Cornel Magembe asisitiza mapato ya ndani yapo kutosheleza kukarabati katapila la halmashauri bila kusubiri fedha au ruhusa kutoka Dodoma na anashangaa hili linashindikana vipi kulifanyia kazi kwa fedha za mapato ya halmashauri ili caterpillar lifanye kazi kwa hali endelevu bila kutelekezwa ....

Madiwani nao wasema tatizo ni mfumo wa manunuzi ya vipuri huwa ni mlolongo mkubwa .... hata hivyo baadhi wa madiwani wasema ni ukosefu wa utashi wa kuwajali wananchi wanaohitaji barabara nzuri zinazokarabatiwa kila wakati ili zipitike na kuchochea uchumi na maendeleo ya watu ...
 

Miradi itakayotekelezwa Geita​

  • Ujenzi wa Barabara ya Mwatulole hadi Mkoani
  • Ujenzi wa Stendi ya mabasi ya kisasa katika eneo la Magogo kata ya Bombambili
  • Ujenzi wa Barabara ya Nyankumbu - Kivukoni hadi Nyamalembo
  • Utafiti wa maji chini ya ardhi, uchimbaji wa kisima pamoja na ujenzi wa miundombinu na mtandao wa maji katika kijiji cha Ikulwa.

BILIONI 13 KUJENGA STENDI YA KISASA GEITA -DED ZAHARA MICHUZI​

Mzee wa Matukio Tuesday, October 31, 2023

69d0b946-fb24-4bb2-8508-130348c8cc0b-780x470.jpg

MKURUGENZI mtendaji wa Halmashauri ya Mji Geita Zahara Michuzi amesema kiasi cha Shilingi bilioni 13 kinatarajiwa kitumika kujenga kituo cha mabasi cha kisasa mjini Geita ikiwa ni sehemu ya Mradi wa Uboreshaji wa Miji Tanzania (TACTS) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia (WB).
Mkurugenzi wa Halmashauri huyo ameyasema hayo leo baada ya kukagua eneo lililotengwa kwa mradi huo ambalo limemegwa kutoka Hifadhi ya msitu wa Usindakwe.
Zahara amesema kituo hicho cha mabasi (stendi) kinakwenda kutatua kero ya muda mrefu kwa mji na mkoa wa Geita kwani stendi ya sasa haina ubora wa miundombinu inayostahimili kutoa huduma bora.
“Hatuna stendi yenye hadhi ya mkoa wenye dhahabu na madini, mheshimiwa Rais kwa kuliona hilo ametupatia hiyo stendi na sasa hivi tupo katika hatua ya upembuzi yakinifu na hatua za manunuzi.
“Tupo hatua za kuweza kupata mkandarasi mzuri mwenye uzoefu wa kujenga stendi hizi, zenye ubora na kuvutia katika mji wetu, kwa hiyo hizo taratibu zimeanza na zinaendelea.”
Amesema hadi Disemba, 2023 taratibu zote za awali zinatarajiwa kukamilika na mikataba itasainiwa ili utekelezaji uanze kwani halmashauri imejipanga mradi ukamilike kwa wakati na ufanisi.
“Stendi ile imelenga katika kukuza mji wa Geita, kuleta fursa mbalimbali za kiuchumi, kwani kutakuwa na sehemu ya uwekezaji wa hoteli, wafanyabiashara, wamachinga, bajaji, bodaboda, mamalishe, babalishe.
“Wakandarasi ambao wanakuja Geita na kusuasua kwenye miradi, mimi ndio mkurugenzi hapa Halmashauri ya Mji wa Geita sitowavumilia, itakuw akata mti panda mti, ukinizingua tnazinguana.”
Ofisa Mipango Miji Halmashauri ya mji wa Geita, Barbara Mustapha amesema eneo la mradi ni hekta 120 kutoka hifadhi ya msitu wa Usindakwe chini ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).
Amesema stendi pekee itatumia ukubwa wa hekta 10 huku eneo linalosalia kutakuwa na vyuo vya kati, maeneo ya biashara na pamoja maeneo ya uwekezaji.
Kaimu Mhandisi wa Miundombinu na Mratibu wa TACTIC Halmashauri ya Mji wa Geita, Mhandisi Oswald Mtei amesisitiza wapo hatua za mwisho za manunuzi na kumpata mkandarasi mradi uanze kujengwa.

Mkurugenzi akionesha eneo la kujenga stendi mpya


View: https://m.youtube.com/watch?v=I6rnDq-xaZk
 
Back
Top Bottom