Hawajui wamilikiMamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), imewataka wadau wote wa sekta ya usafirishaji nchini, kutopandisha nauli kwa kigezo cha kupanda kwa bei za mafuta na badala yake wafuate utaratibu rasmi utakaowekwa na watakaopandisha hawatasita kuwachukulia hatua kali za kisheria.
Akitoa kauli hiyo Kibaha mkoani Pwani wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari, Mkurugenzi Mkuu wa Latra CPA. Dkt. Habibu Suluo, amesema Aprili 8 ndio kitafanyika kikao cha wadau kujadili jambo hilo jijini Dar es Salaam.
Akaongeza kuwa wasafirishaji wanapaswa kujua kuwa hata wananchi bei hizo mpya zinawaumiza na hivyo nao wawe na huruma nao siyo kukimbilia tu kupandisha bei ya nauli.
Mkurugenzi huyo akaongeza kuwa wasafirishaji wote wanaotaka nauli zipande waje na maelezo ya kina namna wanavyotaka ipande na iwe kwa kiasi gani kwa mujibu wa sheria zinavyowataka.
Hahaha, sasa serikali si wasubsdize ili bei ishuke ya mafute, au hamna helaMamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), imewataka wadau wote wa sekta ya usafirishaji nchini, kutopandisha nauli kwa kigezo cha kupanda kwa bei za mafuta na badala yake wafuate utaratibu rasmi utakaowekwa na watakaopandisha hawatasita kuwachukulia hatua kali za kisheria.
Akitoa kauli hiyo Kibaha mkoani Pwani wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari, Mkurugenzi Mkuu wa Latra CPA. Dkt. Habibu Suluo, amesema Aprili 8 ndio kitafanyika kikao cha wadau kujadili jambo hilo jijini Dar es Salaam.
Akaongeza kuwa wasafirishaji wanapaswa kujua kuwa hata wananchi bei hizo mpya zinawaumiza na hivyo nao wawe na huruma nao siyo kukimbilia tu kupandisha bei ya nauli.
Mkurugenzi huyo akaongeza kuwa wasafirishaji wote wanaotaka nauli zipande waje na maelezo ya kina namna wanavyotaka ipande na iwe kwa kiasi gani kwa mujibu wa sheria zinavyowataka.
Nchi hii mwandishi mwenye maswali ni mmoja tu... Pascal MayallaMafuta yanapanda almost 25% nauli unataka ibaki vilevile??
Tatizo lingine sekta ya waandishi wa habari nayo ishaingiliwa imejaa upumbavu kiasi chake, kwanini mtu anavyotoa taarifa kama hio asitokee mwandishi amhoji maswali kua hilo linawezana vipi?
hiyo ndo ukisikia mifumo haisomani, kikao kinapigwa jumatano ijayo , wakati kuna maeneo bei ishachangamkaMafuta yanapanda almost 25% nauli unataka ibaki vilevile??
Tatizo lingine sekta ya waandishi wa habari nayo ishaingiliwa imejaa upumbavu kiasi chake, kwanini mtu anavyotoa taarifa kama hio asitokee mwandishi amhoji maswali kua hilo linawezana vipi?
kama walivyotuahidi gharama za umeme kushuka baada ya bwawa la Nyerere kukamilika. Viongozi wetu ni waongo sanaAkiba ya mafut ipo hadi July,
Hii kauli tuiache kama hii ilivyotuacha
wanatoa ahadi ya kushuka bei, baada ya miaka miwili waziri anaipongeza sekta kwa kutopandisha bei kwa kipindi cha miaka 10 --- wakati huo ahadi ya bei kushuka haijadiliwi tenakama walivyotuahidi gharama za umeme kushuka baada ya bwawa la Nyerere kukamilika. Viongozi wetu ni waongo sana