Mkurugenzi LATRA: Asipandishe mtu nauli kwa kusingizia mafuta kupanda

Mkurugenzi LATRA: Asipandishe mtu nauli kwa kusingizia mafuta kupanda

Hamiliki biashara huyo..kama anazo zote ni za wizi wa kodi na hata kama yupo na gari ni la wizi..mafuta ya wizi kila kitu cha wizi.

Hawezi kuwa mwanaume mwenye akili finyu hivyo kama anajua namna za maisha halisi.
Hajui uchungu wowote kwa sasa..akitakaaongee tofauti wamtoe hapo wafunge akaunti zake..arudi mtaaa ktafuta hela halali.
 
Mafuta yanapanda almost 25% nauli unataka ibaki vilevile??

Tatizo lingine sekta ya waandishi wa habari nayo ishaingiliwa imejaa upumbavu kiasi chake, kwanini mtu anavyotoa taarifa kama hio asitokee mwandishi amhoji maswali kua hilo linawezana vipi?
ni ongezeko la 35% ya bei ya awali
 
Kuna shipper ashanitumia ujumbe mzigo wangu unaokuja malipo yatakuwa tofauti sio yale niliyozoea. Na mimi wateja wangu kuanzia 01/04/2026 bei ya bidhaa nimeongeza hakuna namna.
Inabidi iwe hivyo boss
Hakuna namna

Ova
 
Ila kauli nyingine ni hatari sana kwenye biashara za watu. Kuwaambia wafanyabiashara hivyo ni sawa na kuwaambia wakubali ,itaji yao iporomoke kwa lengo la kuonesha uzalendo wa kugawanya maumivu.

Lengo la biashara yoyote ni kuzalisha faida kama hakuna faida hiyo siyo biashara ni huduma kama huduma nyingine tu. Mtazamo wa kibiashara ni faida na siyo nje ya hapo.

Kama tuna Nia njema ya kusaidiana maumivu nadhani njia nzuri ni Serikali kuondoa ushuru wa bidhaa za mafuta yanayoingia nchini kwa sababu kazi ya Serikali ni kulinda maskahi mapana ya umma "public interest" na siyo kuzalisha faida.

Uwanja huru "buffer zone" kati ya mfanyabiashara na mlaji hauwezi kusimamiwa na mfanyabiashara au mlaji ila Serikali.
 
Back
Top Bottom