Bandari inahitaji taaluma na ubobevu mkubwa wa biashara za usafirishaji baharini na kimataifa. Mkurugenzi wa sasa wa TPA ni msomi wa sheria, Mwenyekiti wa sasa wa bodi ya bandari ni aliyewahi kuwa IGP mstaafu, Ernest Mangu. Kuna wakati hadi wanasiasa kama Renatus Mkinga waliwahi kuwa wajumbe wa bodi ya TPA!
Pamoja na mahitaji mengine yote eneo la bandari linahitaji vipanga waadalifu, watu wenye ubobevu mkubwa katika maritime logistics, shipping and ports management , internationala global supply chain management na nyingine zinazofanana na hizo. Hawa ndio watu wanaoweza kuelewa kwa upana mahitaji ya biashara ya bandari katika ufanisi wa muda na kupunguza gharama.
Uongozi wa bandari haujawahi kuwa wa ubora huo stahiki na kwa sababu hiyo hakuna maajabu yoyote yangetegemewa au kutokea kutokana na pengo hilo.