"Hoja ya kusema kwanini mchakato huu (wa mkataba wa uendelezaji wa bandari ) hauhusishi Bandari ya Zanzibar ni kwa sababu Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) inahusika na upande wa Tanzania Bara na kule nako kuna wanaohusika na Zanzibar japo wote tupo kwenye Jamhuri moja ya Muungano wa Tanzania."Plasduce Mbossa, Mkurugenzi Mkuu wa TPA
“Mtu anapokwambia [bandari] imeuzwa lazima akueleze uratatibu, hiyo imeuzwaje uzwaje? Kwamba mtu anaondoka nayo, au anamiliki. Kwa hiyo ni seme hakuna suala la kuuza bandari. Kitakachofanyika ni kumwambia mwekezaji boresha, weka mitambo, hakikisha meli zinakaa masaa 2 badala siku 9 na vitu vingine vingi. Unamkodisha eno la kufanyia shughuli hizi za kibandari. Na hilo tumekua tukilifanya – mfano kuna kampuni ya Hutchison kutoka Hong Kong ambayo imekua iki operate hapa kwetu kama TICTS – imekaa kwa miaka 22 - haikuwa imeuziwa bandari na ndio sababu imeondoka Disemba 2022 – walikuwa wamekodishwa."-Plasduce Mbossa, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA)
"Katika majadiliano mengi tunayofanya zinatumika sheria za kimataifa. Kwa ujumla hakutakuwa na kipengele chochote kinachopingana na sheria zetu" Plasduce Mbossa, Mkurungezi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA)
"Kifungu cha 23 cha mkataba huu (wa uendelezaji wa bandari) kinasema mkataba huu unaweza kusitishwa iwapo pande mbili zilikubaliana na mikataba ya utekelezaji utakaofuata itakuwa na ukomo kadri ya mjadiliano" Plasduce Mbossa, Mkurungezi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA)
"Mkataba huu (wa uendelezaji wa bandari) si mkataba wa utekelezaji wa mradi wowote, ni mkataba mama na utafuatiwa na mikataba ya uwekezaji ambayo itafikiwa baada ya majadiliano." Plasduce Mbossa, Mkurungezi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA)
"Matarajio yetu ni kwamba wafanyakazi wote wa TPA watabaki na ajira zao na hilo tutaliweka katika mikataba ya makubaliano" Plasduce Mbossa, Mkurungezi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA)
“Hizo allegations [madai yanayohusu ubinafsishaji wa bandari], naamini kwamba zinalenga kudhoofisha jitihada ambazo Serikali inazifanya kuongeza ufanisi katika bandari yetu. Na mimi nasema kwamba tuko kwenye ushindani mkali sana.” Plasduce Mbossa, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA)
"Katika mikataba tunayoingia masuala yote ya ulinzi yanabaki kuwa ya nchi yetu na vyombo vya ulinzi na usalama vitaendelea kuwepo miaka yote. Vifungu vyote vya mkataba vinatakiwa kuzingatia masuala ya ulinzi kuwa ni la nchi husika" Plasduce Mbossa, Mkurungezi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA)
“Mikataba ya utekelezaji ambayo itaingiwa baada ya mkataba huu (wa uendelezaji wa bandari) kuridhiwa itakuwa na muda na pale itakapokwisha maana yake na mkataba huu wa awali utakuwa umekwisha. Maana yake ni kwamba muda wa mkataba huu wa awali utaupata katika mikataba hii inayofuatia” Plasduce Mbossa, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA)
"Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) itaendelea kuendesha maeneo mengine kulingana na makubaliano tutakayokuwa nayo. Lengo ni kuhakikisha kuna ufanisi na kukua kwa shughuli zingine za kiuchumi" Plasduce Mbossa, Mkurungezi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA)
"Hatuwatendei haki kuwaambia wabunge kwamba walipewa rushwa na Kampuni ya DP WORLD walipokwenda Dubai. Na unaiposema rushwa ni kitu kinachothibitishwa na mahakama. Na kama tukisema wabunge wetu walipewa rushwa tunawakosea heshima na mahakama ikisema kwamba wabunge waliopokea rushwa ndio nitakuwa na haki ya kusema kuna mtu/ wabunge wamepewa rushwa. Hatuangalii vitu hivyo" Plasduce Mbossa, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA)
“Baada ya Bunge kuridhia kutakuwa na mikataba ya utekelezaji wa shughuli husika kwa kuzingatia sheria, kama vile mikataba ya TEHAMA, mafunzo, uendeshaji na uendelezaji ambapo kwa sasa mikataba hiyo bado haijasainiwa.” Plasduce Mbossa- Mkurugenzi TPA
“Kwenye mkataba hakuna sehemu kuna miaka 100, nafikiri walioleta hilo wana sababu zao na ni upotoshaji wa hali ya juu. Mkataba uliopo una kifungu kinachosema kwamba kuna muda wa miezi 12 wa kuridhia na ikipita miezi 12 bila kuridhia maana yake mkataba utakuwa umekwisha. Pia kama tutaingia kwenye “negotiation” na tukashindwa kufikia muafaka na kusaini mikataba ya utekelezaji maana yake mkataba utakuwa umekwisha.” - Plasduce Mbossa- Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA)
"Mkataba baina ya serikali ya Dubai na Tanzania (IGA) una masharti ya kuridhiwa na pande zote mbili, masharti yetu ya kuridhiwa kwa mkataba huu ni kupeleka azimio la kuridhiwa kwa mkataba huu (wa uendelezaji wa bandari) bungeni" Plasduce Mbossa, Mkurungezi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA)
View attachment 2650122View attachment 2650123View attachment 2650124View attachment 2650126View attachment 2650126View attachment 2650127View attachment 2650129View attachment 2650129View attachment 2650130View attachment 2650131View attachment 2650132View attachment 2650133View attachment 2650134