Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, Maharage Chande asema pamoja na kukamilika kwa mradi wa Bwawa la Nyerere, watanzania tutegemee migao zaidi!

Maharage wanaweza kumtoa muda si mrefu.

Kwa sababu ni technocrat asiyeweza siasa, katika kazi inayotaka siasa.

Labda wanasubiri mradi tu.

Same thing happenned to Eric Hamisi at TPA.
 
Kwa hiyo ukame huandama Awamu ya 4 na hii tu? Kwa maana mgao wa sasa hivi ni copy&paste ya awamu ya 4, kubalini tu kwamba mko incompetent!
Hivi unajua awamu ya nne imeongeza umeme kiasi gani!?..unajua kabla ya project za awamu ya nne umeme ulikua ukizalishwa kiasi gani!?..unajua mgao ulianza lini!?..unaijua net group solutions na Hali ya umeme ilikuaje kipindi hicho!?..au umepata smart phone kipindi Cha magu ndo unafuatilia mambo kijuujuu!?...una umri gani!?
 

Sema kiasi gani Awamu ya 4 iliongeza?
 
Hivi wadau tujiulize kidogo...

Sasa hivi hata 2,000MW hatuna yaani tukimaliza Bwawa tutakuwa na mara mbili ya uzalishaji wa sasa...

Alafu unatwambia kwamba tunahitaji 60,000, yaani zaidi ya mara kumi ya capacity itakayo-double ?!!!!!

Ili zifanye nini kwa sasa na huo mgao kwanini uendelee wakati tulikuwa hatuna mgao kama huu wakati tuna less MW ?!!!!!

Au hizi ndio justification za kuendelea kununua mafuta na watu kuuzia umeme Tanesco ?!!!!
 
Well said chief, projection by 2045 population ya TZ tutakuwa close to 100M. Power Consumption per capita at current capacity itakuwa imezidiwa vibaya mno. Tunahitaji vyanzo vya umeme zaidi kila mwaka.
 
Idadinm ya watu inaongezeka pia lazima uzingatie.
 
nafikiri atakiwa amekosea labda alimaanisha 6,000Megawatt na Sio 60,000
Sisi hata baada ya Miaka 100. bado hatujafikia mahitaji hayo kaka
Mkuu kama kwa sasa tuko waTZ 60Million, ukichukua hiyo 6000MW ukagawanya kwa population unapata 60KW per head. Kwa shughuli combined za kiuchumi tena viwanda, 60KW consumption per capita mbona ni umeme wa kawaida sana. Haituchuki hata 10 years kma uchumi wa nchi inakua kwa kasi.
 
Idadinm ya watu inaongezeka pia lazima uzingatie.
Naam sikatai ila tupo on the verge ya ku-double capacity ya uzalishaji (na hapo nyuma hata kabla ya hio doubling mgao haukuwa mkali kama wa hivi sasa) na wala sioni influx ya viwanda vyovyote taa na electrical appliances they are more energy efficient kuliko before....

Sasa hata kabla hatujapumua before the doubling tunaambiwa tena kwamba ni business as usual ? (One can not stop thinking huenda ile mitambo ya kina Dowans / symbion tunaona shida / tabu kuizima)

Anyway binafsi najua kwamba haifai hii ndio iwe mwisho wa uzalishaji bali hii iwe kichocheo cha energy mix.... (lakini wakati tunafanya / tunatafuta hio mixture sio kwamba tuwe gizani)

 
Makamba na Maharage ni madalali wanaonadisha nchi hii.
Inabidi watambuliwe hivyo.
 
Kama kausema ukweli, kulikuwa na haja gani Kwa viongozi wetu wakuu wa Taifa, akiwemo aliyekuwa Rais wa awamu ya 5, Hayati Magufuli, kutuongopea kuwa mradi huo ndiyo utakaoweza kumaliza matatizo ya mgao wa Umeme nchini?
Na hivyo viwanda vingi anavyovizungumzia yeye vitamwagika tu mara moja kama uyoga, kiasi kwamba hizo MW 2,000 zote zitakuwa hazitoshi katika muda wa miaka hata miwili wakati njia nyingine za ufuaji zikiongezwa?

Hiyo lugha anayoitumia yeye ni ya kilaghai, akijua mipango wanayoiandaa wao kuwaliza waTanzania.

Wataleta vikampuni vyao hapa, halafu gharama za umeme zitaendelea kuwa juu sana kiasi kwamba hata huo uwekezaji wa viwanda hautakuwepo kwa sababu ya bei kubwa ya umeme.
 
ccm ingepumzika kwanza tu
 
Umetoboa penye ukweli wa asilimia 💯
 
Kesho Desemba 22, 2022 Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua hatua ya kuanza kujaza maji katika bwawa hilo lililokamilika asilimia 79 ikiwa ni matokeo ya uwekezaji wa Sh6.5trilioni zitakazokata kero kabla ya 2025.
Wakati watanzania wanasubiri umeme, hawa wao wanawaza uchaguzi wa 2025? Nchi hii haitakaa ipate maendeleo ikiwa tutaendelea kuongozwa na chama hiki hiki kilichoshindwa kuleta afueni kwa watanzania kwa zaidi ya miaka 60 😱 😱 😳 😳 🙄 🙄
 
Ndivyo alivyotamka huyo Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, kama kukosea basi ni yeye

Kama ni ukilaza, basi utakuwa kwake[emoji1]
Akili za kuambiwa changanya na za kwako

Sio una vabreti tu bila 7bu

Hiyo mega wait 60,000 ni wa Afrika nzima?

Hata angesema 6000 bado angekosea
 
Ndiyo ujue tunaongozwa na utawala wa aina gani 😎
 
Kweli kabisa. Ila kwa nini nchi kama za waarabu wa jangwani wanaendelea sisi wenye kila kitu including mafuta na almasi dhahabu na vito vyote tunabaki masikini tena wa kuomba omba na tunaona sifa ya kupiga makofi tukipata mikopo???
Akili zimeanza kukurudia😃
 
Huyu maharage sijui kala maharagwe ya wapi. Namshauri arudi dstv akaendelee kuuza ving'amuzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…