Kwanza kabisa napenda kukufahamisheni kuwa hakuna kuaminana tena msimwamnini mtu. si Admin, members, owners wala Moderators. Lakini kea sasa Usalama wa members na maisha yao ni muhim zaidi kuliko kupost na kuendelea kubishana.
Nashauri yafuatayo :
1. Admin/Mods wekeni option inayoruhusu members kufuta, ku edit vichwa via habari (hii inawezekana
2. Admin/Mods weaken kite au option ya IGNORE. hii inarahisisha kwa members ku block contents toka kwa trolls
3. Members wote watumie VPN kuingia Jamiiforums hivyo itakuwa ngumu kukamatwa na kupewa kesi zisizowahusu.
4. Kwa usalama zaidi tumieni WiFi ambazo ziko public kama kwenye Malls, Mahoteli au Majumbani au maofisi makubwa hivyo ni vigumu ku pin point who is who.
5. Point number 3 ni muhimu sana hivyo nasisitiza sana hilo
6. Kwa ambao mko kwenye ma Group ya Whatsapp wajulisheni wenzenu kuwa wawe makini na wanayoyasema kwa sababu ya hii sheria mpya
7. Mods na Admin wapatieni members options za kufuta threads zao na pia kujiondoa membership kwa sasa mpaka hapo hali itakapokuwa imetengemaa. Kwa sababu usalama ni muhimu zaidi katiza zama hizi tulizo nano
8. Wajulisheni watu wengine kuwa huu si muda muafaka kujiunga na hii forum mpaka hapo Max atakapotoka nje na kuelezea Umma hatua zipi zimechukuliwa kulinda privacy za members
9. Uongozi wa Jamiiforums Uelezee umma wa watanzania wanafanya jitihada zipi za kisheria ili kumsaidia Max atoke. Je kama ni wanasheria ni kiasi gani kinahitajika etc.
10. Kwa sasa Twitter/facebook/Instagram ni salama zaidi (kama mnatumia majina feki) kujieleza kuliko mtandao wowte ule ambao una uhusiano na Tanzania
WITO KWA SERIKALI
Sisi wengine tulikuwepo toka mwaka 2002 enzi za TZATL, YoungAfricans,Darhotwire,Jambo forums mpaka tumefika Jamiiforums
Ina Uslama na hususana USALAMA WA TAIFA wanatufahamu na tunawafaham na wao wanaamini kuwa tunafanya kazi nzuri ya kukosoa serikali na kusaidia vyombo vya ulinzi na usalama maovu na mengineyo. Sisi kama members wa Jamiiforums tunaamini uhuru wa kujieleza na ndio maana hata kama hatukubaliani na watu lakini bado hutetea uhuru wao wa kujieleza. Sisi ni vijana wazalendo na hatulipwi. Na kwenye dunia hii ya leo serikali na vyombo via ulinzi na usalama walitakiwa kuwa ni partners wetu na sikutupiga vita na siku mbiu ya mambo itakapo lia tutajitokeza kufanya wajibu wetu kupigana na maadui wa nje (hususana nchi jirani ambao wana jeshi kubwa la ma cyber volunteer) wa kwa ku flood DNS za serikali na strategic installations zao.
Tunaomba Max aachiwe na sisi kama members na owners wa Jamiiforums pia itabidi tufanye soul searching kuwa at what point tulipoteza mwelekeo na tufanyeje turudi kwenye kukata issues na sio haya mambo ya ubishi kati ya vijana wa Lumumba na Bavicha
Niko radhi tukawa off line lakini tukirudi turgid fresh na sio kwa hii style tuliyonayo sasa hivi