Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo anashikiliwa na Polisi, anyimwa dhamana

Hii dhambi ya sheria ya mitandao mkwere haitomuacha salama
 
Tulianza na kuzuia Bunge live
Siasa mpaka 2020
Baadaye kama masikhara hivi Mkuu akasema anatamani mitandao ya kijamii hasa JF(Ingawa hakutaja moja kwa moja) isingekuwepo kabisa due to critics ambazo anapata , lakini ni muhimu kukosolewa ili kujua ni wapi ulipojikwaa na kusonga mbele.Sasa hatutaki kushauriwa wala kukosolewa,yeyote atakayethubutu kukosoa basi mpinzani,yaani sasa tunatakiwa kuwa watu wa ndiyo Mzee πŸ™πŸ™
This is awkward Government to deal with😎😎😎
 
China fb ipo sema sio maarufu ni ka uku kwetu na twitter vile.....
 
Vipo vigezo humu na masharti pia. Ulitaka yapi tena? Au ndio woga kwahiyo unaanza kujitakatisha na comments safi
Tumia akili ww
unajua kinachomfanya ashikiliwe na jeshi la polisi au?
 
Ndio maana kuna wahariri na wakiona hakuna ukweli huwa wananondoa taarifa hiyo mapema,
Ni kazi ngumu sana kushindana na technology
Ndio maana narudia tena habari yoyote ya uzushi inaondolewa na hao wahariri. Mfano ni ile habari ya kuteuliwa kwa wassira na CCM ile ilikuwa habari ya uzushi na ilaondolewa.

nikupe mfano mdogo tuu.

Members atakayeanzisha uzi na kusema uteuzi wa mkuu wa mkoa wa arusha umetenguliwa na mod wakahakikisha kuwa ni uzushi watauondoa.

Members atakayeanzisha uzi na kuweka barua ikiwa na nembo ya ikulu na sahihi ya msemaji wa ikulu au muhuri wa hakimu na mod wakahakikisha kuwa ni uzushi na wakaondoa huo uzi hawatakuwa wameondoa na kosa la kughushi sahihi ya msemaji wa ikulu.

Hilo ni kosa la jinai na hata kama uzi utaondolewa na huyo members kuwa banned bado nyuma ya pazia atabaki kuwa mhalifu kama wahalifu wengine.
 
Hii sheria iliyopelekea kukamatwa kwa CEO wa JF ilipelekwa Bungeni na ikapitishwa ina maana imekuwa Sheria, na haina tofauti yoyote ile na sheria nyingine zote zilizopitishwa na Bunge letu halali ambalo tumelichagua wenyewe, sasa kwa nini mnalalamikia leo utekelezaji wa Sheria iliyopitishwa na Bunge?

Kwangu mimi hamna tofauti na mtu anayelalamikia mtu aliyekamatwa kwa kubaka au kuiba kwa kuwa tu anamfahamu, kwa maana wote wamevunja Sheria za nchi zilizopitishwa na Bunge, hivyo kwangu ni unafiki mkubwa kujitokeza sasa hivi kuimba demokrasia wakati muda wa kufanya hivyo ulikuwepo, na hamkuutumia ni kwa nini hamkuandamana kupinga?

Wengi wenu mnaishi nchi za Wazungu lkn hata mifumo ya huko haimuilewi, Sheria ikishapitishwa kinachofwatia ni utekelezaji TU, na hii ni Dunia nzima, hivyo mlipaswa mpinge kabla haijapitishwa na sio kulalamikia utekelezaji wa Sheria huo ni ujuha!
 
Sizonje mtu wa ajabu kabisa kama anataka kufanya kazi afanye itaonekana tuu kwenye kumpongeza tutafanya hivyo na kwenye kumponda tutafanya hivyo daima ndo maisha yetu tuliyochagua great thinkers, we will always be one step ahead of you sizonje!

Musa tu aliyewatoa waisrael kwenye mateso misri alilaumiwa na wengine kumkejeli live japo njia ya kufika kaanan hawakuijua.
Lawama zipo na zitaendelea kikubwa ni kuhakikisha unatenda haki kila inapowezekana japo ni ngumu kumridhisha kila mtu.
 
Max!usijali kulala siku moja lock up,all great people walipitia, komaaa mwanangu.
 
Tafuta ile barua ya Ikulu ikiwa na muhuri wa ikulu na sahihi ya msemaji wa ikulu ikielezea kutenguliwa uteuzi wa mrisho gambo ile ilikuwa ni Pure Criminal case ilipostiwa humu JF kwa mara ya kwanza baada ya ugomvi wa Lema na gambo
Kwa mfano,tamko la kufoji la serikali ni lipi?
 
Habari za mashoga zinahusiana vipi ?
Kung'amua kama sio ukweli ni swala la mtoa habari
Kwanini alete habari ya kizushi ?
Serikali iwe kilasiku kukanusha uzushi !!!
Kwa mfano habari ya kufukia maiti saba waziri mmoja anasema ni wahamiaji haramu na mkubwa wake anasema ni magaidi sasa huo sio uzushi na uchochezi kwa wote au mmoja wao?taarifa kama hii utaamini yupi kwa uchunguzi gani na uhalali gani wauliwe vile?
 
Kiufupi hata wakiifungia Hii mitandao ya kijamii kuna njia nyingi za kuipata na hata kuirudisha hewani.

FBI na CIA kila siku wanapambana na hawa watu wanaoleta illegal downloads kama torrent sites na hawana hata muelekeo wa kushinda vita hiyo. Wanasema ukikata kichwa cha mmoja viwili huota pale ulipokata. Ni kama mbwa akijaribu kuukimbiza mkia wake hatofanikiwa.



Intaneti wengi wetu tunayotumia (Surface web) ni asilimia chache tu ya intaneti yote, na hata ukipewa mwaka mzima huwezi kuimaliza.

Sasa wakitaka kupambana na huu mtandao basi Jamiiforums inaweza hata kuhamia huko kwenye deep web.

Sidhani kama wafanyakazi wa serikalini wapo competent enough kupambana hii vita labda watangaze tenda kwa kampuni binafsi ama kuomba msaada nchi jirani.

Ninachoamini ni kwamba Jamiiforums ipo na itazidi kuwepo.
 

Mkuu yupi huyo?
 
Hapo alichochewa nani na alifanya nn baada ya kuchochewa ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…