Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo anashikiliwa na Polisi, anyimwa dhamana

Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo anashikiliwa na Polisi, anyimwa dhamana

John Pombe Magufuli ....wengine tumekuunga mkono kwenye mvua na jua tukiamini unajenga Taifa jipya na uelekeo mpya. Kukamatwa kwa Maxence Melo na sababu za kukamatwa kwake HAIKUBALIKI!
 
Huu ni ushauri kwa wale wenye hofu ya Mungu kutambua kuwa kujisajiri kwa majina ya uongo ni kutenda dhambi ya uongo.

Na hii ndiyo sababu wengi wanajificha kwenye majina ya uongo kudaganya au kutukana.
Wakiamini hawawezi kupatikana.
Hii forum ni free and open to everyone hulazimishwi, inasomwa na watu wa mataifa mbalimbali si Tanzania pekee, hivyo kumlazimisha mchina ajisajili kwa jina lake haitakuwa fair utakuwa unaingilia privacy yake.
 
Jamii forum wabadilike ili kila mwanachama aje humu kwa jina lake halisi kwani kuna ubaya gani?

Hivi kama wewe unamheshimu na kumwogopa Mungu na umeahidi moyoni mwako kuyatenda yaliyo ya kweli na kuukwepa uongo.

Harafu ukajiunga jf kwa jina la uongo huoni kwamba unatenda dhambi?

Jf inawaongoza wana chama wake kutenda dhambi ya uongo na kwenda jehanum ya moto.

Nashauri kila mwanachama aje kwa jina lake halisi.
Kwa majina haya ya uongo kitu gani kinafichwa?
Mkuu mbona wewe siyo verified member?
 
Uhuru Wa kujieleza ndiyo Sera ya Jf, ndo maana kila MTU anauhuru Wa kutumia jina lolote, na taarifa za siri ni za mhim, vinginevyo watu wataacha kuchangia...

Hum ndani kunawatu Wa juu kabisa na wasomi, usishangae hata presidooo yumo, ila kwa a.k.a, so watuache tujiachie walao tuwe na sehem ya kuondoa stresses,

Maana life ngum so tukinyimwa na kuongea kunasiku watu wataongea kwa vitendo, jaman nawaza kwa sauti tu...
 
Jaman, huu ukuu WA watu kutesa wanyonge ipo siku itakuwa shubiri kwa kizazi chao,kwanini Tanzania imekuwa kituko siku hizi? Huu Ni mfumo gan WA maisha? Serikali tupeni uhuru tafadhali
 
John Pombe Magufuli ....wengine tumekuunga mkono kwenye mvua na jua tukiamini unajenga Taifa jipya na uelekeo mpya. Kukamatwa kwa Maxence Melo na sababu za kukamatwa kwake HAIKUBALIKI!
Ulimuunga mkono kwa sababu hukumjua. Haya ya sasa ni jpm in action original. Endelea kumkubali tu.
 
Mkuu wewe mkongwe sana humu. Sheria za JF unazijua. Unafikiri Max anaweza kulinda mwanachama mzushi?

Sasa mkuu, unadhani Max anamkingia nani kifua?

Yaani wale wanachama wazushi?
 
Hayo hayakuwa makusudio ya kuanzishwa kwa JF.

Max na wakuu wengine walikuwa na lengo jema kabisa la kuanzisha JF.
Ninakumbuka wakati uleeeee zilikuwa zikiletwa thread za udaku au madai fulani zilikuwa zikiwekwa pending kusubiri ukweli. Kama hakuna ukweli zilikuwa zinafutwa.

Kwa sasa nadhani MOD's wamezidiwa na uwingi wa thread kiasi kwamba inawawia vigumu kupitia kila thread.

Kwa sasa kuna hizi ID's zilizojiunga late 2015 na mwaka huu 2016 ambazo hata michango yake ni kama uko facebook au instagram. Ninaamini michango ya aina hii ya kifacebook na instagram imewafanya baadhi ya watu wenye uelewa mpana kwa sasa kutochangia kwenye mijadala mbali mbali.
 
Uhuru Wa kujieleza ndiyo Sera ya Jf, ndo maana kila MTU anauhuru Wa kutumia jina lolote, na taarifa za siri ni za mhim, vinginevyo watu wataacha kuchangia...

Hum ndani kunawatu Wa juu kabisa na wasomi, usishangae hata presidooo yumo, ila kwa a.k.a, so watuache tujiachie walao tuwe na sehem ya kuondoa stresses,

Maana life ngum so tukinyimwa na kuongea kunasiku watu wataongea kwa vitendo, jaman nawaza kwa sauti tu...
Uhuru wa kujieleza una mipaka yake soma hii paragraph nadhani imewekwa hapo juu na moderator katika post #1 kuwa

" Watumiaji wa mtandao wa JamiiForums wako huru kuweka mijadala, kuanzisha mijadala, kuchangia chochote pasipo kuvunja sheria za nchi au kuhatarisha usalama wa taifa."

Unapoweka barua ya Ikulu tena ikiwa na nembo ya ikulu na sahihi ya kufoji ya msemaji wa ikulu huku ukijua kufanya hivyo ni kosa la jinai nia nini hasa kama si kutaka kuvunja sheria za nchi au kuhatarisha usalama wa taifa. Na hicho si serikali tuu hata uongozi wa JF unakipinga.

Alipofika maxence mello leo ni ujinga wetu sisi kama members wa JF kujali zaidi maslahi ya Matumbo yetu huku tukijua wazi tunawasababishia matatizo uongozi wa JF.

Tukipost kwa staha na kwa kutoa mawazo ambayo si ya kutengeneza makosa ya jinai kama kuleta Machapisho ya serikali tena ya kufoji sidhani kama mello leo hii angekuwa selo.
 
Wanazidi kututia ujasili wa kufanya lolote popote wakati wowote kwa yeyote..this is intensive training for tanzanians...freedom is coming tomorrow
 
Wanataka kuturudisha gizani kwa faida ya wachache. Bwana wa majeshi no mkuu kuliko. Baba tutakuombea vipi ikiwa jamiiforum inataka kutekwa nyara. Wengi wetu miskiti na makanisa yako humu humu jf , ndimo tunakokuombea.
 
Jamii forum wabadilike ili kila mwanachama aje humu kwa jina lake halisi kwani kuna ubaya gani?

Hivi kama wewe unamheshimu na kumwogopa Mungu na umeahidi moyoni mwako kuyatenda yaliyo ya kweli na kuukwepa uongo.

Harafu ukajiunga jf kwa jina la uongo huoni kwamba unatenda dhambi?

Jf inawaongoza wana chama wake kutenda dhambi ya uongo na kwenda jehanum ya moto.

Nashauri kila mwanachama aje kwa jina lake halisi.
Kwa majina haya ya uongo kitu gani kinafichwa?
Wewe Jina lako halisi ni "nyamnini "nani? anza na wewe na wengine watafuata
 
Na tuwe makini hasa wale tulio jukwaa la biashara ukitoa namba ya simu kule imekula, au ukisema uletewe mzigo "utaletewa vitu" [HASHTAG]#justthinkinglikeaCIAagent[/HASHTAG]
 
Kumbuka mambo mengi kama si yote yanayofanyika gizani au kwa kificho yanatoka kwa yule mwovu shetani.
Kwa hiyo ya bungeni yote yanatoka kwa yule mwovu shetani kwa vile yanafanyika gizani?
 
Back
Top Bottom