TANZIA Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Gissima Nyamo-Hanga na dereva wake wafariki dunia

TANZIA Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Gissima Nyamo-Hanga na dereva wake wafariki dunia

Tuweke mpango na kupanua trunk roads zote. Barabara zetu kuu nyingi bado ni nyembamba sana
 
Another scrap metal, LC300 hilo wanangu wa Tandale, ilala na shaurimoyo.

Kila siku tunawaambia mboreshe miundo mbingu iwe rafiki Kwa watanzania hamuelewi, angalia sasa miundombinu inawaua wenyewe.
Mjue pia Watanzania wanakufa Kila siku pia huku barabarani kwa sababu ya miundombinu mibovu.
 
Hakuna dharuru ndugu yangu ,hii watumishi wanajua ...Hii tunaita road trip ,hapo mtu atakaa njiani siku mbili au tatu ili kuongeza per diem ...Huyo jamaa anaweza hata kuchukua ndege ya kukodi (charter flight) akaenda anapotaka..


Ni ujanja tu ndugu yangu.
Tushawahi kusafiri kwa siku 3 kilomita 1200.
Ingawa usafiri ulikuwa wa bure na nilikuwa nalala kwenye basi kunavyokaribia kupambazuka lakini nilitumia zaidi ya laki 2 kwa kujibana maana kila mkoa tukawa tunalala inatulazimu tunywe bia tu.
 
Inna Lilah Wainna Ilaih rajiuun,Sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake yeye tutarejea.Mwenyezi Mungu atufanyie wepesi
 
Mkuu kutembea na gari kuna raha yake, Mbona Mabalozi wa nchi za Ulaya na Marekani utakuta wana safari kwa Gari kuto Dar mpaka Iringana wengine mpaka Kigoma, kusafiri kwa Gari binafsi kuna raha yake.
Kama dereva akiwa na nidhamu ya barabara siyo hawa wa serikali kiburi mpaka kwenye nywele
 
Mhandisi Nyamohanga Gissima Mkurugenzi wa TANESCO na Dereva Wake Wafariki dunia ambaye jina lake sijalipata wamefariki Dunia kwenye Ajali liyyotokea saa nane Usiku wakiwa njiani kuelekea Msoma. Walikuwa wanakaribia Serengeti

Wapumzike kwa amani

"Tunayaangaza maisha yako"

TANESCO MAKAO MAKUU, S.L.P. 453, DODOMA, TANZANIA, SIMU 180

TAARIFA KWA UMMA

TANZIA

Jumapili, 13 Aprili 2025.

Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) inasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga, kilichotokea leo tarehe 13 Aprili 2025 kufuatia ajali ya gari iliyotokea katika Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara.

Bodi ya Wakurugenzi inatoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, wafanyakazi wa TANESCO, na Watanzania wote kwa msiba huu mkubwa.

Taarifa zaidi kuhusu taratibu za mazishi na shughuli nyingine za maombolezo zitatolewa kadri mipango inavyoendelea kuratibiwa.

Imetolewa Na:

KURUGENZI YA MAWASILIANO NA HUDUMA KWA

WATEJA TANESCO MAKAO MAKUU DODOMA

====

MY TAKE

Tanzania tumemkosea nini Mungu? Kwanini tukipata Mchapakazi hadumu kwenye Uongozi anafariki Dunia? Inabidi tuliombee Taifa. Nampongeza Nyamohanga kwa kulitendea haki taifa. Alijuwa mchapakazi na mwenye IQ kubwa pia ameachia Vitu vingi na kafanya vitu vingi TANESCO sio Kama yule Maharage na Kampani yake. Nahisi kuna mkono wa mtu.

Haya ma V8 LC yameua Vigogo wengi sana
 
Mkuu kutembea na gari kuna raha yake, Mbona Mabalozi wa nchi za Ulaya na Marekani utakuta wana safari kwa Gari kuto Dar mpaka Iringana wengine mpaka Kigoma, kusafiri kwa Gari binafsi kuna raha yake.
Hawa wa kwetu Huwa wako speed na kiburi Cha gari ya serikali
 
Mkuu kwa gari ya Aina hiyo, umbali wa safari na majukumu ya anayeendeshwa ni hasara Sana kutembea mwendo mdogo.

Gari inamruhusu kukanyaga Moto, na Sheria za barabarani nazo haziwabani Sana watu wenye nyadhifa kubwa.
Ajali zitawabana
 
Mhandisi Nyamohanga Gissima Mkurugenzi wa TANESCO na Dereva Wake Wafariki dunia ambaye jina lake sijalipata wamefariki Dunia kwenye Ajali liyyotokea saa nane Usiku wakiwa njiani kuelekea Msoma. Walikuwa wanakaribia Serengeti

Wapumzike kwa amani

"Tunayaangaza maisha yako"

TANESCO MAKAO MAKUU, S.L.P. 453, DODOMA, TANZANIA, SIMU 180

TAARIFA KWA UMMA

TANZIA

Jumapili, 13 Aprili 2025.

Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) inasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga, kilichotokea leo tarehe 13 Aprili 2025 kufuatia ajali ya gari iliyotokea katika Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara.

Bodi ya Wakurugenzi inatoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, wafanyakazi wa TANESCO, na Watanzania wote kwa msiba huu mkubwa.

Taarifa zaidi kuhusu taratibu za mazishi na shughuli nyingine za maombolezo zitatolewa kadri mipango inavyoendelea kuratibiwa.

Imetolewa Na:

KURUGENZI YA MAWASILIANO NA HUDUMA KWA

WATEJA TANESCO MAKAO MAKUU DODOMA

====

MY TAKE

Tanzania tumemkosea nini Mungu? Kwanini tukipata Mchapakazi hadumu kwenye Uongozi anafariki Dunia? Inabidi tuliombee Taifa. Nampongeza Nyamohanga kwa kulitendea haki taifa. Alijuwa mchapakazi na mwenye IQ kubwa pia ameachia Vitu vingi na kafanya vitu vingi TANESCO sio Kama yule Maharage na Kampani yake. Nahisi kuna mkono wa mtu.

Looh, ajali mbaya sana hii Mungu azilaze mahali pema roho za marehemu! Gissima alikuwa anajua kuchapa kazi, nilifanya naye kazi kwa ukaribu kabisa kipindi akiwa mkurugenzi wa ufundi pale REA kabla hajawa DG wa REA!
 
Mchina akiongea kiswahil kikimpiga chenga mnaona poa ila mswahili akipigwa chenga nakizingu mnaona dhambi nan anawaroga nyie
Mchina akiongea kiswahili na kukosea ni sawa kwa sababu hana option pale anapokuwa Tz. Sasa huyu ndugu yetu ana ulazima gani wa kutumia lugha inayompiga chenga wakati kuna kiswahili?
 
Back
Top Bottom