peno hasegawa
JF-Expert Member
- Feb 24, 2016
- 18,223
- 31,465
Kwao ni Mkoa wa Mara?
Kwa vigezo vipi?Wazungu wanaamini usafiri wa ndege ni salama zaidi kuliko barabara, hivyo ni Bora viongozi kutumia ndege zaidi.
R.I.P
Madhambi yanayofanywa na mihimili ya Dola yanamchukuza Mungu na kwa njia hiyo Mungu anafikisha ujumbe kwa wateuliwa wengi wao wakiwa wema na endapo wenye mihiimili ya Dola wakeiendelea na maovu yao hapo ndipo Mungu anayashusha ghadhabu kwao.Mhandisi Nyamohanga Gissima Mkurugenzi wa TANESCO na Dereva Wake Wafariki dunia ambaye jina lake sijalipata wamefariki Dunia kwenye Ajali liyyotokea saa nane Usiku wakiwa njiani kuelekea Msoma. Walikuwa wanakaribia Serengeti
Wapumzike kwa amani
"Tunayaangaza maisha yako"
TANESCO MAKAO MAKUU, S.L.P. 453, DODOMA, TANZANIA, SIMU 180
TAARIFA KWA UMMA
TANZIA
Jumapili, 13 Aprili 2025.
Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) inasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga, kilichotokea leo tarehe 13 Aprili 2025 kufuatia ajali ya gari iliyotokea katika Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara.
Bodi ya Wakurugenzi inatoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, wafanyakazi wa TANESCO, na Watanzania wote kwa msiba huu mkubwa.
Taarifa zaidi kuhusu taratibu za mazishi na shughuli nyingine za maombolezo zitatolewa kadri mipango inavyoendelea kuratibiwa.
Imetolewa Na:
KURUGENZI YA MAWASILIANO NA HUDUMA KWA
WATEJA TANESCO MAKAO MAKUU DODOMA
====
MY TAKE
Tanzania tumemkosea nini Mungu? Kwanini tukipata Mchapakazi hadumu kwenye Uongozi anafariki Dunia? Inabidi tuliombee Taifa. Nampongeza Nyamohanga kwa kulitendea haki taifa. Alijuwa mchapakazi na mwenye IQ kubwa pia ameachia Vitu vingi na kafanya vitu vingi TANESCO sio Kama yule Maharage na Kampani yake. Nahisi kuna mkono wa mtu.
Umeelezea vizuri sana hapo, safari kama hiyo lazima iwe imeandaliwa kitu kinaitwa Journey Management Plan na watu wa logistics & safety wa Tanesco, swali la kujiuliza kwa nini asafiri usiku? Je gari limefungwa mfumo wa kudhibiti mwendokasi? Ni masaa mangapi gani gari la Serikali linaruhusiwa kutembea mchana au usiku?Ndio asafiri SAA nane ya usiku? Kuendesha Gari usiku ni hatari sana kwa dereva, abiria, chombo chenyewe na watumiaji wengine wa barabara.
Ndio maana kwenye taasisi zinazoongozwa na watu wenye akili wanakuwa na kitu kinaitwa journey management kabla ya kuanza safari yoyote.
Anaonyesha safari itaanza asubuhi ya SAA ngapi, mtapita njia ipi? Barabara mtakayoitumia ikoje? Mtakula wapi? Mtalala wapi? Etc.
Unapoendesha Gari kukiwa na mwanga wa Asili, dereva huona vizuri na akili inakuwa active.
Kuendesha SAA nane usiku ni hatari sana, boss kalala, dereva anaendesha huku kasinzia
Ajali ngapi zinatokea asubuhi na mchana?Ndio asafiri SAA nane ya usiku? Kuendesha Gari usiku ni hatari sana kwa dereva, abiria, chombo chenyewe na watumiaji wengine wa barabara.
Ndio maana kwenye taasisi zinazoongozwa na watu wenye akili wanakuwa na kitu kinaitwa journey management kabla ya kuanza safari yoyote.
Anaonyesha safari itaanza asubuhi ya SAA ngapi, mtapita njia ipi? Barabara mtakayoitumia ikoje? Mtakula wapi? Mtalala wapi? Etc.
Unapoendesha Gari kukiwa na mwanga wa Asili, dereva huona vizuri na akili inakuwa active.
Kuendesha SAA nane usiku ni hatari sana, boss kalala, dereva anaendesha huku kasinzia
tukumbushe mkuuDo u think is the first time such issue happen? Do u know Salvatory Mosha the brain behind Tanesco 🤔
wanasema dereva alimkwepa mwendesha baiskeli!nikawaza saa 7 za usiku, mwendesha baiskeli katoka wapi usiku wote huu?Aisee Land cruiser lote halifai kama karatasi vile, sijui wamepataje ajali na nimeona hapo lorry liko pembeni, uso Kwa uso Nini?. Kusema kweli wakati mwingine hata kama una haraka sana hebu tafuta sehemu ulale kwanza utulie upate utimamu tena.
Una haraka ya kwenda wapi?. Miundombinu yenyewe si mizuri sana ukihama kidogo tu tayari jua ushakufa na hasa ukikutana na wazee wa malorry aaahh umekwisha tena usiku. Kama Kuna uwezekano wa kusubiri Hadi kupambazuke basi ni Bora usubiri kukuche, inakuongezea kidogo nafasi ya kuishi.
Sisi hatujifunzi, Hadi likutokee wewe ndo unapata akili, Bado wengi tu watakufa sana Kwa vitu vidogo tu ambavyo tunavidharau tuwapo safarini.
Ndege hazipati ajali?Mkurugenzi wa Tanesco anasafiri umbali wote kutoka dar mpaka Msoma kwa gari kwani ndege hazikuwepo?
Walllah Hawa watu wanatia taifa hasaraMbona hujaongezea na mwendo kasi?
Ni kweli inaendeshwa ardhini Kawa ipo angani.Hizo gari wanazichomoa bana
Kama ndege
Anyway poleni ndg jamaa
Ova
Aisee baiskeli usiku wa manane?wanasema dereva alimkwepa mwendesha baiskeli!nikawaza saa 7 za usiku, mwendesha baiskeli katoka wapi usiku wote huu?
Mda wote anaiona alhamdulillah.Mungu anakuona