TANZIA Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Gissima Nyamo-Hanga na dereva wake wafariki dunia

TANZIA Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Gissima Nyamo-Hanga na dereva wake wafariki dunia

Mhandisi Nyamohanga Gissima Mkurugenzi wa TANESCO na Dereva wake ambaye jina lake ni Muhajir Mohamed Haule, wamefariki Dunia kwenye Ajali liyyotokea saa nane Usiku wakiwa njiani kuelekea Msoma. Walikuwa wanakaribia Serengeti
View attachment 3302678View attachment 3302679
Picha hapa juu ni Muhajir Mohamed Haule, Dereva wa TANESCO wakati wa Uhai wake

Wapumzike kwa amani

"Tunayaangaza maisha yako"

TANESCO MAKAO MAKUU, S.L.P. 453, DODOMA, TANZANIA, SIMU 180

TAARIFA KWA UMMA

TANZIA

Jumapili, 13 Aprili 2025.

Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) inasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga, kilichotokea leo tarehe 13 Aprili 2025 kufuatia ajali ya gari iliyotokea katika Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara.

Bodi ya Wakurugenzi inatoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, wafanyakazi wa TANESCO, na Watanzania wote kwa msiba huu mkubwa.

Taarifa zaidi kuhusu taratibu za mazishi na shughuli nyingine za maombolezo zitatolewa kadri mipango inavyoendelea kuratibiwa.

Imetolewa Na:

KURUGENZI YA MAWASILIANO NA HUDUMA KWA

WATEJA TANESCO MAKAO MAKUU DODOMA

====

MY TAKE

Tanzania tumemkosea nini Mungu? Kwanini tukipata Mchapakazi hadumu kwenye Uongozi anafariki Dunia? Inabidi tuliombee Taifa. Nampongeza Nyamohanga kwa kulitendea haki taifa. Alijuwa mchapakazi na mwenye IQ kubwa pia ameachia Vitu vingi na kafanya vitu vingi TANESCO sio Kama yule Maharage na Kampani yake. Nahisi kuna mkono wa mtu.

mbn dereva hajaandikwa kwenye barua?👿
 
You are very stupid

Hukua na sababu yoyote ya kuandika inflammatory comment Kama hiyo

Hujui kwanini alisafiri usiku tena aiku ya ijumaa…. What if ndio muda pekee alioweza kupata kufanya mambo ya kifamilia?
Shida wale wa facebook wamekimbilia huku kwahyo mtu anacomment tu bila kuifikiria ile comment yake utafikiri hana ubongo
 
Barua ya Kurugenzi ya Mawasiliano kutoka TANESCO imetaja kifo kimoja tu cha aliyekuwa DG wao na driver hatajwi. Hii ni bahati mbaya? Au watatoa notice nyingine ya driver peke yake? Au driver ni “mtu mdogo asiye na impact” na huwa hatajwi kwenye taratibu zao??

Atleast ile Taarifa kwa Umma kutok Ikulu imetambua kifo cha driver na imemtaja
 
Kupitia hizo picha inaonekana ni collision kwa nyuma..Lori limepaki barabarani pengine bila kuwasha indicators au kuweka alama kuashiria limesimama..utii wa sheria za barabarani kwa watanzania ni mdogo sana..hali ya kutokujali ni ya kiwango cha juu sana!
RIP Dereva na Eng. Gissing.
Mkuu kwa kifupi Bongo hapa kuna sisi madereva wa hovyo mno.

Nilikuwa Mbeya,kwenye Kona,kama Roho iliniambia punguza mwendo..akaja jamaa nyuma akanipita bila kuomba.

Anamaliza kona tu anakutana na gari dogo limepark si pembeni ni katikati ya barabara tunapita.

Jamaa aliuma brake nyingi sana na kukwepa uzuri upande wa pili hakukuwa na gari inakuja.

Mhusika alipark pale hakuwa na warning sign yeyote ile.

Ulizuka ugomvi mmoja mkubwa sana pale.
 
Gari za kijapani huwa ni nyepesi sana, bodi inanyambuka kama karatasi, nyepesi huwa zinapea na kukosa balance ukiwa high speed.
Defensive driving ni muhimu sana kwenye haya magari na barabara zetu pia.
Sio kwa hilo Mkuu ,mwendo mwendo na maamuzi ya hovyo.
Maisha hata angekuwa mjerumani hapo hatoki mtu.
Angalia hiyo gari nyuma ilivyobaki.
 
Hata mimi nashangaa ,wanaenda trip ndefu ili mradi wapate per diem wote ,dereva na mkurugenzi... Mfano sisi Dar es salaam unakuta tunaenda trip ya kizazi mpaka Mbeya au Mwanza na gari badala hata ya kuchukua ndege ,kote Mbeya na Mwanza kuna viwanja vizuri na route za ndege za kilq siku.
Nani atambebea begi!
===
Ni ajali.
WAlale mahala pema peponi!
 
Back
Top Bottom