TANZIA Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Gissima Nyamo-Hanga na dereva wake wafariki dunia

Aisee Land cruiser lote halifai kama karatasi vile, sijui wamepataje ajali na nimeona hapo lorry liko pembeni, uso Kwa uso Nini?. Kusema kweli wakati mwingine hata kama una haraka sana hebu tafuta sehemu ulale kwanza utulie upate utimamu tena.

Una haraka ya kwenda wapi?. Miundombinu yenyewe si mizuri sana ukihama kidogo tu tayari jua ushakufa na hasa ukikutana na wazee wa malorry aaahh umekwisha tena usiku. Kama Kuna uwezekano wa kusubiri Hadi kupambazuke basi ni Bora usubiri kukuche, inakuongezea kidogo nafasi ya kuishi.

Sisi hatujifunzi, Hadi likutokee wewe ndo unapata akili, Bado wengi tu watakufa sana Kwa vitu vidogo tu ambavyo tunavidharau tuwapo safarini.
 
Wazungu wanaamini usafiri wa ndege ni salama zaidi kuliko barabara, hivyo ni Bora viongozi kutumia ndege zaidi.
R.I.P
Kwa vigezo vipi?
Umelinganisha uingi wa magari barabarani na uingi wa ndege hewani ukaona uwiano upo sambaba?

Ni hasara kubwa kwetu sote kumpoteza mTanzania yeyote katika hali hiyo. Ni matumaini yangu kuwa yeye hakuwa mshiriki katika mpango wa kiuhayawani wa kununua umeme Ethiopia.
 
Madhambi yanayofanywa na mihimili ya Dola yanamchukuza Mungu na kwa njia hiyo Mungu anafikisha ujumbe kwa wateuliwa wengi wao wakiwa wema na endapo wenye mihiimili ya Dola wakeiendelea na maovu yao hapo ndipo Mungu anayashusha ghadhabu kwao.

GOD BLESS TANGANYIKA
 
Duuh hilo Ndinga limeteketea mbayaa, Ms zimepotea km zotee.

RIP Eng. ila Mmmh
 
Umeelezea vizuri sana hapo, safari kama hiyo lazima iwe imeandaliwa kitu kinaitwa Journey Management Plan na watu wa logistics & safety wa Tanesco, swali la kujiuliza kwa nini asafiri usiku? Je gari limefungwa mfumo wa kudhibiti mwendokasi? Ni masaa mangapi gani gari la Serikali linaruhusiwa kutembea mchana au usiku?
 
Ajali ngapi zinatokea asubuhi na mchana?
 
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU

Dar es Salaam
13 Aprili, 2025

SALAMU ZA RAMBIRAMBI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametumia salamu za rambirambi Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko kufuatia kifo cha aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika La Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Gassima Nyamo-Hanga pamoja na dereva wake Muhajir Mohamed Haule.

Marehemu Nyamo-Hanga na dereva wake wamefariki usiku wa kuamkia leo tarehe 13 Aprili, 2025 katika ajali ya gari iliyotokea katika Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara.

Rais Dkt. Samia anawapa pole Wizara ya Nishati, TANESCO, familia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Nyamo-Hanga na Haule.

Mwenyezi Mungu aziweke roho za marehemu Nyamo-Hanga na Haule mahala pema peponi, Amina.

Sharifa B. Nyanga
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu
 

Attachments

  • IMG-20250413-WA0006.jpg
    114.7 KB · Views: 29
Jana nimenusurika ajari mbili dar es salaam hapo mataa kamata na nyingine temeke kwenye junction moja zimenifikirisha Sana pia nilijikuta nimesema MUNGU WANGU sijui ILO neno lilikujaje mdomoni tukapona hivyo..

Last year tulisafiri na gari mdogo mbili kwenda mkoani msibani nilicho gundua kuendesha gari dar es salaam na kwenda route ndefu mikoani bila uzoefu ni hatare sanaa
 
wanasema dereva alimkwepa mwendesha baiskeli!nikawaza saa 7 za usiku, mwendesha baiskeli katoka wapi usiku wote huu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…